CITY YAKIRI KOSA LA KUKIUKA SHERIA ZA MADAWA HARAMU, NAE PAPY DJILOBODJI ‘JELA’ MECHI 4!

ETIHAD-SITWAKATI Klabu ya Manchester City wakikiri kukiuka Sheria za Kuzuia Matumizi ya Madawa Haramu, Mchezaji wa Sunderland Papy Djilobodji amefungiwa Mechi 4 kwa kosa la kucheza kwa fujo.

CITY NA MADAWA

Manchester City walifunguliwa Mashitaka na FA, Chama cha Soka England, hapo Januari 12 kwa Kosa la kukiuka Sheria za Kuzuia Matumizi ya Madawa Haramu na hii Leo wameamua kukubali kosa lao.

Waliposhitakiwa, ilidaiwa City walishindwa kuwapa Taarifa sahihi Maafisa wanaopima Wachezaji Matumizi ya Madawa Haramu.

Kila Klabu hupaswa kujulisha Wachezaji wao watakuwa wapi kwa ajili ya kupimwa lakini City walishindwa kutoa Taarifa za Ratiba ya Mazoezi na wapi Wachezaji hao watapatikana baada ya Mazoezi ili Maafisa wanaohusika wajue wakati wote wapi watawapata wakitakiwa kupimwa.

Imedaiwa City ilishindwa mara 3 kupeleka Taarifa za waliko Wachezaji wao na ndio maana FA ikawashitaki.

Kawaida kosa kama hilo huadhibiwa kwa Faini.

PAPY DJILOBODJI ‘JELA’ MECHI 4!

Beki wa Sunderland Papy Djilobodji amefungiwa Mechi 4 baada ya kukutwa na hatia ya kucheza kwa fujo.

Beki huyo mwenye Miaka 28 alipinga Kosa lake ilipodaiwa alimpiga Usoni kwa Mkono Mchezaji wa West Bromwich Albion Darren Fletcher wakati Timu yake ikichapwa 2-0 Jumamosi iliyopita kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England.

Tukio hilo halikuonwa na Waamuzi wa Mechi hiyo na kupitiwa na Jopo Huru ambalo sasa limeridhika ni Kosa lililostahili Kadi Nyekundu.

Papy Djilobodji, Mchezaji kutoka Senegal, atafungiwa Mechi 4 badala ya 3 kwa vile Novemba 19 pia alitolewa nje kwa Kadi Nyekundu kwenye Mechi ya Sunderland na Hull City.

Mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea sasa atazikosa Mechi za Sunderland dhidi ya Tottenham hapo Januari 31 ikichezwa Nyumbani, na nyingine ni na Crystal Palace, Ugenini, Southampton, Nyumbani, na Everton, Ugenini.

Kukosekana huku kwa Papy Djilobodji ni pigo kwa Sunderland ambao wako mkiani mwa EPL.

ARSENE WENGER KUYAKUBALI MASHITAKA YA FA, SASA KIFUNGO KINAMNGOJA!

WENGER-RC-ASUKUMA-REFAArsene Wenger amethibitisha kuwa atakubali Mashitaka ya FA, Chama cha Soka England, ya Utovu wa Nidhamu yaliyotokana kumkashifu Refa na pia kumsukuma Refa wa Akiba baada ya kuamriwa kutoka nje ya Uwanja na Refa.

Jumapili iliyopita kwenye Mechi ambayo Arsenal iliifunga Burnley 2-1, Wenger alimsukuma Refa wa Akiba Anthony Taylor mara tu baada ya kuamriwa na Refa wa Mechi hiyo Jon Moss kutoka nje ya Uwanja kwa kumkashifu ikidaiwa alimwita ‘laghai’.

Wenger alitupwa nje ya Uwanja Dakika ya 93 mara baada ya Burnley kupewa Penati ambayo walisawazisha Bao na Gemu kuwa 1-1 lakini Dakika chache baadae Refa huyo huyo, Jon Moss, ndie aliwapa Arsenal Penati tata na kufunga Bao lao la ushindi katika Dakika ya 98.

Mara baada ya Mechi hiyo, Wenger, mwenye Miaka 67, aliungama na kuomba radhi.

