LIGI KUU ENGLAND: LIVERPOOL YASHINDA YAITOA CITY KILELENI!

>>BAADAE LEO CHELSEA KUIKWANYUA LIVERPOOL KILELENI WAKIIFUNGA SPURS?

EPL - LIGI KUU ENGLAND

Ratiba/Matokeo:

**Saa za Bongo

Jumamosi Novemba 26

Burnley 1 Manchester City 2           

Hull City 1 West Bromwich Albion 1           

Leicester City 2 Middlesbrough 2               

Liverpool 2 Sunderland 0               

Swansea City 5 Crystal Palace 4                

2030 Chelsea v Tottenham Hotspur 

+++++++++++++++++++++++++++++

LIVER-MILNERBAO za Divock Origin a Penati ya James Milner zimewaweka Liverpool kileleni mwa EPL, Ligi Kuu England, walipoifunga Sunderland 2-0 huko Anfield.

Kwenye Mechi hiyo Liverpool walipata pigo kwa nyota wao mkubwa wa sasa Philippe Coutinho kuumia Enka kabla ya Haftaimu na sasa anahofiwa kuwa nje kwa muda.

Lakini Origi, alieingizwa kumbadili Coutinho, ndio alianza kuitoboa Sunderland kwenye Dakika ya 75 na Penati ya Dakika za Majeruhi kuipa Liverpool ushindi ambao umewaweka kileleni mwa EPL wakifungana kwa Pointi na Man City ambao mapema hii Leo, Man City iliifunga Burnley 2-1 na kukaa kileleni mwa EPL kwa muda.

Mechi ya mwisho hii Leo ni huko Stamford ikiwa ni Dabi ya Jiji la London wakati Wenyeji Chelsea watacheza na EPL-NOV26BTottenham Hotspur na ushindi kwao utawarejesha tena kileleni mwa EPL wakizipiku Liverpool na City.

VIKOSI:

Liverpool:Karius, Clyne, Matip, Lovren, Milner, Wijnaldum, Henderson, Can, Mane, Firmino, Coutinho

Akiba: Klavan, Moreno, Lucas, Mignolet, Origi, Oviemuno Ejaria, Woodburn.
Sunderland:Pickford, Jones, Kone, O’Shea, Van Aanholt, Pienaar, Denayer, Ndong, Watmore, Anichebe, Defoe

Akiba: Mannone, Larsson, Khazri, Manquillo, Love, Januzaj, Gooch.
REFA:Anthony Taylor

Ratiba:

**Saa za Bongo

Jumapili Novemba 27

1500 Watford v Stoke City             

1715 Arsenal v Bournemouth         

1930 Manchester United v West Ham United         

1930 Southampton v Everton         

Jumamosi Desemba 3

1530 Manchester City v Chelsea      

1800 Crystal Palace v Southampton          

1800 Stoke City v Burnley              

1800 Sunderland v Leicester City              

1800 Tottenham Hotspur v Swansea City             

1800 West Bromwich Albion v Watford                

2030 West Ham United v Arsenal              

Jumapili Desemba 4

1630 Bournemouth v Liverpool                

1900 Everton v Manchester United            

Jumatatu Desemba 5

2300 Middlesbrough v Hull City