KLABU AFRIKA: DROO ZA MAKUNDI CAF CHAMPIONZ LIGI, KOMBE LA SHIRIKISHO ZAFANYIKA!

CAF-DROODROO za kupanga Makundi ya Mashindano makubwa kwa Klabu za Afrika zimefanyika hii Leo na Mabingwa Watetezi wa CAF CHAMPIONZ LIGI, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, kupewa Kundi C ambalo ni tata.

Pamoja nao ni Timu mpya kwenye hatua hii ya Mashindano hayo, Saint George ya Ethiopia, Esperance ya Tunisia na AS Vita Club ya Congo DR, wote hao wakiwa ni Mabingwa wa zamani wa Mashindano haya.

Vigogo wakubwa wa Sudan, Al Hilal na Al Merreikh, wote wapo Kundi A pamoja na Etoile du Sahel ya Tunisia na Klabu ya Mozambique Ferroviario Beira.

DROO KAMILI:

CAF CHAMPIONZ LIGI

KUNDI A

Etoile du Sahel (Tunisia)   

Al Hilal (Sudan)      

Al Merreikh (Sudan)

Ferroviario Beira (Mozambique)

KUNDI B

Zamalek (Egypt)

USM Alger (Algeria)

Al Ahly Tripoli (Libya),

CAPS United (Zimbabwe)

KUNDI C

Mamelodi Sundowns (South Africa, Mabingwa Watetezi)

Esperance (Tunisia)

AS Vita Club (DR Congo)

Saint George (Ethiopia)

KUNDI D

Al Ahly (Egypt)

Wydad Casablanca (Morocco)

Coton Sport (Cameroon)

Zanaco (Zambia)

**Mechi za Kwanza za Makundi zitachezwa Mei 12-14

CAF KOMBE LA SHIRIKISHO

KUNDI A

-KCC [Uganda]

-FUS de Rabat [Morocco]

-Rivers United [Nigeria]

-Clube Africain [Tunisia]

KUNDI B

-Platinum Stars [South Africa]

-CS Sfaxien [Tunisia]

-Mbabane Swallows [Swaziland]

-MC Alger [Algeria]

KUNDI C

-Zesco United [Zambia]

-Al Hilal [Sudan]

-Libolo [Angola]

-Smouha [Egypt]

KUNDI D

-SuperSport [South Africa]

-TP Mazembe [congo DR]

-Horoya AC [Guinea]

-Centre de Formation de Mounana [Gabon]

**Mechi za Kwanza za Makundi zitaanza Wikiendi ya Mei 13 na 14

 

 

TOKA TFF: KAMATI YA KATIBA, SHERIA NA HADHI ZA WACHEZAJI KUKAA JUMANNE - KUPITIA POINTI ZA 'CHEE' ZA SIMBA?

>CAF YAPTISHA VIWANJA VYA UHURU, CCM KIRUMBA KUTUMIKA KIMATAIFA

PRESS RELEASE NO. 287                  APRILI 15, 2017

KAMATI YA KATIBA, SHERIA NA HADHI ZA WACHEZAJI KUKAA JUMANNE

TFF-TOKA-SITKamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), inatarajiwa kukutana Jumanne Aprili 18, 2017 kwa lengo la kupitia uamuzi uliofanywa na Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji Ligi Tanzania maarufu kwa jina la Kamati ya Saa 72.

Kwa mujibu wa Katiba ya TFF, Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF, ina mamlaka ya kutafsiri sheria na kanuni za mpira wa miguu nchini kama ilivyoainishwa kwenye katiba na sehemu ya utangulizi ya kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Kamati hiyo inakutana kutokana na ombi la timu ya Kagera Sugar ambayo imeomba kupitiwa upya uamuzi uliofanywa na Kamati ya Saa 72 ambayo kwa mujibu wa kanuni, ilitoa matokeo mapya ya mchezo kati ya timu hiyo na Simba uliofanyika Aprili 2, mwaka huu huko Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.

Katika mchezo huo, Kagera Sugar ilishinda mabao 2-1, lakini Simba ilikata rufaa ikidai kuwa Kagera Sugar ilivunja kanuni ya 37 (4) ya Ligi Kuu ya Vodacom kwa kumchezesha mchezaji Fakhi Mohammed ambaye alidaiwa na Simba kuwa alikuwa na kadi tatu za njano katika mechi tofauti za Liku Kuu ya Vodacom. Hivyo, ikaadhibiwa kwa mujibu wa kanuni ya 37 (37) ambayo ilitoa pointi tatu na magoli matatu kwa Simba.