FA ilimpa hadi Leo Alhamisi Saa 3 Usiku, Saa za Bongo, kujibu Mashitaka yake.

Sasa Wenger amesema hatapinga Mashitaka hayo na kuiachia FA impe Adhabu.

Mwaka 2012, Meneja wa Newcastle wakati huo, Alan Pardew, alitwangwa Faini Pauni 20,000 na kufungiwa Mechi 2 kwa kumsukuma Refa Msaidizi, Mshika Kibendera.

Akiongea hapo Jana, Wenger alieleza: “Nipo England kwa Miaka 20 na nimeona mengi na nyinyi mnajua.”

Alipohojiwa kuhusu Adhabu anayotegemewa kupewa, Wenger alisema: “Sitegemei kitu. Niliongea baada ya Mechi ile.”

Licha ya kutoboa kwamba atakubali Mashitaka, Wenger pia alisema ataomba yeye mwenyewe aende kujieleza mbele ya Jopo litakalojadili Kesi yake.

WENGER KWA PILATO FA KWA KUMKASHIFU REFA NA KUMSUKUMA REFA WA AKIBA!

>>MAREFA WASTAAFU WATAKA AFUNGIWE SI CHINI MECHI 6!

WENGER-RC-ASUKUMA-REFAFA, Chama cha Soka England, kimemfungulia rasmi Mashitaka ya Utovu wa Nidhamu Meneja wa Arsenal Arsene Wenger kwa madai ya kumkashifu Refa na pia kumsukuma Refa wa Akiba.

Jumapili, kwenye Mechi ambayo Arsenal iliifunga Burnley 2-1, Wenger alimsukuma Refa wa Akiba Anthony Taylor mara tu baada ya kuamriwa na Refa wa Mechi hiyo Jon Moss kutoka nje ya Uwanja kwa kumkashifu ikidaiwa alimwita ‘laghai’.

Wenger alitupwa nje ya Uwanja Dakika ya 93 mara baada ya Burnley kupewa Penati ambayo walisawazisha Bao na Gemu kuwa 1-1 lakini Dakika chache baadae Refa huyo huyo, Jon Moss, aliekuwa mbaya ndie aliwapa Arsenal Penati tata na kufunga Bao lao la ushindi katika Dakika ya 98.

Mara baada ya Mechi hiyo, Wenger, mwenye Miaka 67, aliungama na kuomba radhi.

Lakini Leo, FA imetoa tamko rasmi la kumfungulia Mashitaka ya Utovu wa Nidhamu na kumpa hadi Alhamisi Saa 3 Usiku, Saa za Bongo, kujibu Mashitaka yake.

Mwaka 2012, Meneja wa Newcastle wakati huo, Alan Pardew, alitwangwa Faini Pauni 20,000 na kufungiwa Mechi 2 kwa kumsukuma Refa Msaidizi, Mshika Kibendera.

Lakini, hii Leo, Marefa Wastaafu wa England, akiwemo Keith Hackett na Howard Webb, wamekuja juu na kutaka itolewe Adhabu kali kwa Wenger kwa Kifungo kisichopungua Mechi 6 ili kuwa Onyo kali kwamba Marefa hawaguswi.

EPL – Ligi Kuu England

Ratiba

**Saa za Bongo

[Zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku isipokuwa inapotajwa]

Jumanne Januari 31

Arsenal v Watford            

Bournemouth v Crystal Palace               

Burnley v Leicester City              

Middlesbrough v West Bromwich Albion          

Sunderland v Tottenham Hotspur          

Swansea City v Southampton               

2300 Liverpool v Chelsea            

Jumatano Februari 1

West Ham United v Manchester City               

2300 Manchester United v Hull City                

2300 Stoke City v Everton 

Jumamosi Februari 4

1530 Chelsea v Arsenal               

1800 Crystal Palace v Sunderland          

1800 Everton v Bournemouth               

1800 Hull City v Liverpool           

1800 Southampton v West Ham United           

1800 Watford v Burnley              

1800 West Bromwich Albion v Stoke City         

2030 Tottenham Hotspur v Middlesbrough                

Jumapili Februari 5

1630 Manchester City v Swansea City             

1900 Leicester City v Manchester United           

VAN GAAL ASTAAFU SOKA!

