JURGEN KLOPP AMTETEA ROONEY: ‘MALEJENDARI WALIGIDA KAMA MASHETANI, KUCHOMA KAMA WEHU!’

>>WENGER NAE ATETEA: ‘SOTE TUSHAPITIA UJANA, HATUKUWA MALAIKA!’

ROONEY-KEPTENI-ENGLANDMENEJA wa Liverpool Jurgen Klopp anaamini chochote alichofanya Kepteni wa England Wayne Rooney kwenye Usiku ambao Wachezaji wa Timu ya Taifa walipewa Ofu hakikuwa kitu kibaya.

Klopp pia amedai Malejendari wote wa Soka ‘walikunywa kama Mashetani na kuvuta kama Wehu!’.

Kauli ya Klopp inafuatia zogo lililoikumba England baada ya Picha za Rooney kuzagaa Magazetini na Mitandaoni akinaswa akiwa ‘chakari’ ingawa Meneja wa England Gareth Southgate alithibitisha Siku hiyo Wachezaji wote walipewa Ofu baada ya kuichapa Scotland 3-0 kwenye Mechi ya kusaka Tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia.

Picha hizo za Rooney zilipigwa akiwa kwenye Hoteli waliyofikia Wachezaji wa Timu ya Taifa ya England baada kuombwa na Mashabiki waliokuwa kwenye Harusi kupiga nao Picha.

Tayari Rooney ameshaomba radhi kwa tukio hilo.

Lakini Jurgen Klopp anaamini inabidi Watu waweke sawa tukio lote.

Akiongea na Wanahabari kuelekea Gemu ya Timu yake Liverpool ambayo Jumamosi ipo Ugenini huko Southampton, Klopp alieleza: “Nawaonea imani Wachezaji. Najua sisi tupo kwenye neema, tunzavuna hela nyingi na kufanya kazi tunayoipenda lakini mwishoe inaweza kushangaza ikijulikana pia sisi ni Binadamu!”

Amefafanua: “Mara nyingine tunaalikwa kwenye Harusi, Bethdei na lolote na tunaweza kujichunga na kusema hatunywi au hatuvuti. Lakini Watu wote tuliowapenda, Malejendari wote tuliowapenda na kuwahusudu ‘walikunywa kama Mashetani na kuvuta kama Wehu’ na kubaki Wachezaji wazuri tu!”

Klopp amesema: “Sijui Wayne alikuwa wapi lakini hili si jambo kubwa! Baada ya Wiki 2 au 3 kila Mtu atasahau hili sasa ya nini kulikuza?”

Nae Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema Wachezaji wa sasa wanajitunza vyema.

Wenger amesema: “Sote tumewahi kuwa Vijana, na sote hatukuwa Malaika tukiwa na Miaka 20, 21 na kwa ujumla ni sehemu ya Ujana kufanya makossa. Baada ya hapo Wachezaji wakubwa hujitathmini na kujikosoa.”