POLISI WAMKIMBIZA VALENCIA WAKIWANIA KUMNASA ALIPOBADILISHWA UWANJANI KWENYE MECHI!

ENNER-VALENCIAJANA huko Quito, Nchini Ecuador, kumepotea tukio la kushangaza pale Mchezaji wa Ecuador Enner Valencia alipokimbizwa na Polisi wakitaka kumkamata mara tu baada ya kubadilishwa Uwanjani wakati wa Mechi ya Kanda ya Nchi za Marekani ya Kusini za kuwania kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia.

Kwenye Mechi hiyo ambayo Ecuador iliifunga 3-0 Chile, Enner Valencia anaechezea Everton huko England akiwa kwa Mkopo kutoka West Ham, alibadilishwa kwenye Dakika ya 82 alipopata matatizo ya kupumua kutokana na Quito kuwa juu sana toka Usawa wa Bahari na alipokuwa akitolewa Uwanjani kwenye Kigari cha Machela huku akiwekewa Chombo cha Kupumua Usoni, Polisi wapatao 12 walikifukuza Kigari hicho ili kumkamata kutokana na Amri ya Mahakama.

Inasemekana Mchezaji huyo alikuwa akipuuza Amri ya Mahakama ya kulipa matunzo ya kila Mwezi ya Binti yake wa Miaka Mitano waliozaa na Sharon Valencia, ambae wametengana, kiasi ambacho kinadaiwa kuwa ni Pauni 13,000.

Polisi hao walishindwa kumnasa Mchezaji huyo ambae aliingizwa kwenye Ambulensi na kupelekwa Hospitali.

Awali kabla Mechi hiyo, Polisi walifika kwenye Kambi ya Timu ya Taifa ya Ecuador lakini walishindwa kumkamata.

Hata hivyo, imedaiwa kuwa hivi sasa Amri hiyo ya kukamatwa imefutwa lakini mmoja wa Wanasheria wa Mama wa Mtoto wa Valencia, Paul Marin, alisikitishwa na kitendo cha Polisi wa Nchi yao kushindwa kumkamata Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Nchi hiyo aliepuuza Amri halali ya Mahakama ya Nchi.

Kwenye Mechi hiyo na Chile Bao hizo 3 za Ecuador zilifungwa na Staa wa Manchester United Antonio Valencia, Cristian Ramirez na Felipe Caicedo.

Hivi sasa Enner Valencia yuko shwari Kambini mwa Ecuador ambayo Jumanne ijayo itacheza na Bolivia.

RASHFORD ATAKUWA SUPASTAA!

RASHFORD-ROONEYKEPTENI wa Manchester United na England Wayne Rooney ameeleza kuwa Chipukizi Marcus Rashford atapanda chati na kuwa Supastaa mwenye Jina kubwa kwenye Soka.
Rashford, mwenye Miaka 18, ameibuka na kupanda juu haraka mno baada ya Meneja aliepita wa Man United Louis van Gaal kumpa nafasi kucheza kwa mara ya kwanza Timu ya Kwanza kwenye UEFA EUROPA LIGI dhidi ya Midtjylland Mwezi Februari.
Kwenye Gemu hiyo Kijana huyo akapiga Bao 2 na Siku 3 baadae, kwenye Mechi yake ya kwanza ya EPL, Ligi Kuu England dhidi ya Arsenal akapiga tena Bao 2.
Tangu wakati huo Rashford amekuwa ni moto kwenye Mechi zote anazochezeshwa.
Ingawa Rooney amekiri bado Staa huyo hajakomaa lakini amebainisha uwezo na kipaji chake kitamfikisha mbali.
Rooney ameeleza: "Marcus anafanya vizuri. Ni Kijana mdogo mwenye mvuto mkubwa Duniani hivi sasa. Nina hakika akiendelea kufanya bidii na kukua basi atakuwa Supastaa Miaka ijayo!"
Radhford alikuwemo kwenye Kikosi cha England kilichokuwa Fainali za EURO 2016 huko France Juni na Julai chini ya Kocha Roy Hodgson lakini alipokuja Sam Allardyce na kuisimamia England Mechi 1 tu hakuitwa.
Badala yake Rashford akachukuliwa England U-21, chini ya Gareth Southgate, na yeye kupiga Hetitriki kwenye ushindi dhidi ya Norway.
Radhford sasa amerejeshwa tena England ambayo sasa ipo chini ya Meneja wa muda Gareth Southgate na Jumamosi itacheza na Malta kwenye Mechi ya Kundi lao la Nchi za Ulaya zinazosaka kwenda Russia Mwaks 2018 kucheza Fainali za Kombe la Dunia huku Rashford akitabiriwa sana kuanza Mechi hiyo.
Hivi sasa Rashford pia yumo Kikosi cha Kwanza cha Man United chini ya Meneja Jose Mourinho na kumfanya Rooney asugue Benchi.
Rooney amenena: "Ni muhimu Wachezaji chipukizi wanaofurahisha wazawadiwe wakistahili na nadhani anastahili!"

EPL: BAO LA ‘MKONO’ DAKIKA YA 93 LAWAPA USHINDI ARSENAL!

EPL - LIGI KUU ENGLAND

Ratiba/Matokeo:

Jumapili 2 Oktoba 2016

Man United 1 Stoke 1       

Leicester 0 Southampton 0         

Tottenham 2 Man City 0             

Burnley 0 Arsenal 1

++++++++++++++++++++++++

BURNLEY0ARSENAL1-BAO-MKONOBAO la Dakika ya 93 linalosadikiwa kuwa ni la mkono limewapa ushindi wa 1-0 Arsenal walipocheza Ugenini huko Turf Moor na Burnley.

