BAADA KUTISHIWA KUSHITAKIWA, LIVERPOOL YAJITOA KUMSAKA VAN DIJK!

SOUTHAMPTON-VANDIJKLiverpool wameomba radhi kwa Southampton kwa kutoelewana kokote kulikotokea wakati wao wakimsaka Beki Virgil van Dijk.

Juzi, Southampton waliwataka Wasimamiza wa EPL, LIGI KUU ENGLAND, kuichunguza Liverpool kwa kutaka kumrubuni Sentahafu wao, Virgil van Dijk, mwenye Miaka 25, kinyume cha taratibu.

Meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp, alimtaka Beki huyo wa Kimataifa wa Netherlands na Mchezaji huyo mwenyewe akadaiwa kusema anaitaka Liverpool badala ya Klabu kadhaa nyingine zilizoonyesha nia nae.

Hilo liliwafanya Southampton waamini Liverpool walienda moja kwa moja kwa Van Dijk badala ya kupitia rasmi Klabuni kwao na hivyo kuitaka EPL kuchunguza.

Jana Liverpool walitoa Taarifa rasmi ya kuomba radhi na pia kutamka sasa hawatashughulika tena kutaka kumnunua Van Dijk.

Mwaka Jana, Van Dijk alisaini Mkataba Mpya wa Miaka 6 na Southampton na Klabu hiyo ikaweka thamani yake ya kununuliwa kuwa Pauni Milioni 50 licha wao kumnunua kwa Pauni Milioni 13 kutoka kwa Celtic ya Scotland Mwaka 2015.

MCHEZAJI WA ZAMANI NEWCASTLE NA IVORY COAST, CHEICK TIOTE AFARIKI GHAFLA!

TIOTE-RIPKIUNGO wa zamani wa Klabu ya England Newcastle na Timu ya Taifa ya Ivory Coast Cheick Tiote amefariki Jana huko China akiwa Mazoezini na Klabu yake.
Habari za Kifo cha Tiote, Miaka 30, zimethibitishwa na Wakala wake Emanuele Palladino ambae Jana Jioni alitoa tamko rasmi kuwa Tiote alipoteza maisha akikimbizwa Hospitalini.
Palladino ameeleza: "Kwa huzuni kubwa nathibitisha kifo cha Mteja wangu alieanguka Mazoezini akiwa na Klabu yake Beijing Enterprises na kufariki akiwa njiani Hospitalini. Hatuwezi kusema zaidi wakati huu na tunaomba Familia yake isibuguziwe wakati huu mgumu. Tunaomba Sala zenu wote!"
Tiote alipata umaarufu mkubwa akiwa England alipoichezea Newcastle Gemu 156 katika Miaka 7 yake baada ya kuhamia hapo akitokea FC Twente ya Netherlands.
Aliihama Newcastle Februari 2017 kwenda China kujiunga na Beijing Enterprises.
Rambirambi za Kifo hiki zilimiminika kila sehemu na moja ni hii Posti ya Twitter kutoka kwa Mchezaji mwenzake, Demba Ba, waliekuwa nae Newcastle:

TIOTE-DEMBA-TWITTER

UHAMISHO ENGLAND: HEKAHEKA ZISHAANZA, PATA MCHEZAJI YUPI KENDA WAPI HADI LEO, NANI KATEMWA!

UHAMISHO-SIT-17-18WAKATI Bosi wa Manchester City Pep Guardiola akiwa wa kwanza kabisa kuchupa kwenye harakati za Uhamisho mara tu baada ya Msimu kumalizika akijiweka sawa kwa Msimu Mpya wa 2017/18 unaoanza Agosti 12 kwa kumwaga Pauni Milioni 43 kumnunua Kiungo wa AS Monaco Bernardo Silva, Klabu nyingine nazo zishaanza kuchanganya.

Akimnunua Silva, Guardiola na City yake, pia walitangaza kuwaacha Wachezaji Watano ambao ni pamoja na Pablo Zabaleta ambae amejiunga na West Ham.

Nao Chelsea, Mabingwa Wapya wa England, hawajaingia kwa kishindo kwenye Mbio hizi za Uhamisho licha kuweka wazi kuwaacha Wachezaji wao Wawili.

HADI SASA HAYA NDIO YAMEJIRI KLABU KWA KLABU:

FAHAMU: Dirisha la Uhamisho litafunguliwa rasmi Julai 1 na Kufungwa Alhamisi Agosti 31 Saa 7 Usiku, Saa za Bongo.

