IBRAHIMOVIC NA MINGS KUSULUBIWA NA PILATO WA FA, KUFUNGIWA?

MINGS-IBRALEO REFA Kevin Friend ataonyesha kama ni rafiki au la wakati akiwasilisha Ripoti yake ya Mechi aliyochezesha Jumamosi kati ya Manchester United na Bournemouth huko Old Trafford na kuishia kwa Sare ya 1-1.

Mbali ya Zlatan Ibrahimovic kukosa Penati katika Mechi hiyo iliyojaa matukio mengi ikiwemo la Refa huyo kutoa Kadi ya Njano kwa Mchezaji wa Bournemouth Andrew Surman na ‘kusahau’ kuwa hiyo ni Kadi ya Njano ya Pili na kupita Dakika kadhaa ndipo ‘alipokumbuka’ na hivyo kumuwasha Kadi Nyekundu, tukio kubwa ni ‘vita’ kati ya Sentahafu wa Bournemouth Tyrone Mings na Straika wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic.

Vita hiyo ilifikia wakati Refa Kevin Friend kuwaonya wote Wawili lakini ikafikia kilele pale Mings alipomtimba Kichwani Ibrahimovic aliekuwa ameanguka katika Dakika ya 44 na Dakika 2 baadae Ibrahimovic alionekana ‘kumpiga kiwiko’ Mings wakati akipiga Kichwa Mpira wa Kona.

Wachezaji wote hao Wawili wamejitetea kuwa matukio hayo si ya kusudi.

Lakini kinachofuatia ni nini kimeandikwa kwenye Ripoti ya Refa Friend ambayo Leo itatua Mezani kwa FA, Chama cha Soka England.

Ikiwa Refa huyo atakiri kuwa aliyaona Matukio hayo Mawili basi stori inakwisha hapohapo kwani FA hawawezi tena kuchukua hatua zaidi.

Lakini ikiwa Refa Friend atakuwa si rafiki tena akidai hakuyaona au kutotaja chochote kwenye Ripoti yake basi FA, kwa mujibu wa Kanuni, wanaweza kuamua kupeleka Matukio hayo Mawili kwa Jopo Huru la Marefa wa Zamani Watatu ambao watayapitia na kuamua kama yalistahili Kadi Nyekundu au la.

Wakiamua ni Kadi Nyekundu basi FA itatoa Kifungo cha Mechi 3 au zaidi ikitegemea uzito wa kila Kosa.

Ikiwa atafungiwa basi Ibrahimovic atazikosa Mechi ya Robo Fainali ya FA CUP dhidi ya Chelsea na Mechi za Ligi dhidi ya Middlesbrough na West Bromwich Albion.

LIGI KUU CHINA YAVUNJA REKODI DUNIANI KUTUMIA FEDHA NYINGI UHAMISHO WACHEZAJI!

IMG-20170301-WA0000KLABU za CSL, Ligi Kuu China, ndio watumiaji wakubwa wa Fedha Duniani kwa Mwaka 2017 kwa kutumia Pauni Milioni 333.54 kwenye Dirisha la Uhamisho ambalo kwao lilifungwa Jana Februari 28.
Hadi kufikia Januari 31wakati Dirisha la Uhamisho lao likifungwa, EPL, Ligi Kuu England, ndio ilikuwa ikiongoza kwa kutumia Fedha nyingi kununua Wachezaji wakimwaga £222.32m.
Kwa vile China Dirisha lilikuwa wazi hadi Jana, Klabu za CSL huko China zilifanikiwa kuivunja Rekodi hiyo ya EPL ambayo ilikuwa ikitamba Duniani.
China ilianza kutunisha Misuli yao ya Fedha tangu Mwaka mmoja uliopita walipomwaga £292.94m kuwanunua Wachezaji wengi wakiwemo kina Ramires, Jackson Martinez na Alex Teixeira huku wakivunja Rekodi yao ya kumnunua Mchezaji kwa Dau kubwa mara 3 ndani ya Mwezi mmoja
Ilitarajiwa kuwa safari hii China haitatumia Fedha nyingi kununua Wachezaji baada ya FA yao kuweka vizuizi kadhaa kwa Klabu kuwa na Wachezaji wageni wasiozidi Watatu kwa Mechi moja.
==========
2017 MATUMIZI KUNUNUA WACHEZAJI:
***£=Pauni Milioni
1. CSL - 333.54
2. EPL - 222.32
3. Bundesliga - 86.84
4. Serie A - 83.24
==========
Lakini Shanghai SIPG chini ya Kocha Andre Villas-Boas ambayo Msimu uliopita iliweka Rekodi ya kuvunja Dau la Uhamisho kwa kutumia £47.43m kumnunua Mbrazil Hulk kutoka Klabu ya Urusi Zenit St Petersburg, Mwezi Januari iliilipa Chelsea £51m kumnunua Oscar.
Nao Shanghai Shenhua, waliotumia Dau dogo la £8.93m kumnunua Mchezaji wa Timu ya Argentina Boca Juniors Carlis Tevez, waliweka Rekodi ya Dunia na kumfanya Mchezaji huyo wa zamani wa West Ham, Man United, Man City na Juventus kuwa ndie anaezoa Mshahara mkubwa Duniani kwa kulipwa £615,000 kwa Wiki.
Wachezaji wengine waliotimkia China kwenye Dirisha la Uhamisho lililofungwa Jana ni Axel Witsel wa Juve (£17m/€20m) kwenda Tianjin Quanjin chini ya Kocha Lejendari wa Italy Fabio Cannavaro ambae pia alimnasa Alexandre Pato wa Brazil kwa Dau la £15.3m.
Nayo Changhun Yatai iliilipa Watford £19.81m kumbeba Odion Ighalo ambae hakuwika huko England.
Mbrazil Hernanes alijiunga na Hebei China Fortune waliyoilipa Juve  £6.8m huku Christian Bassogog akilipiwa £3.74m kwenda Henan Jianye kutoka Aalborg baada kung'ara akiwa na Cameroon kwenye AFCON 2017 walipotwaa Ubingwa wa Africa huko Gabon Mwezi uliopita.

