CAF YAANIKA 5 WAGOMBEA TUZO MCHEZAJI BORA AFRIKA 2016!

CAF-BESTCAF, Shirikisho la Soka Afrika, Leo limetangaza Majina ya Wachezaji Watano ambao watagombea Tuzo ya Mchezaji Bora Afrika kwa Mwaka 2016.

Mbali ya hao, pia Majina Matano ya Wagombea Wachezao Soka lao ndani ya Bara la Afrika pia yametajwa kwa wanaowania Tuzo ya Mchezaji Bora Afrika kwa Mwaka 2016 kwa Daraja hilo.

Wagombea hawa wameamuliwa kutokana na Kura za Wajumbe wa Kamati za CAF za Wanahabari na ile ya Ufundi na Maendeleo pamoja na Nusu ya Jopo la Watu 20 la Magwiji wa Soka.

LISTI ZA WAGOMBEA:

WAGOMBEA – Mchezaji Bora Afrika 2016:

1. Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon & Borrusia Dortmund)

2. Riyad Mahrez (Algeria & Leicester City)

3. Sadio Mane (Senegal & Liverpool)

4. Mohamed Salah (Egypt & Roma)

5. Islam Slimani (Algeria & Leicester City)

WAGOMBEA – Wachezao Soka ndani ya Bara la Afrika:

1. Khama Billiat (Mamelodi Sundowns & Zimbabwe)

2. Keegan Dolly (Mamelodi Sundowns & South Africa)

3. Rainford Kalaba (TP Mazembe & Zambia)

4. Hlompho Kekana (Mamelodi Sundowns & South Africa)

5. Denis Onyango (Mamelodi Sundowns & Uganda)

Ili kupata Washindi wa Tuzo hizi mbili, Kura zitapigwa na Makocha Wakuu au Wakurugenzi wa Ufundi wa Nchi 54 Wanachama wa CAF pamoja na Nchi Wanachama Washiriki za Visiwa vya Reunion na Zanzibar pamoja na ile Nusu nyingine ya Jopo la Watu 20 la Magwiji wa Soka.

Hafla ya kukabidhi Tuzo hizo iitwayo The 2016 Glo-CAF Awards Gala ambayo inadhaminiwa na Kampuni kubwa ya Mawasiliano, Globacom, itafanyika Alhamisi Januari 5, 2017 huko Abuja, Nigeria.

Habari MotoMotoZ