CAF YAPTISHA VIWANJA VYA UHURU, CCM KIRUMBA KUTUMIKA KIMATAIFA

Shirikisho la Mpira wa barani Afrika (CAF), limevipitisha Viwanja vya Uhuru, Dar es Salaam na CCM Kirumba, jijini Mwanza kwa ajili ya michuano mbalimbali ya kimataifa ngazi ya klabu na timu za taifa.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linachukua nafasi hii kuwapongeza wamiliki viwanja hivyo kwa namna walivyoweza kutunza hadi kukidhi matakwa ya CAF.

Pongezi zinakwenda kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ndio wamiliki wa Uwanja wa Uhuru na Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mwanza ambao ndio wamiliki wa Uwanja wa CCM Kirumba.

Viwanja hivyo vilikaguliwa hivi karibuni kwa nyakati tofauti na Mkaguzi wa CAF na FIFA, Maxwell Mtouga kwa kukagua vema na kutoa taarifa ambayo imefanya taasisi za CAF na FIFA - zinazoongoza mpira wa miguu, kupitisha viwanja hivyo kwa ajili ya kutumika kwa ajili ya mechi za kimataifa.

…………………………………………………………………………………………

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA

POGBA: ‘MSINIHUKUMU KWA ADA YA UHAMISHO AU MAGOLI!’

MANUNITED-POGBA-WAYAPaul Pogba amesema asihukumiwe kwa Kiwango cha Ada yake ya Uhamisho au Magoli anayofunga kwani yupo wakati murua Klabuni Manchester United.

Pogba, ambae alivunja Rekodi ya Ada ya Uhamisho Duniani alipohama kutoka Juventus mwanzoni mwa Msimu huu, amesema anaamini anaandamwa pasipo na haki licha ya kuisaidia Man United kubeba EFL CUP pamoja na Ngao ya Jamii na bado wapo mawindoni kutwaa UEFA EUROPA LIGI.

Akiongea na Wanahabari kuelekea Mechi yao ya Robo Fainali ya huko Brussells, Belgium dhidi ya RSC Anderlecht ikiwa ni Mechi ya Kwanza ya Robo Fainali ya UEFA EUROPA LIGI, Pogba amejieleza vizuri tu.

Amesema: “Najisikia safi, kwa kweli. Tumetwaa Vikombe Viwili, lakini ni wazi nataka kufanya vyema zaidi. Nafanya vizuri, Timu ipo vizuri na tunatilia mkazo kubeba EUROPA LIGI na kupigania 4 Bora kwenye Ligi. Mie nimesahau Ada ya Uhamisho, hiyo imepita, naangalia Uwanjani na kufanya vyema kwa Timu yangu.”

Ameongeza: “Watu wanataka nifunge Magoli na wananihukumu kwa kutofunga Magoli, lakini hiyo ndio Soka. Wanataka nifunge kwa sababu ya Ada ya Uhamisho. Kazi yangu ni Kiungo, kutengeneza Mabao. Kama ningefunga yale Magoli yote yaliyopiga Posti [Mashuti 9], Watu wangekuwa kimya!”

Alipoulizwa tofauti ya Soka la Italy na England na hasa hii mara ya pili kucheza England, Pogba alijibu: “Huko Italy ni mbinu, Magoli machache. Lakini hapa England, ni kushambulia na ni ngumu. Timu 5 za juu na zile 2 za juu zinakaribiana mno. Hujui nini litatokea…tizama Arsenal kapigwa 3-0 na Crystal Palace!”

EPL, LIGI KUU ENGLAND

Ratiba:

Jumamosi Aprili 15

1430 Tottenham Hotspur v Bournemouth                  

1700 Crystal Palace v Leicester City                

1700 Everton v Burnley     

1700 Stoke City v Hull City

1700 Sunderland v West Ham United              

1700 Watford v Swansea City               

1930 Southampton v Manchester City             

Jumapili Aprili 16

1530 West Bromwich Albion v Liverpool 

1800 Manchester United v Chelsea        

Jumatatu

2200 Middlesbrough v Arsenal              

WENGER YUPO TU ARSENAL, AASHIRIA KUBAKI!

