WENGER ARUKA TETESI ZA KWENDA PSG, ADAI NI ‘HABARI FEKI!’

WENGER-HATIMAArsene Wenger amezikanusha habari kuwa amepewa Mkataba kujiunga na Mabingwa wa Nchini kwao France, Paris Saint-Germain.

Wenger, mwenye Miaka 67, anamaliza Mkataba wake na Arsenal mwishoni mwa Msimu huu lakini tayari Klabu hiyo ishamwekea Mezani Mkataba Mpya wa Miaka Miwili na yeye Juzi, mara baada ya kutandikwa 3-1 na West Bromwich Albion huko The Hawthorns, kutamka tayari ashaamua nini hatima yake na uamuzi huo utakuwa bayana hivi karibuni.

Kipigo hicho cha Arsenal ni chao cha 4 katika Mechi zao 5 za mwisho za EPL, Ligi Kuu England na kimewashusha hadi Nafasi ya 6.

Hali hiyo imewagawanya mno Mashabiki wa Arsenal na kumekuwa na Maandamano ya Makundi Mawili kati yao, moja likimpinga na jingine kumsapoti.

Hivi karibuni Wenger alikaririwa akisema kuwa ikiwa ataondoka Arsenal basi atatua Klabu nyingine kuendelea na kazi na PSG, Klabu ya Nchini kwao na Tajiri, inaonekana ni muafaka kwake hasa baada ya Meneja wao Msimu huu, Unai Emery, kuonekana kuyumba.

Lakini Wenger hii Leo amekanusha uvumi huo kwa kutamka: “Ni uvumi wa uongo, ni kile kinachoitwa ‘Habari Feki’! Naikanusha rasmi, si kweli!”

Mbali ya kuzorota hivi karibuni, na hasa kubamizwa Jumla ya Bao 10-2 na Bayern Munich katika Mechi 2 na kutupwa nje ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, Wachambuzi huko England wamesisitiza Wenger atasaini Mkataba mpya na kubaki Arsenal.

Pengine tamko la kubakia huko Emirates linasubiri nini kitajiri kwa matokeo ya Uwanjani ya Mwezi Aprili ambao wanauanza kwa mtanange mkali wa EPL hapo Aprili 2 wakiwa Nyumbani kuwavaa Man City ambao pia watapambana nao tena huko Wembley Stadium kwenye Nusu Fainali ya FA CUP hapo Aprili 23.

BORO YAMTIMUA KARANKA, SWAHIBA WA MOURINHO!

MOU-KARANKAAitor Karanka ametimuliwa Umeneja na Middlesbroughambayo ni maarufu kama Boro.

Karanka, Raia wa Spain mwenye Miaka 43, ameondolewa Asubuhi hii akiiacha Timu hiyo aliyodumu nayo kwa Miaka Mitatu na Nusu ikiwa Nafasi ya 19 kati ya Timu 20 za EPL, Ligi Kuu England.

Boro hawajashinda katika Mechi 10 za Ligi, mara ya mwisho ikiwa Desemba 17, huku wakifunga Bao 3 tu katika kipindi hicho.

Aliekuwa Msaidizi wa Meneja, Steve Agnew, ndie atakaimu nafasi ya Karanka.

Kutimuliwa kwa Karanka, ambae ni swahiba mkubwa wa Meneja wa Man United, Jose Mourinho, Timu ambayo Boro wataivaa katika Mechi ya Ligi inayofuata, kulitangazwa kwenye Tovuti ya Klabu hiyo Asubuhi hii.

Karanka na Mourinho walikuwa wote huko Real Madrid baada ya Mourinho kumteua kuwa Msaidizi wake Juni 2010.

Licha ya kusuasua, Karanka aliamini atarekebisha mambo kwenye Mechi zao 11 za Ligi walizobakisha na hasa alipata imani hiyo baada ya kucheza vizuri Mechi yao ya mwisho walipopigwa 2-0 na Man City kwenye Robo Fainali ya FA CUP Jumamosi iliyopita.

 

 

PEP GUARDIOLA: ‘BILA KOMBE MSIMU WA MANCHESTER CITY UMEFELI!’

PEP-TAJIPep Guardiola amekiri kuwa ikiwa kwenye Msimu wake huu wa kwanza na Manchester City utaisha bila kutwaa Kombe lolote basi utakuwa umefeli.

Akiwa na mafanikio makubwa kwenye Klabu za Barcelona na Bayern Munich, Guardiola alitegemewa kupata mafanikio makubwa alipotua City lakini matarajio ya kutwaa Ubingwa wa England yanafifia wakiwa nyuma ya Vinara wa Ligi Chelsea kwa Pointi 10 huku Mechi zimebaki 11.

Hata hivyo, Manchester City bado wamo kwenye FA Cup na UCl, UEFA CHAMPIONZ LIGI.

Guardiola ameeleza: “Kama sipati Kombe sitakuwa hapa muda mrefu! Bila Kombe hautakuwa Msimu mzuri! Nilijua hilo tangu Agosti. Kuwa Meneja kunategemea mafanikio!”