**LISTI HII ITAKUWA IKIONGEZWA KADRI UHAMISHO UNAPOKAMILIKA/KUTHIBITIKA [Si Uvumi!].

Brighton & Hove Albion

Ndani

Pascal Gross - Ingolstadt - Ada Haikutajwa

Josh Kerr - Celtic - Ada Haikutajwa

Burnley

Nje

Michael Kightly - Wameachwa

Joey Barton - Wameachwa

George Green - Wameachwa

R J Pingling - Wameachwa

Christian Hill - Wameachwa

Taofiq Olmowewe - Wameachwa

Jon Flanagan – Mwisho wa Mkopo, anarudi Liverpool

Chelsea

Nje

Juan Cuadrado - Juventus - Ada Haikutajwa

Christian Atsu - Newcastle United - Ada Haikutajwa

Everton

Nje

Tom Cleverly - Watford - Ada Haikutajwa

Manchester City

Ndani

Bernardo Silva - Monaco (£43million)

Nje

Pablo Zabaleta - West Ham

Gael Clichy - Wameachwa

Jesus Navas - Wameachwa

Willy Caballero - Wameachwa

Baccary Sagna - Wameachwa

Newcastle United

Ndani

Christian Atsu - Chelsea - Ada Haikutajwa

Nje

Southampton

Nje

Cuco Martina - Wameachwa

Lloyd Isgrove - Wameachwa

Harley Willard - Wameachwa

Martin Caceres - Wameachwa

Swansea

Nje

Gerhard Tremmel - Wameachwa

Marvin Emnes - Wameachwa

Liam Shephard - Wameachwa

Josh Vickers - Wameachwa

Owain Jones - Wameachwa

Tom Dyson - Wameachwa

Tom Holland - Wameachwa

Alex Samuel - Stevenage - Ada Haikutajwa

Watford

Ndani

Tom Cleverly - Everton - Ada Haikutajwa

West Ham

Ndani

Pablo Zabaleta - Manchester City

Nje

Jonathan Calleri - Deportivo Maldonado – Mwisho wa Mkopo

Gokhan Tore - Besiktas - End of loan

Alvaro Arbeloa - Wameachwa

Sam Howes - Wameachwa

Sam Ford - Wameachwa

Kyle Knoyle - Wameachwa

Sam Westley - Wameachwa

ANTONIO CONTE WA MABINGWA CHELSEA NDIE MENEJA BORA WA MSIMU – LMA!

>ATWAA KOMBE SASA LINAITWA SIR ALEX FERGUSON!

CONTE-SIR ALEX-TROPHYMENEJA wa Mabingwa Wapya wa England Chelsea, Antonio Conte, ndie ameteuliwa kuwa Meneja Bora wa Msimu wa EPL, LIGI KUU ENGLAND, na Chama cha Mameneja wa Ligi [League Managers Association].

Uteuzi huo wa Conte ulitangazwa Jumatatu Usiku kwenye Hafla ya 25 ya Chakula cha Usiku iliyofanyika huko London na kukabidhiwa Kombe ambalo sasa linaitwa SIR ALEX FERGUSON LMA-WINNERSTROPHY.

Conte, akiwa kwenye Msimu wake wa kwanza tu na Chelsea, ambayo Msimu uliopita ilimaliza Nafasi ya 10 kwenye EPL, kutwaa Ubingwa wa England.

Msimu huu, Chelsea waliweka Rekodi ya kushinda Mechi 30 za EPL zikiwemo Mechi 13 mfululizo walizoshinda kuanzia Oktoba 1 na kumaliza Ligi wakiwa Mabingwa Pointi 7 mbele ya Timu ya Pili Tottenham.

Nae Chris Hughton ametwaa Tuzo ya Meneja Bora wa Mwaka kwenye Daraja la Championship baada kuiwezesha Brighton kupanda Daraja na kutua EPL.

Kutoka Ligi 1, Meneja Bora ni Bosi wa Sheffield United Chris Wilder kwa kuisaidia Northampton kupanda Daraja na kuingia Championship.

Ligi 2, Meneja Bora ni Paul Cook baada kuiwezesha Portsmouth kutwaa Ubingwa wa Daraja hilo na kupanda.

ENGLAND: MSIMU UJAO WACHEZAJI WANAOJIANGUSHA KUSUDI ‘KIFUNGONI’!

DIVING-SIMULATIONMSIMU ujao wa Soka huko England Wachezaji wanaojiangusha kusudi Uwanjani ili kumhadaa Refa sasa watakabiliwa na Kifungo kwa mujibu wa Kanuni Mpya.

Kanuni hiyo imepitishwa Leo kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa FA, Chama cha Soka England.

Kwa mujibu wa Kanuni hiyo, kutakuwepo na Jopo maalum litakalopitia Mikanda ya Mechi kila Jumatatu kufuatia Mechi za Wikiendi na kuchambua matukio ya kujiangusha kwa makusudi ili kumhadaa Refa.

Jopo hilo maalum, ikiwa litampata na hatia kwa kauli moja Mchezaji kwa Kosa hilo, basi atakabiliwa na Kifungo.

Lakini, kwa mujibu wa Kanuni hiyo Mpya, Matukio ambayo yatachunguzwa na kushushiwa Adhabu ni yale tu ambayo yamesababisha Penati au yatasababisha Mchezaji mwingine kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu au Kadi za Njano 2 na hivyo kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.

FA imesisitiza ni kuwa yale Matukio Dhahiri ya Udanganyifu ndio yatashughulikiwa na Jopo hilo maalum.

Jopo hilo litakuwa na Watu Watatu ambao ni Refa wa zamani, Meneja wa zamani na Mchezaji wa zamani.

Ili Kanuni hii mpya ianze kutumika, pia inahitaji ridhaa za Bodi za EPL, Ligi Kuu England, Ligi za chini na Chama cha Wachezaji wa Kulipwa, PFA [Professional Footballers' Association].

Mfumo kama huu umekuwa ukitumika huko Scotland tangu 2011.

Habari MotoMotoZ