MANUNITED-VANGAAL-BAIBAIBOSI wa zamani wa Manchester United na Timu ya Taifa ya Netherlands Louis van Gaal ameamua kustaafu Ukocha baada ya kuwemo kwenye kibarua hicho kwa Miaka 26.

Van Gaal, mwenye Miaka 65, amekuewa hana kazi tangu atimuliwe na Man United Mwezi Mei 2016 mara tu baada ya kuiwezesha Klabu hiyo kutwaa FA CUP.

Habari za kustaafu kwa Van Gaal zimechomoza kwenye Gazeti la huko Netherlands, De Telegraaf, ambalo lilimnukuu akisema: “Nilidhani nitaacha nilipotoka Man United, kisha nikasema ngoja nipumzike lakini sasa naona sitarejea tena Ukocha!”

Uamuzi huo umekuja mara tu baada ya kupokea Tuzo ya Utumishi uliotukuka toka kwa Serikali ya Netherland.

Mbali ya Man United, Van Gaal pia aliwahi kuwa na Klabu za Ajax, Barcelona, Bayern Munich na AZ.

VAN GAAL – Tuzo kubwa Maishani mwake:

Ubingwa: Ajax (1993-94, 1994-95, 1995-96), Barcelona (1997-98, 1998-99), AZ Alkmaar (2008-09), Bayern Munich (2009-10)

UEFA CHAMPIONZ LIGI: Ajax (1994-95)

Uefa Cup: Ajax (1991-92)

FA Cup: Manchester United (2015-16)

EPL: EVERTON YAICHAKAZA MAN CITY!

EPL – Ligi Kuu England

Ratiba/Matokeo:

**Saa za Bongo  

Jumapili Januari 15

Everton 4 Manchester City 0

1900 Manchester United v Liverpool

+++++++++++++++++++++

EPL-SOKATAMU-SITEVERTON Leo huko Goodison Park imewaonyesha Manchester City kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England, kwa kuwatandika Bao 4-0 kipigo ambacho ni kibaya mno kwa Meneja wa City katika himaya yake kwenye Mechi za Ligi.

City walikuwa nyuma 1-0 hadi Haftaimu kwa Bao la Romelu Lukaku la Dakika ya 34.

Kipindi cha Pili Everton wakatandika Bao nyingine 3 katika Dakika 47, 79 na 90 Wafungaji wakiwa Kevin Mirallas na Chipukizi Tom Davies na Ademola Lookman.

Matoke ohayo yamewaacha City wakiwa Nafasi ya 5 na Everton wakiwa Nafasi ya 7.

Mechi inayofuata kwa City ni Jumamosi ijayo wakiwa kwao Etihad kucheza na Timu ngumu Tottenham Hotspur wakati Everton wako Ugenini huko Selhurst Park kucheza na Crystal Palace.

VIKOSI VILIVYOANZA:

EVERTON: Robles, Holgate, Ashley Williams, Funes Mori, Coleman, Davies, Barry, Baines, Barkley, Mirallas, Lukaku

Akiba: Schneiderlin, Jagielka, Lennon, McCarthy, Valencia, Stekelenburg, Lookman.

MAN CITY: Bravo, Sagna, Otamendi, Stones, Clichy, Zabaleta, Touré, Silva, De Bruyne, Sterling, Agüero

Akiba: Kolarov, Caballero, Jesus Navas, Delph, Sané, Iheanacho, García.

REFA: Mark Clattenburg.

EPL – Ligi Kuu England

Ratiba

**Saa za Bongo  

Jumamosi Januari 21

1530 Liverpool v Swansea City    

1800 Bournemouth v Watford               

1800 Crystal Palace v Everton              

1800 Middlesbrough v West Ham United

1800 Stoke City v Manchester United    

1800 West Bromwich Albion v Sunderland       

2030 Manchester City v Tottenham Hotspur     

Jumapili Januari 22

1500 Southampton v Leicester City       

1715 Arsenal v Burnley     

1930 Chelsea v Hull City    

Habari MotoMotoZ