UHAMISHO WA PEDRO MASHAKANI: BARCA, MAN UNITED ZAVUTANA ADA YAKE!

PEDRO-MASHAKANIWIKI hii ilitarajiwa Dili ya Uhamisho wa Fowadi wa Barcelona Pedro kutoka Barcelona kwenda Manchester United kukamilika lakini imechelewa kutokana na mvutano kuhusu malipo ya Ada yake.

Juzi, Pedro, mwenye Miaka 28, ndie aliefunga Bao la ushindi wakati Barca inaichapa Sevilla Bao 5-4 huko Tbilisi, Georgia na kutwaa UEFA Super Cup na ilitegemewa mara baada ya Mechi hiyo atahamia Old Trafford.

Lakini sasa imedaiwa upo mvutano ambapo inasemekana Man United haitaki kulipa Dau lote la Pauni Milioni 21.3 kwa mkupuo na badala yake wanataka kulipa Pauni Milioni 17.7 mbele na kisha kulipa polepole Pauni Milioni 3.6 zikiwa nyongeza ambazo zitaendana na mafanikio atakayopata Mchezaji huyo akiwa na Man United.

Lakini Barca imegoma na inataka Ada yote kamili ilipwe mara moja.

Wachambuzi wanahisi kuwa uchelewesho huu unaweza kutoa mwanya kwa Man City na Chelsea kuwazunguka Man United na kumnunua Fowadi huyo licha ya kuwa ameshaafikiana maslahi yake binafsi na Man United na pia upo uwezekano akabakia Barca kwani Klabu hiyo inamuuza shingo upande kutokana na matakwa ya Mchezaji mwenyewe.

Mwenyewe Pedro hataki kubaki Barca ambako anasugua Benchi licha ya Jana kuanza Mechi ya Kwanza ya Supercopa Barca walipotwanga 4-0 na Athletic Bilbao huko Estadio San Mamés.

Chini ya Kocha Luis Enrique, Pedro anabaki kuwa chaguo la 4 nyuma ya Mafowadi wengine, Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar, wakati Barca wakicheza Mechi.

XHERDAN SHAQIRI RASMI ATUA STOKE KWA DAU LA REKODI YA KLABU!

SHAQIRIStoke City wamekamilisha kumsaini Winger wa Inter Milan Xherdan Shaqiri kwa Dau la Pauni Milioni 12 ambalo ni Rekodi kwa Klabu yao.

Dau kubwa ambalo Stoke wamewahi kulipa kumnunua Mchezaji ni Mwaka 2011 walipolipa Pauni Milioni kumnunua Peter Crouch kutoka Tottenham.

Jumapili, wakati Stoke City inachapwa 1-0 na Liverpool kwenye Mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu England, Shaqiri, Mchezaji wa Kimataifa wa Uswsisi mwenye Miaka 23 alikuwepo Uwanjani Britannia kushuhudia Mechi hiyo.

Shaqiri anakuwa Mchezaji wa 9 kusainiwa na Stoke, ambayo iko chini ya Meneja Mark Hughes, katika Kipindi hiki.

Shaqiri alijiunga na Inter Milan kutoka kwa Mabingwa wa Germany Bayern Munich Mwezi Januari na kuifungia Bao 3 katika Mechi 20 na pia kuipigia Nchi yake Uswisi Mabao 17.

Stoke City-Wachezaji wengine waliowasaini kabla Msimu huu kuanza:

Moha El Ouriachi (Barcelona)

Joselu (Hannover 96)

Shay Given (Aston Villa)

Philipp Wollscheid (B Leverkusen)

Jakob Haugaard (FC Midtjylland)

Marco van Ginkel (Chelsea - loan)

Glen Johnson (Liverpool)

Ibrahim Afellay (Barcelona)

+++++++++++++++++++++++

LIGI KUU ENGLAND

RATIBA:

**Saa za Bongo

Ijumaa Agosti 14

2145 Aston Villa v Man United     

Jumamosi Agosti 15

1445 Southampton v Everton         

1700 Sunderland v Norwich            

1700 Swansea v Newcastle             

1700 Tottenham v Stoke                 

1700 Watford v West Brom             

1700 West Ham v Leicester            

Jumapili Agosti 16

1530 Crystal Palace v Arsenal        

1800 Man City v Chelsea                 

Jumatatu Agosti 17

2200 Liverpool v Bournemouth        

KEPTENI LAZIO NJIANI OLD TRAFFORD?