Bao hilo lilitokana na Kona ya Mesut Ozil na Theo Walcott kupiga Kichwa na kumkuta Alex Oxlade-Chamberlain ambae alirejesha Mpira Golini na kumgonga Mkononi Laurent Koscielny na kutinga.EPL-OKT1C

Mbali ya kuwa ni Mkono, Bao hilo pia limezua utata wa Ofsaidi kwa Laurent Koscielny wakati Mpira ukimgonga na pia Dakika za Nyongeza 2 kumalizika wakati linafungwa.

Ushindi huu umewaweka Arsenal Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 4 nyuma ya Vinara Man City.

VIKOSI:
Burnley: Heaton, Lowton, Keane, Mee, Ward, Gudmundsson, Hendrick, Marney, Defour, Boyd, Vokes.
Akiba: Flanagan, Kightly, Bamford, Robinson, Tarkowski, Arfield, O’Neill.
Arsenal: Cech, Bellerin, Mustafi, Koscielny, Monreal, Xhaka, Cazorla, Walcott, Ozil, Iwobi, Sanchez.
Akiba: Gibbs, Gabriel, Ospina, Oxlade-Chamberlain, Holding, Reine-Adelaide, Elneny.
REFA: Craig Pawson

EPL - LIGI KUU ENGLAND

**Saa za Bongo

Jumamosi 15 Oktoba 2016

1430 Chelsea v Leicester            

1700 Arsenal v Swansea             

1700 Bournemouth v Hull           

1700 Man City v Everton            

1700 Stoke v Sunderland            

1700 West Brom v Tottenham               

1930 Crystal Palace v West Ham           

Jumapili 16 Oktoba 2016

1530 Middlesbrough v Watford             

1800 Southampton v Burnley                

Jumatatu 17 Oktoba 2016

2200 Liverpool v Man United      

BAADA USHINDI MNONO ULAYA JUVE, NAPOLI WIKIENDI KUKIMBIZANA SERIE A

SERIEA-JUVEJuventus na Napoli wanarudi kwenye Ligi yao ya Italy ya Serie A baada kuzoa ushindi mnono kwenye Makundi yao ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI Juzi Kati-Wiki.

Juve, Mabingwa Watetezi wa Serie A, Jumapili wapo Ugenini kucheza na Empoli baada ya Juzi kuitwanga Dinamo Zagreb 4-0 Ugenini kwenye Mechi yao ya Kundi H la UCL na kupaa kileleni.

Juve, chini ya Kocha Massimiliano Allegri, wakiwa na ‘Wauuaji’ wa Zagreb Miralem Pjanic, Gonzalo Higuain, Paulo Dybala na Dani Alves, hawategemewi kupoteza Pointi huko Empoli na ushindi utawabakiza kileleni mbele ya Napoli.

Hiyo hiyo Jumapili Napoli wapo Ugenini kuivaa Atalanta huko Bergamo na Kocha wao Sarri ameonya licha ya Juzi kuwafunga Benfica kwenye UCL sasa mtihani wao ni Atalanta.

SERIE A

Ratiba

Jumamosi Oktoba 1

1900 Pescara v Chievo

2145 Udinese v Lazio

Jumapili Oktoba 2

1330 Empoli v Juventus

1600 Atalanta v Napoli

1600 Bologna v Genoa

1600 Cagliari v Crotone

1600 Sampdoria v Palermo

1600 AC Milan v Sassuolo

1600 Torino v Fiorentina

2145 Roma v Inter Milan

LIGI ENGLAND KUPATA VAKESHENI DESEMBA!

EPL-LogosENGLAND inaelekea kusalimu amri na kutoa Mapumziko kwa Ligi zao kwa Mwezi Desemba kama zilivyo Ligi nyingine kubwa za huko Ulaya.
Wakati Nchi kama Spain, Italy na Germany zikisitisha Ligi zao, za La Liga, Serie A na Bundesliga, katika Majira ya Baridi katika kipindi cha Krismasi na Mwaka Mpya, utamaduni wa England umekuwa kupuyanga Mechi mfululizo kwa kipindi hicho kitu ambacho kimetambuliwa kuathiri Timu zao kwenye Mashindano ya Kimataifa.
Sasa Mkuu wa Ligi, Shaun Harvey, amedokeza mabadiliko kadhaa kwenye mfumo wao wa Soka ili kutoa nafasi kwa Ligi zao kwenda Vakesheni ya Majira ya Baridi.
Mabadiliko hayo yataikumba FA CUP ambapo Mechi za Marudiano baada ya Sare zitafutwa na Mechi za Raundi za 4 na 5 zitachezwa Kati Wiki badala ya Wikiendi.
Harvey amesema mabadiliko hayo yatatoa mwanya kwa Gemu nyingi za Ligi na pia kuzalisha Fedha zaidi hasa za kuzisaidia Timu za Madaraja ya chini ambapo Daraja la Championship litapunguzwa Timu 4.
Huko nyuma, FA CUP iliondoa Marudiano kwenye Nusu Fainali kuanzia 1999 na kuanzia Msimu huu hamna Marudiano kwenye Raundi ya 6 ikimaanisha Mechi za Raundi hiyo Mshindi lazima apatikane Siku hiyo hiyo.
Mabadiliko hayo yashakubalika na yako kwenye mchakato wa kupitishwa na kupigiwa Kura mwishoni mwa Msimu huu.