WEST HAM YAIKATIA RUFAA NYEKUNDU YA FEGHOULI, KOCHA WA BAYERN ATHIBITISHWA MENEJA MPYA SWANSEA!

SWANSEA-CLEMENTWest Ham imethibitisha kukataa Rufaa kupinga Kadi Nyekundu ya Mchezaji wao Sofiane Feghouli aliyopewa Jumatatu Usiku walipochapwa 2-0 na Manchester United na wakati huo huo Swansea City kuthibitisha uteuzi wa Paul Clement kama Meneja wao mpya.

RUFAA

West Ham imethibitisha kukataa Rufaa kupinga Kadi Nyekundu ya Mchezaji wao Sofiane Feghouli aliyopewa Jumatatu Usiku walipochapwa 2-0 na Manchester United.

Kiungo huyo kutoka Algeria alipewa Kadi Nyekundu na Refa Mike Dean kwa kumchezea Rafu mbaya Sentahafu Phil Jones katika Dakika ya 15.

Feghouli, mwenye Miaka 27, amekuwa Mchezaji wa 5 kuonyeshwa Kadi Nyekundu na Refa Mike Dean Msimu huu.

Ikiwa Kifungo cha Feghouli kitathibitishwa, Mchezaji huyo atazikosa Mechi 3 za Swansea dhidi ya Manchester City hapo Ijumaa ikiwa ni Mechi ya Raundi ya 3 ya FA CUP, na Mechi 2 za EPL, Ligi Kuu England, wakicheza na Crystal Palace na Middlesbrough.

PAUL CLEMENT MENEJA MPYA SWANSEA CITY.

Swansea wamemthibitisha Paul Clement kama Meneja wao mpya na amepewa Mkataba wa Miaka Miwili na Nusu.

Clement, mwenye Miaka 44 na Bosi wa zamani wa Derby County ambae yupo Bayern Munich kama Kocha Msaidizi, alikuwa mazungumzoni na Swansea kuwa Meneja wao wa 3 Msimu huu.

Clement anarithi nafasi ya Bob Bradley alietimuliwa mara baada ya Swansea kuchapwa 4-1 na West Ham Siku ya Boksing Dei baada kudumu kwa Siku 85 tu.

Clement amewahi kufanya kazi kama Msaidizi wa Carlo Ancelotti huko

Chelsea, Paris St Germain, Real Madrid na sasa Bayern Munich.

Lakini kazi pekee aliyofanya kama Meneja, huko Derby County, ilitibuka Miezi 8 tu tangu ateuliwe alipotimuliwa Februari 2016 bila kutegemewa kwani aliiweka Derby Nafasi ya 5 baada kuongoza Ligi ya Daraja la Championship Miezi Miwili nyuma.