LUCAS-BIGLIAWAKATI tayari kuna habari makubaliano ya Fowadi wa Barcelona Pedro kuhamia Manchester United yamekamilika, zipo ripoti nyingine zinadai Kepteni wa Lazio ya Italy Lucas Biglia ameafika Mkataba wa Miaka Minne Klabu hiyo ya England.

Ripoti hizo, ambazo chanzo chake ni Wasambaza Habari wa France Le10sport.com, zimedai Kiungo huyo alishaafikiana maslahi yake binafsi na Man United na kilichobaki ni Klabu husika kukubaliana Ada ya Uhamisho.

Imedaiwa Man United imetoa Ofa ya Pauni Milioni 17 lakini Lazio wanataka Pauni Milioni 25 kwa Kiungo huyo mwenye Miaka 29.

Kuhusu Pedro, inasemekana Man United na Barcelona tayari wana makubaliano ila Barca wanataka Fowadi huyo abakie kwao hadi wamalize kucheza na Sevilla kwenye Fainali ya UEFA SUPER CUP itakayochezwa Jumanne huko Tbilisi, Georgia.

Klabu hizo mbili zimekubaliana Ada ya Uhamisho ya Pauni Milioni 18.1 ambayo itapanda kwa Pauni Milioni 4.2 kutokana na Bonasi mbalimbali za mafanikio ya Fowadi huyo.

Ikiwa Pedro na Biglia watatua Old Trafford basi Wachezaji hao watafanya Man United iwe imepata Wapya 7 katika kipindi hiki kuelekea Msimu mpya kufuatia kusainiwa Memphis Depay, Matteo Darmian, Morgan Schneiderlin, Bastian Schweinsteiger na Sergio Romero.

MECHI ZA MAN UNITED:

LIGI KUU ENGLAND

Agosti 14 [Saa 2145]: Aston Villa [Villa Park]

UEFA CHAMPIONZ LIGI

Agosti 18 [Saa 2145]: Man United v Club Brugge

LIGI KUU ENGLAND

Agosti 22 [Saa 1445]: Newcastle United [Old Trafford]

UEFA CHAMPIONZ LIGI

Agosti 26 [Saa 2145]:  Club Brugge v Man United

LIGI KUU ENGLAND

Agosti 30 [Saa 1800]: Swansea City [Liberty Stadium]

HADI SASA-UHAMISHO WA WACHEZAJI 8 BORA BEI CHEE, ENGLAND!

SERGIO-ROMEROWACHAMBUZI huko England wameibuka na kutaja Uhamisho Bora wa Wachezaji katika kipindi hiki ambao hawakugharimu hata Senti moja.

IFUATAYO NI ORODHA YA WACHEZAJI HURU 8 BORA WALIOHAMA BILA KULIPWA ADA YA UHAMISHO:

8. Sergio Romero: Sampdoria kwenda Man United

-Sampdoria ilibidi imruhusu Romero, mwenye Miaka 28, kuhama kama Mchezaji Huru baada ya Mkataba wake kumalizika.

-Ni Kipa mwenye Kipaji aliecheza Dakika 458 kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil Mwaka Jana bila kufungwa Bao na kuifikisha Argentina Fainali.

7. Glen Johnson: Liverpool kwenda Stoke

Johnson atafikisha Miaka 31 lakini Stoke hawakusita kumsaini.

