KUELEKEA DABI YA MANCHESTER: IBRA AMTIA MCHECHETO BRAVO!

IMG-20160908-WA0001Zlatan Ibrahimovic amechochea moto wa Dabi ya Manchester itakayochezwa Jumamosi Uwanjani Old Trafford kwa kumpelekea onyo Kipa mpya wa Manchester City Claudio Bravo kupitia Mtandao wa Jamii wa Facebook.
Bravo, mwenye Miaka 33 na ambae ni Nahodha wa Nchi yake Chile, alijiunga na Man City hivi karibuni kutoka Barcelona na Jumamosi anatarajiwa kukaa Golini kwa mara ya kwanza wakati City ikitua Old Trafford kuwavaa Mahasimu wao Manchester United.
Ibrahimovic, aliejiunga na Man United Msimu huu akitokea PSG na ambae ndie Mfungaji Bora wa Man United kwa sasa, aliposti Video kwenye Facebook ikiwa na kauli ya 'kumtisha' Bravo huku akionekana akifungasha Boksi lenye vifaa vya Mazoezi ili alitume kama Paseli liende Uwanja wa Etihad kwa Bravo.
Bango la Video hiyo lilikuwa na maneno: "Karibu Manchester! Hivi ni vifaa vya Mazoezi, utavihitaji. Ntakuona Jumamosi."
IMG-20160908-WA0000
 

AFCON 2017: SAFU FAINALI YAKAMILIKA, UGANDA NDANI KWA MARA YA KWANZA TANGU 1978!

AFCON2017-LOGONCHI 5 Jana zilifuzu kutinga Fainali za Mataifa ya Afrika, AFCON 2017, zirakazochezwa huko Gabon Januari 2017.
Nchi hizo ni Burkina Faso, Democratic Republic of Congo, Togo, Tunisia na Uganda.
Tano hizo zinaungana na Algeria, Cameroon, Egypt, Ghana, Guinea-Bissau, Ivory Coast, Mali, Morocco, Senegal na Zimbabwe ambazo zilifuzu awali wakiungana na Wenyeji wa Fainali Gabon kufanya Jumla ya Timu 16.
Hapo Jana, kwenye Mechi za mwisho za Makundi, Togo ilipiga Bao 5, DR Congo na Tunisis Bao 4 kila mmoja na Burkina Faso kupiga Bao la ushindi Dakika 9 kabla Mechi yao kwisha.
Lakini furaha kubwa ilikwenda kwa Uganda ambao walifanikiwa kufuzu Fainali kwa kuwa moja ya Timu ya Pili Bora 2 zilizofuzu na kwenda Fainali yao ya kwanza ya AFCON tangu 1978.
Uganda walimaliza Nafasi ya Pili nyuma ya Ghana katika Kundi lao.
Tunisia waliifunga Liberia 4-1  na kutwaa ushindi wa Kundi A wakati huko Lome Togo waliitwanga Djibouti 5-0 na kutinga kama Washindi wa Pili Bora wakiungana na Uganda.
DER Congo waliichapa Central African Republic 4-1 na kutwaa ushindi wa Kundi B.
Nao Burkina Faso, wakicheza Ugenini, walifunga Bao katika Dakika za Majeruhi, Dakika ya 99, na kushinda 2- 1 dhidi ya Botswana kwenye Nechi iliyozaa Kadi Nyekundu 3 ambazo 2 walipewa Burkina Faso lakini wakafanikiwa kuipiku Uganda na kutwaa ushindi wa Kundi D na kutinga Fainali kwa ubora wao wa uso kwa uso na Uganda.
Hata hivyo, furaha ilibaki Uganda kwani wamefuzu Fainali kama Washindi wa Pili Bora.

MAN UNITED: SCHWEINI KIKOSINI TIMU YA KUCHEZA LIGI KUU ENGLAND 2016/17!

MANUNITED-MOU-SCHWEINIKIUNGO na aliekuwa Nahodha wa Germany Bastian Schweinsteiger ni miongoni mwa Wachezaji 25 wa Manchester United ambao wamesajiliwa rasmi kwa ajili ya Ligi Kuu England, EPL, kwa Msimu huu wa 2016/17.

Schweinsteiger, mwenye Miaka 32 na ambae aliiongoza Germnay Mwaka 2014 kutwaa Kombe la Dunia huko Brazil, alitajwa na Meneja Jose Mourinho kuwa yupo kwenye hatihati kutoichezea tena Timu hiyo.

Mapema Wiki hii, Schweinsteiger alistaafu rasmi kuichezea Germany baada ya kucheza Mechi 121 na kufunga Bao 24.

Kwa mujibu wa Kanuni za EPL, Klabu zote 20 za EPL zilipaswa kupeleka Majina 25 ya Wachezaji wao.

Schweinsteiger, ambae alitua Man United Julai 2015, amekuwa hafanyi Mazoezi na Kikosi cha Kwanza tangu Mourinho aanze kazi yake.

Lakini mwenyewe ameshasema kuwa yeye yupo tayari kuichezea Man United wakati wowote ule.

+++++++++++++++++++++++++++

JE WAJUA?

-Safari hii Ligi hii ya England haina tena Jina la Mdhamini na itajulikana rasmi kama Ligi Kuu tofauti na Msimu uliopita ilipoitwa Barclays Premier League kutokana na udhamini wa Barclays.

