HENRIKH MKHITARYAN HAJAKATA TAMAA NDOTO YAKE NA MANCHESTER UNITED!

MANUNITED-MKHITARYANHenrikh Mkhitaryan ameapa kupigania nafasi ndani ya Manchester United huku akisisitiza hakuna kitakachomsimamisha kutimiza ndoto yake na Timu hiyo.

Wadau wengi walitegemea makubwa kutoka kwa Mkhitaryan, mwenye Miaka 27, tangu ahamie Man United kutoka Borussia Dortmund mwanzoni mwa Msimu kwa Dau la Pauni Milioni 26.3.EPL-NOV18

Lakini Staa huyo kutoka Armenia amekuwa hana Namba kabisa Kikosini mwa Man United na amecheza Mechi 1 tu katika Siku 54 wakati Man United inafungwa 2-1 na Fenerbahce huko Uturuki Alhamisi iliyopita katika Mechi ya Kundi A la UEFA EUROPA LIGI.

Baada ya kipigo hicho, Meneja wa Man United Jose Mourinho aliwapandishia Wachezaji wake na Mkhitaryan kuambiwa anahitaji kufanya juhudi zaidi.

Licha ya kuhuzunishwa na kutopata namba, lakini Mkhitaryan hajakata tamaa na ameapa: “Ni kweli sichezi sana lakini sitakata tamaa. Nimetoka mbali mno kuja kucheza Manchester United na hakuna kitakachonizuia kutimiza ndoto yangu. Sitarudi nyuma, nitapata nguvu ya kutimiza lengo lango!”

Hivi sasa Man United ipo ‘mapumzikoni’ kupisha Mechi za Kimataifa na itarudi dimbani Novemba 19 kucheza Mechi ya EPL, Ligi Kuu England, Uwanjani Old Trafford na Arsenal.

EPL - LIGI KUU ENGLAND

Ratiba:

**Saa za Bongo

Jumamosi Novemba 19

1530 Manchester United v Arsenal FC

1800 Everton FC v Swansea City

Southampton FC v Liverpool

Sunderland v Hull City

Watford v Leicester City

Crystal Palace FC v Manchester City

Stoke City FC v Bournemouth FC

2030 Tottenham Hotspur v West Ham United

Jumapili Novemba 20

1900 Middlesbrough v Chelsea FC

Jumatatu Novemba 21

2300 West Bromwich Albion FC v Burnley FC