LIGI KUU ENGLAND: STOKE WASHINDA UGENINI!

 >MECHI NYINGINE LEO NI EMIRATES ARSENAL-BOURNEMOUTH, OLD TRAFFORD NI MAN UNITED-WEST HAM!

EPL - LIGI KUU ENGLAND

Ratiba/Matokeo:

Jumapili Novemba 27

Watford 0 Stoke City 1                  

1715 Arsenal v Bournemouth         

1930 Manchester United v West Ham United         

1930 Southampton v Everton

+++++++++++++++++++++++++++++

WATFORD-STOKESTOKE CITY wamepanda hadi Nafasi ya 10 kwenye EPL, Ligi Kuu England, baada ya kushinda 1-0 huko Ugenini Vicarage Road Stadium walipowafunga Wenyeji wao Watford ambao wako Nafasi ya 8.

Bao la ushindi la Stoke lilitokana kwa Kona iliyopigwa Dakika ya 29 na XherdanEPL-NOV27B Shaqiri ilipounganishwa kwa Kichwa na Charlie Adam na Mpira kupiga Posti na kisha kumgonga Kipa Heurelho Gomes na kutinga wavuni kuwapa Stoke City Bao.

Watford walimaliza Mechi hii wakiwa Mtu 10 baada ya Mchezaji wao Britos kumwangusha Shaqiri na kulambwa Kadi ya Njano ya Pili na hivyo kupewa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 90.

Baadae Leo zipo Mechi 3 nyingine za EPL lakini macho ni huko Emirates Arsenal wakicheza na Bournemouth na huko Old Trafford wakati Man United wakikipiga na West Ham United.

VIKOSI:

Watford: Gomes; Kaboul, Prödl, Britos; Janmaat, Capoue, Behrami, Holebas; Amrabat, Deeney, Pereyra.

Akiba: Pantilimon, Kabasele, Mariappa, Zuniga, Guedioura, Ighalo, Okaka.

Stoke City: Grant; Johnson, Martins-Indi, Muniesa, Pieters; Imbula, Adam, Walters; Shaqiri, Diouf, Arnautovic.

Akiba: Given, Bony, Crouch, Bojan, Ramadan, Ngoy, Verlinden.

REFA: Robert Madley

Ratiba:

**Saa za Bongo

Jumamosi Desemba 3

1530 Manchester City v Chelsea      

1800 Crystal Palace v Southampton          

1800 Stoke City v Burnley              

1800 Sunderland v Leicester City              

1800 Tottenham Hotspur v Swansea City             

1800 West Bromwich Albion v Watford                

2030 West Ham United v Arsenal              

Jumapili Desemba 4

1630 Bournemouth v Liverpool                

1900 Everton v Manchester United            

Jumatatu Desemba 5

2300 Middlesbrough v Hull City