GLEN-JOHNSON

6. Ibrahim Afellay: Barcelona kwenda Stoke

-Ni Kiungo Mshambuliaji aliezichezea Barcelona na Schalke na pia Timu ya Taifa ya the Netherlands mara 50 lakini majeruhi yalimfanya asijenge jina huko Spain.

IBRAHIM-AFFELAY
5. Youssouf Mulumbu: West Brom kwenda Norwich

-Meneja wa Norwich, Alex Neil, amekiri wamekula bingo kumchota Mulumbu kama Mchezaji Huru hasa baada ya kuichezea zaidi ya Mechi 200 West Brom kama Kiungo mahiri.

MULUMBU
4. Tom Cleverley: Man United kwenda Everton

-Everton wamemsaini Tom Cleverley kutoka Man United kama Mchezaji Huru baada ya kuwa kwa Mkopo Msimu uliopita huko Aston Villa.

cleverley

3. Micah Richards: Man City kwenda Aston Villa

-Msimu uliopita Micah Richards alikuwa kwa Mkopo huko Italy kwenye Klabu ya Serie A Fiorentina.

richards
2. Andre Ayew: Marseille kwenda Swansea

-Ni Mtoto wa Lejendari wa Ghana, Abedi Pele, mwenye Miaka 25 ambae ameichezea Ghana kwenye Fainali 2 za Kombe la Dunia na pia kuwahi kushinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ghana.

ayew

1. James Milner: Man City kwenda Liverpool

-Baada ya kutwaa Mataji kadhaa huko Etihad akiwa na Man City, Milner ametua Liverpool bila kugharimu hata senti moja.

JAMES-MILNERSZCZESNY AKOPESHWA AS ROMA, YOUNG KUTUA SPURS?

Wojciech-SzczesnyWAKATI Kipa wa Arsenal Wojciech Szczesny amejiunga na moja ya Vigogo wa Italy, Klabu ya AS Roma , kwa Mkopo wa Msimu mmoja, zipo habari zilizozagaa huko London kuwa Tottenham Hotspur inamtaka Winga wa Manchester United, Ashley Young.
SZCZESNY AKOPESHWA AS ROMA
Msimu uliopita, Szczesny, mwenye Miaka 25, alipoteza namba kwa David Ospina na Msimu huu Arsenal imejiimarisha kwenye safu ya Kipa kwa kumnunua Mwezi uliopita Kipa kutoka Chelsea Petr Cech.
Szczesny, Kipa wa Kimataifa wa Poland ambae ameidakia Arsenal mara 180, ameanzia Timu za Vijana za Timu hiyo mara baada ya kujiunga Mwaka 2006 akitokea Klabu ya Nchi kwao Legia Warsaw.
Licha ya kumtoa kwa Mkopo, Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, amedai Kipa huyo bado anaweza kuwa hazina kwao kwa vile atapata uzoefu zaidi huko Italy.
YOUNG KUTUA SPURS?
Winga wa Manchester United Ashley Young anavumishwa kutakiwa kwa udi na uvumba na Klabu ya London Tottenham Hotspur.
Ingawa habari hizi hazijathibitishwa, Spurs wamesemwa kuwa wanahitaji Winga ili kuziba pengo wanaloweza kuwa nalo ikiwa Mawinga wao kina Erik Lamela, Andros Townsend na Aaron Lennon, watahama kama pia inavyovumishwa.
Ripoti hizo zimedai Spurs inamwona Young, mwenye Miaka 30 na ambae amebakiza Mwaka mmoja tu kwenye Mkataba wake na Man United, kama mlengwa wao mkuu kutokana na Mchezaji huyo kukabiliwa na upinzani mkubwa kwenye nafasi yake huko Old Trafford.
Katika pozisheni ya Young huko Man United, Wachezaji wanaochipukia ambao wanamkosesha raha ni Mbrazil Andreas Pereira, Adnan Januzaj na Mchezaji mpya Memphis Depay huku pia upo uwezekano wa Muargentina Angel Di Maria kuleta upinzani ikiwa hatahamia PSG kama inavyosemwa.

Habari MotoMotoZ