DERBY DELLA MADONNINA: AC MILAN, INTER MILAN SARE!

Derby Della MadonninaWABABE wa Uwanja wa San Siro huko Jijini Milan Nchini Italy, AC Milan na Inter Milan Jana walitoka Sare 2-2 katika Mechi ya Serie A inayobatizwa Jina la ‘Derby Della Madonnina’.

Bao 2 za Fernández Saez zilielekea kuwapa ushindi AC Milan lakini Ivan Perisic alisawazisha katika Dakika za Majeruhi na kuwapa Inter Sare ya 2-2 katika Mechi yao kwanza chini ya Meneja Stefano Pioli.

Matoke ohayo bado yamewaacha Mabingwa Juventus kuwa kilelewni wakiwa na Pointi 33 kwa Mechi 13 wakifuata AS Roma na AC Milan waliofungana kwa Pointi 26 kila mmoja huko nao pia wamecheza Mechi 13 kila mmoja.

++++++++++++++++++++

MAGOLI:

AC Milan 2

Fernández Saez (42' & 58')

Inter Milan 2

Candreva (53')

Perisic (92')

++++++++++++++++++++

Inter Milan, ambao pia wamecheza Mechi 13, wapo Nafasi ya 9 wakiwa na Pointi 18.

VIKOSI:

AC Milan: Donnarumma; Abate, Paletta, Gomez, De Sciglio; Kucka, Locatelli, Bonaventura; Suso, Bacca, Niang

Akiba: Gabriel, Plizzari, Antonelli, Ely, Zapata, Mati Fernandez, Honda, Pasalic, Poli, Sosa, Lapadula, Luiz Adriano

Inter Milan: Handanovic; D’Ambrosio, Miranda, Medel, Ansaldi; Brozovic, Kondogbia, Joao Mario; Candreva, Icardi, Perisic

Akiba: Carrizo, Berni, Ranocchia, Santon, Murillo, Nagatomo, Melo, Banega, Gnoukouri, Jovetic, Biabiany, Eder, Gabriel Barbosa

Habari MotoMotoZ