EMIRATES FA CUP – DROO ROBO FAINALI: MABINGWA MAN UNITED KUTUA STAMFORD BRIDGE KUIVAA CHELSEA!

EMIRATES-FACUP-2017-SITDROO ya Raundi ya 6 ya EMIRATES FA CUP, ambayo ndiyo Robo Fainali, imefanyika Leo na Mabingwa Watetezi Manchester United wataenda huko Stamford Bridge kupambana na Vinara wa EPL, Ligi Kuu England.

Mechi hizi zitachezwa Wikiendi ya Machi 10 hadi 13.

DROO KAMILI:

Chelsea v Man Utd

Middlesbrough v Huddersfield au Man City

Tottenham v Millwall

Sutton United au Arsenal v Lincoln City

+++++++++++++++++++

JE WAJUA?

-FA CUP 2016/17, ambalo pia hujulikana kama FA Challenge Cup, ni mara ya 136 kushindaniwa kila Mwaka tangu lilipoanzishwe na linatambuliwa kama ndio Mashindano ya kale kupita yote Duniani.

-Kombe hili linadhaminiwa na Kampuni ya Ndege ya Emirates na kwa sababu za kiudhamini linaitwa Emirates FA Cup.

-Timu 736 zilikubaliwa kushiriki Mashindano haya Msimu huu na yalianza kwa Raundi ya Awali na yatafikia Tamati kwa Fainali itakayochezwa Uwanjani Wembley Jijini London hapo Mei 27, 2017.

-Mshindi wa FA CUP ataingizwa Hatua ya Makundi ya UEFA EUROPA LIGI Msimu wa 2017/18.

-Bingwa Mtetezi ni Manchester United.

+++++++++++++++++++

Raundi ya 5 ya FA CUP itakamilika Jumatatu Usiku wakati Timu ambayo haipo kwenye Mfumo rasmi wa Ligi huko England, Sutton United, wakiwa Wenyeji wa Arsenal.

FA CUP

Ratiba:

Raundi ya 5

Jumatatu Februari 20

**Saa za Bongo

2255 Sutton United v Arsenal               

TAREHE MUHIMU:

HATUA

RAUNDI

DROO

MECHI

Raundi za Awali

Raundi ya Awali kabisa

8 Julai 2016

6 Agosti 2016

Raundi ya Awali

20 Agosti 2016

Raundi ya 1 Mchujo

15 Agosti 2016

3 Septemba 2016

Raundi ya 2 Mchujo

5 Septemba 2016

17 Septemba 2016

Raundi ya 3 Mchujo

19 Septemba 2016

1 Oktoba 2016

Raundi ya 4 Mchujo

3 Oktoba 2016

15 Oktoba 2016

Mashindano rasmi

Raundi ya 1

17 Oktoba 2016

5 Novemba 2016

Raundi ya 2

7 Novemba 2016

3 Desemba 2016

Raundi ya 3

5 Desemba 2016

7 Januari 2017

Raundi ya 4

Kujulishwa

28 Januari 2017

Raundi ya 5

Kujulishwa

18 Februari 2017

Raundi ya 6 [Robo Fainali]