WENGER-YUPOMENEJA wa Arsenal Arsene Wenger Leo ametoa ishara ya kubakia kwake Klabuni hapo baada kuzungumzia mipango yao ya kabla Msimu Mpya wa 2017/18 kuanza.

Wenger, ambae Mkataba wake na Arsenal unamalizika mwishoni mwa msimu huu na tayari upo Mezani Mkataba Mpya wa Miaka Miwili, amekataa kutoboa kama ataendelea na Arsenal au atang’oka huku kukiwa na presha kutoka Kundi la Mashabiki wakitaka aondoke.

Mkataba wa Wenger, mwenye Miaka 67 na ambaye yuko Arsenal kwa Miaka 20, unaisha Juni lakini ametoa fununu za mipango yake kwa ajili ya Msimu Mpya unaoanza Agosti.

Wenger ameeleza: “Ninayo Mipango. Hiyo ndio kazi yangu kupanga.”

Alipobanwa nani atatangaza kama atabaki Arsenal, Wenger alijibu: “Klabu. Sina la kuongeza hapo. Siwezi kusema zaidi na nlichosema awali!”

Hivi karibuni Wenger alitamka kuwa ashaamua kuhusu kubaki au kuondoka Arsenal na Watu wasubiri tamko tu.

Hivi sasa Arsenal wapo Nafasi ya 5 kwenye EPL, Ligi Kuu England, na pia Nusu Fainali ya FA CUP ambako watacheza na Man City kwenye Nusu Fainali.

EPL – Ligi Kuu England

Ratiba:

Jumamosi Aprili 8

1430 Tottenham Hotspur v Watford                

1700 Manchester City v Hull City          

1700 Middlesbrough v Burnley              

1700 Stoke City v Liverpool                  

1700 West Bromwich Albion v Southampton              

1700 West Ham United v Swansea City           

1930 Bournemouth v Chelsea               

Jumapili Aprili 9

1530 Sunderland v Manchester United            

1800 Everton v Leicester City               

Jumatatu Aprili 10

2200 Crystal Palace v Arsenal     

LIVERPOOL YAFUNGIWA KUSAINI CHIPUKIZI, FAINI £100,000!

LIVER-U-WILL-NEVER-WALK-ALONELiverpool imepigwa Faini Pauni Laki 1 na kufungiwa kusaini Chipukizi baada ya kukiri kuvunja Sheria za Ligi Kuu England, EPL, zinazolinda na kudhibiti Usajili wa Makinda hao.

Liverpool wamepatikana na Hatia ya kumrubuni Chipukizi aliekuwa Klabuni Stoke City na sasa hawaruhusiwi kusaini Chipukizi yeyote kwa Mwaka Mmoja na Kifungo cha Mwaka Mmoja unaofuata kusimamishwa na kuwepo kwenye Angalizo kwa Miaka Mitatu ili kosa hilo lisirudiwe.

Wasimamizi wa EPL wameridhika kuwa Liverpool ilijaribu kumrubuni Kijana wa Miaka 12 aliyesajiliwa na Stoke City kwa kutoa Ofa ya kumlipia Ada za Shule na kuwalipa Wazazi wake ili aihame kwao bila maridhiano kwa Klabu hizo mbili kitu ambacho kilikuwa kinyume cha taratibu.

EPL imesema Liverpool wamekiri Kosa lao na wamekubali Adhabu zao.

EPL – Ligi Kuu England

Ratiba:

Jumatano Aprili 5

2145 Arsenal v West Ham United          

2145 Hull City v Middlesbrough             

2145 Southampton v Crystal Palace                 

2145 Swansea City v Tottenham Hotspur                  

2200 Chelsea v Manchester City           

2200 Liverpool v Bournemouth

Jumamosi Aprili 8

1430 Tottenham Hotspur v Watford                

1700 Manchester City v Hull City          

1700 Middlesbrough v Burnley              

1700 Stoke City v Liverpool                  

1700 West Bromwich Albion v Southampton              

1700 West Ham United v Swansea City           

1930 Bournemouth v Chelsea               

Jumapili Aprili 9

1530 Sunderland v Manchester United            

1800 Everton v Leicester City               

Jumatatu Aprili 10

2200 Crystal Palace v Arsenal