MCHEZAJI WA ZAMANI NEWCASTLE NA IVORY COAST, CHEICK TIOTE AFARIKI GHAFLA!

TIOTE-RIPKIUNGO wa zamani wa Klabu ya England Newcastle na Timu ya Taifa ya Ivory Coast Cheick Tiote amefariki Jana huko China akiwa Mazoezini na Klabu yake.
Habari za Kifo cha Tiote, Miaka 30, zimethibitishwa na Wakala wake Emanuele Palladino ambae Jana Jioni alitoa tamko rasmi kuwa Tiote alipoteza maisha akikimbizwa Hospitalini.
Palladino ameeleza: "Kwa huzuni kubwa nathibitisha kifo cha Mteja wangu alieanguka Mazoezini akiwa na Klabu yake Beijing Enterprises na kufariki akiwa njiani Hospitalini. Hatuwezi kusema zaidi wakati huu na tunaomba Familia yake isibuguziwe wakati huu mgumu. Tunaomba Sala zenu wote!"
Tiote alipata umaarufu mkubwa akiwa England alipoichezea Newcastle Gemu 156 katika Miaka 7 yake baada ya kuhamia hapo akitokea FC Twente ya Netherlands.
Aliihama Newcastle Februari 2017 kwenda China kujiunga na Beijing Enterprises.
Rambirambi za Kifo hiki zilimiminika kila sehemu na moja ni hii Posti ya Twitter kutoka kwa Mchezaji mwenzake, Demba Ba, waliekuwa nae Newcastle:

TIOTE-DEMBA-TWITTER

Habari MotoMotoZ