Guardiola ametoboa kuwa akiwa na Bayern hakutwaa UCL bali alitwaa Ligi mara 3 na hilo kuonekana ni maafa.

Ameeleza: “Nilitwaa Ubingwa wa Ligi mara 3 mfululizo, tulibeba Vikombe Viwili kati ya Vitatu na kufika Nusu Fainali na Fainali ya vingine na hayo kuonekana ni maafa!”

RIPOTI: ARSENAL YATENGA £60m KUMCHOTA MBADALA WA ALEXIS SANCHEZ!

ARSENAL-SANCHEZ-MKONOARSENAL wanatarajiwa kutoa Ofa ya Pauni Milioni 60 ili kumnunua Straika wa Lyon ya France Alexandre Lacazette baada ya kukata tamaa ya kuweza kumbakiza Alexis Sanchez kwa ajili ya Msimu ujao.
Mpaka sasa Fowadi wao kutoka Chile Sanchez bado hajakubali kusaini Mkataba mpya huku wa sasa ukiwa umebakiza Miezi 18 tu na Meneja wa Arsenal Arsene Wenger inadaiwa ashakata tamaa ya kuendelea kuwa nae.
Hilo limemfanya Wenger kutafuta mbadala wake na Lacazette yupo juu kabisa ya Listi ya walengwa wake.
Ripoti huko England na France zimedai Lyon itadai ilipwe si chini ya Pauni Milioni 50 na Dau halisi kufikia Pauni Milioni 60 ikutegemea vigezo zaidi vya mafanikio ya Mchezaji huyo.
Kabla Msimu huu wa sasa kuanza Arsenal walitoa Ofa ya Pauni Milioni 35 kumnunua Lacazette lakini ilikataliwa na Lyon na sasa Dau limepanda wakati pia Liverpool wakiripotiwa kumnyemelea.
Licha ya kuwafungia Lyon Bao 27 katika Mechi zao 31 Msimu huu Lyon wako tayari kumuuza Lacazette kwa Dau kubwa muafaka kwao.

CARRICK KUTUNUKIWA MECHI YA HESHIMA OLD TRAFFORD KWA UTUMISHI ULIOTUKUKA!

>WASHIRIKI VAN DER SAR, NEVILLE, RIO, SCHOLES, GIGGS DHIDI YA GERRARD, LAMPARD, OWEN!

MANUNITED-CARRICK-ABEBA-FACUPMichael Carrick ametunukiwa Mechi ya Heshima na Klabu yake Manchester United kwa Utumisha wake uliotukuka wa Miaka 11.

Kwa mujibu wa matakwa ya Carrick mwenyewe, ambae ndie Naibu Kepteni wa Man United, Fedha zote zitakazopatikana baada ya kutoa Matumizi zitagawiwa kwa Mifuko ya Hisani kama Msaada kupita Mfuko wake mwenyewe ulioanzishwa hivi karibuni uitwao Michael Carrick Foundation na kusajiliwa rasmi.

Miongoni mwa Sherehe za Siku hiyo Maalum, Jumapili Juni 4, ni Mechi kati ya Kombaini ya Manchester United ya Mwaka 2008 dhidi ya Timu ya Nyota wa Michael Carrick.

Kikosi cha Man United ambacho Wachezaje wake wamethibitisha kushiriki ni pamoja na Edwin van der Sar, Gary Neville, Rio Ferdinand, Paul Scholes na Ryan Giggs wakati Nyota wa Michael Carrick watakuwemo kina Steven Gerrard, Frank Lampard na Michael Owen huku wengi wengine wakiwa mbioni kuthibitisha.

MANUNITED-CARRICK-MAR2

Mwenyewe Michael Carrick ameeleza: “Kuichezea Klabu kubwa kabisa Duniani kwa Miaka 11 ni kitu ambacho nasikia fahari kubwa na ni heshima kubwa kutunukiwa hii Mechi ya Heshima. Gemu hii itakuwa spesho kwangu na Familia yangu na natumaini itakuwa Siku ya Kumbukumbu kubwa ya Sherehe kwa Washiriki wote.

Meneja wa Man United, Jose Mourinho, ameeleza: “Nimefurahi sana Michael amepewa Mechi hii. Michael ni Mtu wa ajabu, mwema na Profeshenali halisi. Analeta utulivu kwenye Kikosi chetu na kuwatuliza akili wenzake waweze kushambulia zaidi. Ni mwelewa mzuri wa Gemu na mfano bora mno kwa Wachezaji Vijana!”

Nae Ed Woodward, Makamu Mwenyekiti Mtendaji wa Manchester United, ameeleza: "Michael ni kielelezo halisi cha Mchezaji wa Manchester United. Anacheza kwa kipaji cha hali ya juu ambacho huonyesha hajitutumui. Ni Mchezaji Kitimu kwa Asilimia 100 na Wachezaji Chipukizi huegemea kwake.Tangu mwanzo alionyesha Ushujaa mkubwa kwa kuvaa Jezi yenye Namba ya Nguli Roy Keane na amejijenga zaidi!”