BAADA KUTISHIWA KUSHITAKIWA, LIVERPOOL YAJITOA KUMSAKA VAN DIJK!

SOUTHAMPTON-VANDIJKLiverpool wameomba radhi kwa Southampton kwa kutoelewana kokote kulikotokea wakati wao wakimsaka Beki Virgil van Dijk.

Juzi, Southampton waliwataka Wasimamiza wa EPL, LIGI KUU ENGLAND, kuichunguza Liverpool kwa kutaka kumrubuni Sentahafu wao, Virgil van Dijk, mwenye Miaka 25, kinyume cha taratibu.

Meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp, alimtaka Beki huyo wa Kimataifa wa Netherlands na Mchezaji huyo mwenyewe akadaiwa kusema anaitaka Liverpool badala ya Klabu kadhaa nyingine zilizoonyesha nia nae.

Hilo liliwafanya Southampton waamini Liverpool walienda moja kwa moja kwa Van Dijk badala ya kupitia rasmi Klabuni kwao na hivyo kuitaka EPL kuchunguza.

Jana Liverpool walitoa Taarifa rasmi ya kuomba radhi na pia kutamka sasa hawatashughulika tena kutaka kumnunua Van Dijk.

Mwaka Jana, Van Dijk alisaini Mkataba Mpya wa Miaka 6 na Southampton na Klabu hiyo ikaweka thamani yake ya kununuliwa kuwa Pauni Milioni 50 licha wao kumnunua kwa Pauni Milioni 13 kutoka kwa Celtic ya Scotland Mwaka 2015.

Habari MotoMotoZ