Kujulishwa

11 Machi 2017

Nusu Fainali

Kujulishwa

22 na 23 Aprili 2017

FAINALI

27 Mei 2017

 

LISTI FIFA/COCA COLA UBORA DUNIANI: ARGENTINA BADO 1, BRAZIL 2, EGYPT JUU AFRIKA, TANZANIA MPOROMOKO TU, NI YA 158!

FIFA-RANKINGSFIFA Leo imetoa Listi mpya ya ubora Duniani kwa nchi Wanachama wake, ambayo huitwa Listi ya FIFA/Coca Cola Ubora Duniani, na Vinara wake bado ni Argentina wakifuatia Brazil na kwa Afrika Egypt ndio wapo juu kabisa huku Tanzania ikishuka Nafasi 2 na kukamata Namba 158.

5 Bora kwenye listi hiyo zimebaki zile zile bila mabadiliko na nazo ni Argentina (1), Brazil (2), Germany (3), Chile (4) na Belgium (5).

Kwa Afrika, Nchi ambayo iko juu kabisa ni Egypt, waliotolewa Fainali ya AFCON 2017, ambao sasa wapo Nafasi ya 23 baada kupanda Nafasi 12 wakifuata Senegal walio Nafasi ya 31 na Mabingwa Wapya wa Afrika ambao ndio waliwafunga Egypt, Cameroun, wapo Nafasi ya 33 baada kupaa Nafasi 29.

Listi nyingine ya FIFA/Coca Cola Ubora Duniani itatolewa itatolewa Tarehe 9 Machi 2017.

FIFA LIST YA UBORA DUNIANI – 20 BORA:

NAFASI

NCHI

NAFASI ILIZOPANDA AU KUSHUKA

1

Argentina

0

2

Brazil

0

3

Germany

0

4

Chile

0

5

Belgium

0

6

France

1

7

Colombia

-1

8

Portugal

0

9

Uruguay

0

10

Spain

0

11

Switzerland

0

12

Wales

0

13

England

0

14

Poland

1

15

Italy

1

16

Croatia

-2

17

Mexico

1

18

Peru

1

19

Costa Rica

-2

20

Iceland

1

SERIE A: JUVE YAIDUNDA INTER KATIKA DERBY D'ITALIA, YAZIDI KUPAA KILELENI!

Derby dItaliaBAO safi la Juan Cuadrado limewapa Vinara wa Serie A Juventus ushindi wa 1-0 dhidi ya Inter Milan na kuwaweka Pointi 6 mbele ya Timu ya Pili Napoli huku wakiwa na Mechi 1 mkononi.

Kipigo hicho cha Inter Milan kwenye Mechi inayobatizwa ‘Derby d'Italia’ kimevunja wimbi laoSERIEA-FEB5 la ushindi wa Mechi 7 mfululizo za Serie A.

Kwa Juve hiyo ilikuwa Mechi yao ya 28 kushinda mfululizo Uwanjani kwao.

Kwenye Mechi nyingine zilizochezwa Jana, Lazio waliitwanga Timu ya Mkiani Pescara Bao 6-2 huku Marco Parolo akipiga Bao 4.

Ushindi huo umewaweka Lazio Nafasi ya 4 wakiwa na Pointi 43, Pointi 4 nyuma ya Timu ya 3 AS Roma.

VIKOSI:

JUVENTUS: Buffon; Lichtsteiner (Dani Alves 80), Bonucci, Chiellini, Alex Sandro; Khedira, Pjanic; Cuadrado (Marchisio 70), Dybala (Rugani 84), Mandzukic; Higuain

INTER MILAN: Handanovic; Murillo, Medel, Miranda; Candreva (Eder 58), Gagliardini, Brozovic (Kondogbia 58), D'Ambrosio; Joao Mario (Palacio 79), Perisic; Icardi

REFA: Rizzoli

SERIE A

Matokeo

Jumapili Februari 5

AC Milan 0 Sampdoria 1

Atalanta 2 Cagliari 0

Chievo Verona 0 Udinese 0

Empoli 1 Torino 1

Pescara 2 Lazio 6

Genoa 0 Sassuolo 1

Palermo 1 Crotone 0

Juventus 1 Inter Milan 0