MOURINHO: HATUPATI MATOKEO TUNAYOSTAHILI! TUNAPATA SARE, TUKISTAHILI USHINDI, WAPINZANI WANAFURAHIA!

MANUNITED-MOU-PLAYERS-TRAININGJose Mourinho amesikitishwa na Timu yake kutopata ushindi Jana walipoongoza 1-0 huko Goodison Park katika Mechi ya EPL, Ligi Kuu England, na Everton kusawazisha kwa Penati ya Dakika ya 88.

Sare hiyo ni ya 6 kwa Man United tangu mwanzoni mwa Oktoba.

Akiongea na Wanahabari mara baada ya Mechi hiyo ya Jana, Mourinho alieleza: “Hatupati matokeo tunayostahili. Tunapata Sare tukistahili ushindi!”

“Wapinzani wanaondoka Uwanjani wakifurahia Sare, sisi tunaondoka Uwanjani tukihisi tulistahili zaidi!”

Vile vile, Meneja huyo wa Man United aliwaponda Wanahabari kwa jinsi wanavyoielezea Timu yake.

Amenena: “Timu zangu zikicheza Soka la kuridhisha na kutwaa Mataji mnadai si sawa. Sasa Timu yangu inacheza Soka safi sana, wakati hiki ni kipindi cha mpito hapa Man United kwa Miaka Miwili au Mitatu iliyopita, sasa mnadai kinachotakiwa ni ushindi tu!”

Aliongeza: “Kwa wakati huu zipo Timu zinazojihami na Wachezaji 11 na kubutua Mipira mbele katika Kaunta Ataki na kushinda…mnadai ni safi! Amuane!”

Alipoulizwa maoni yake kuhusu Matukio mawili ya Mechi hiyo na Everton na la kwanza likiwa ni lile la Beki wake Marcos Rojo kuruka kwa Miguu Miwili kumkabili Romelu Lukaku na kupewa Kadi ya Njano badala Nyekundu, Mourinho, ambae ametoka tu kwenye Kifungo cha Mechi Moja, alijibu hakuona tukio hilo.

Alipoulizwa kuhusu Penati ya Everton iliyozaa Bao la kusawazisha, ambayo baadhi ya Wachambuzi huko England walidai ulikuwa ni uamuzi mbovu, Mourinho alijibu: “Sina mawazo yeyote. Sina la kusema!”

Mechi inayofuata ya Man United ni Alhamisi ya Kundi A la UEFA EUROPA LIGI Ugenini huko Ukraine dhidi ya Zorya Lugansk ambayo ni ya mwisho kwa Kundi hilo na ambayo wanahitaji Pointi 1 tu kutinga Raundi ya Mtoano ya Timu 32.

Kisha Jumapili wako kwao Old Trafford kucheza na Tottenham Hotspur.

EPL, LIGI KUU ENGLAND

Ratiba:

**Saa za Bongo

Jumatatu Desemba 5

2300 Middlesbrough v Hull City   

Jumamosi Desemba 10

1530 Watford v Everton    

1800 Arsenal v Stoke City           

1800 Burnley v Bournemouth      

1800 Hull City v Crystal Palace    

1800 Swansea City v Sunderland 

2030 Leicester City v Manchester City             

Jumapili Desemba 11

1500 Chelsea v West Bromwich Albion  

1715 Manchester United v Tottenham Hotspur           

1715 Southampton v Middlesbrough               

1930 Liverpool v West Ham United                 

Jumanne Desemba 13

2245 Bournemouth v Leicester City       

2245 Everton v Arsenal     

Jumatano Desemba 14

2245 Middlesbrough v Liverpool  

2245 Sunderland v Chelsea         

2240 West Ham United v Burnley

2300 Crystal Palace v Manchester United

2300 Manchester City v Watford            

2300 Stoke City v Southampton            

2300 Tottenham Hotspur v Hull City               

2300 West Bromwich Albion v Swansea City              

Jumamosi Desemba 17

1530 Crystal Palace v Chelsea               

1800 Middlesbrough v Swansea City     

1800 Stoke City v Leicester City  

1800 Sunderland v Watford                  

1800 West Ham United v Hull City          

2030 West Bromwich Albion v Manchester United      

Jumapili Desemba 18

1630 Bournemouth v Southampton       

1900 Manchester City v Arsenal   

1900 Tottenham Hotspur v Burnley                 

Jumatatu Desemba 19

2300 Everton v Liverpool