DAIMA: www.sokaintanzania.com

+++++++++++++++++++++++++++

MAN UNITED – Kikosi kamili cha EPL: Eric Bailly, Daley Blind, Michael Carrick, Matteo Darmian, David De Gea, Memphis Depay, Sadik El-Fitouri, Marouane Fellaini, Ander Herrera, Zlatan Ibrahimovic, Sam Johnstone, Phil Jones, Jesse Lingard, Juan Mata, Henrikh Mkhitaryan, Paul Pogba, Marcos Rojo, Sergio Romero, Wayne Rooney, Morgan Schneiderlin, Bastian Schweinsteiger, Chris Smalling, Antonio Valencia, Ashley Young

EPL kwa sasa ipo Mapumzikoni kupisha Mechi za Kimataifa kwa Wiki 2 na Mechi inayofuata ni Manchester Dabi kati ya Man United na Man City ndani ya Old Trafford.

LIGI KUU ENGLAND

Msimu Mpya 2016/17

Ratiba:

**Saa za Bongo

Jumamosi Septemba 10

1430 Man United v Man City                

1700 Arsenal v Southampton                

1700 Bournemouth v West Brom           

1700 Burnley v Hull          

1700 Middlesbrough v Crystal Palace               

1700 Stoke v Tottenham             

1700 West Ham v Watford          

1930 Liverpool v Leicester          

Jumapili Septemba 11

1800 Swansea v Chelsea   

Jumatatu Septemba 12

2200 Sunderland v Everton          

PAUL MERSON AMSHANGAA WENGER ‘KUMTOSA’ JACK WILSHERE!

JACK-WILSHEREPaul Merson, Mchezaji wa zamani wa Arsenal ambae sasa ni Mchambuzi, ameshangaa jinsi Jack Wilshere alivyotoswa kwenda Bournemouth kwa Mkopo wa Msimu Mzima.

Merson, ambae kama Wilshere, alikuwa Kiungo mahiri, anaamini Mchezaji huyo Msimu huu angeibeba sana Arsenal na ametoboa kuwa Meneja wa Arsenal Arsene Wenger atajutia uamuzi huu.

Merson ameeleza: “Nimestushwa na uamuzi huu. Huu ni Msimu mrefu mno. Arsenal wapo kwenye Mashindano Manne na hawana Mtu kama Jack Wilshere kwenye Timu yao!”

Aliongeza: “Kama upo 1-0 nyuma na zimebaki Dakika 10 nani utamuingiza, Theo Walcott, Alex Oxlade-Chamberlain au Jack Wilshere?”

"Jack Wilshere ndie ambae anaweza kupigana kupangua Difensi ya Mtu 11!”

Merson amekiri uamuzi huo wa Wenger ni wazi utamuumiza Wilshere, mwenye Miaka 24, ambae alikuwepo Arsenal tangu ana Miaka 9, na hilo litamfanya aichukie Arsenal ya Wenger.

Merson ameeleza: “Enzi zetu unaenda kwa Mkopo Mwezi Mmoja au Miwili Mitatu. Mwaka mmoja ni mrefu. Nani anajua kuwa anaweza kuwa Mchezaji Bora wa Mwezi wa Ligi wakati Arsenal imefungwa Gemu mbili wakikumbuka wamemruhusu Wilshere aondoke Mwaka?”

Merson alimalizia: “Wasiwasi wangu ni kuwa mapenzi yake kwa Arsenal yatapotea. Anaweza akafikiria hili na kujiuliza, kwanini mimi nimepelekwa Mkopo?”

ARSENAL KUMRUHUSU WILSHERE KUONDOKA KWA MKOPO

WILSHEREArsenal wako tayari kumruhusu Kiungo wao wa England Jack Wilshere kuondoka kwenda kuchezea Klabu nyingine kwa Mkopo.
Wilshere, mwenye Miaka 24, amekuwa akikumbwa na majeruhi ya mara kwa mara kiasi cha Msimu uliopita kuichezea Arsenal Mechi 3 tu baada ya kuvunjika Mguu wa Kushoto.
Baada ya Msimu huo kwisha, Wilshere aliichezea England Mechi 6 zikiwemo Mechi 3 za kwenye Fainali za EURO 2016 huko France Mwezi Juni na Julai.
Lakini Jana hakuwemo kwenye Kikosi cha England cha Wachezaji 23 kilichotangazwa na Meneja mpya Sam Allardyce kwa ajili ya Mechi zao za Kundi F la kuwania kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia.
Kwa ajili ya Msimu huu mpya, Arsenal ililipa Pauni Milioni 35 kumnunua Kiungo wa Switzerland Granit Xhaka.
Wilshere, ambae ameichezea England mara 34 na Gemu 80 za Ligi Kuu England akiwa na Arsenal, ameingizwa Gemu 2 tu za Ligi Msimu huu akitokea Benchi kuichezea Arsenal.
Mwaka 2010, Wilshere aliwahi kwenda Bolton Wanderers kucheza kwa Mkopo.
Wilshere ana muda hadi kesho Usiku kuamua wapi aende kwa Mkopo kabla Dirisha la Uhamisho kufungwa rasmi.