FIFA LISTI UBORA DUNIANI: BRAZIL NAMBARI WANI, EGYPT JUU AFRIKA, TANZANIA YAPANDA 22!

FIFA-RANKINGSWAKATI Brazil imekamata Nambari Wani Duniani katika Listi ya Ubora Duniani iliyotolewa hii Leo na FIFA, Tanzania imechomoka kutoka Nafasi ya 157 iliyoshikilia Mwezi uliopita na kupanda Nafasi 22 juu.

Brazil imerejea kileleni kwa mara ya kwanza baada ya Miaka 6 na hili limekuja baada ya mafanikio makubwa chini ya Kocha wao Tite ambae ameshinda Mechi 9 mfululizo tangu atwae wadhifa Mwaka Jana wakifunga Bao 25 na kufungwa 2 tu.

Hivi karibuni Brazil ilishinda Mechi zake zote 2 za Kundi la Nchi za Marekani ya Kusini na kuwa Nchi ya Kwanza kufuzu kuingia Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia.

Wiki iliyopita, Brazil kwanza iliifunga Uruguay 4-0 huko Montevideo na Siku 3 baadae kuichapa 3-0 Paraguay huko Sao Paolo, Brazil.

Brazil wameitoa Argentina kwenye Namba 1 ya Listi ya Ubora baada ya Argentina hivi karibuni kushinda Mechi 1 tu, walipoifunga Chile 1-0, na kisha kuchapwa 2-0 na Bolivia.

Argentina sasa wameshika Namba 2 baada kukaa kileleni kwa Miezi 12 walipowang'oa Mabingwa wa Dunia Germany ambao sasa wako Nafasi ya 3.

Katika 10 Bora Nchi pekee mpya ni Switzerland ambayo ipo wa 9 baada ya kuifunga Latvia 1-0 kwenye Mechi ya Kundi lao la Ulaya la kusaka kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018.

Nao Vigogo Netherlands, baada ya Wiki hii kuchapwa na Bulgaria na Italy, wamezidi kuporomoka kwa Nafasi 11 na kuangukia Nafasi ya 32 ikiwa ndio Nafasi ya chini kabisa katika Historia yao.

Wengine walioporomoka mno ni Uruguay walioshuka Nafasi 6 na kuangukia Nafasi ya 15 baada Wiki hii kuchapwa na Brazil na Peru.

Wakati Egypt ndiyo Timu ya juu kabisa kwa Afrika ikishika Nafasi ya 19, Tanzania sasa ipo Nafasi ya 135 ikitokea Nafasi ya 157 baada ya kuzifunga Botswana na Burundi Nchi ambazo ziko juu yake.

FIFA LISTI YA UBORA DUNIANI – 20 BORA:

1       Brazil

2       Argentina

3       Germany

4       Chile

5       Colombia

6       France

7       Belgium

8       Portugal

9       Switzerland

10      Spain

11      Poland

12      Italy

13      Wales

14      England

15      Uruguay

16      Mexico

17      Peru

18      Croatia

19      Egypt

20      Costa Rica

 

WENGER ADOKEZA KUBAKI ARSENAL ILA WACHEZAJI WAPYA KULETWA NA KLABU SI YEYE!

>NI KILIO KWA WADAU WA ‘NI ARSENAL FC SI ARSENE FC’!

WENGER-OUT-APR1Arsene Wenger amedokeza kubakia Klabuni Arsenal pale alipotoboa anafanya mipango kwa ajili ya Msimu Mpya lakini akasema Wachezaji Wapya watatua hapo kwa ajili ya Klabu na si yeye.

Hata hivyo, Wenger amesisitiza mipango ya Msimu Mpya anaifanya hata kama angekuwa anaondoka mwishoni mwa Msimu huu.

Habari hizi zitakuja kama pigo kubwa kwa Washabiki wanaoshinikiza Wenger aondoke kwa kutoleta mafanikio yeyote tangu 2004 walipotwaa Ubingwa wa England kwa mara ya mwisho.

Wadau hao, wenye Kampeni iliyobatizwa ‘NI ARSENAL FC SI ARSENE FC’, ni wazi watakatishwa tamaa na habari hizi baada ya presha yao kupamba moto hasa baada ya Arsenal kucharazwa 10-2 katika Mechi 2 na Bayern Munich na kutupwa nje ya UCL, UEFA CHAMPIONZ kwenye Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ikiwa ni mara ya 7 mfululizo kufeli Hatua hiyo ya Mashindano hayo.

Inaelekea sasa Wenger atasaini Mkataba Mpya wa Miaka Miwili na moja ya Wachezaji Wapya ambao Wenger amependekeza watue Emirates ni Mchezaji wa Borussia Dortmund, Marco Reus.

Pia inasemekana Wenger sasa anasaka mbadala wa Mesut Ozil na Alexis Sanchez ambao inadaiwa wako mbioni kuhama licha ya Wenger mwenyewe kutamka Juzi wanataka kubaki na mazungumzo nao yanaendelea vizuri.

Akiosha mikono kuwa Wachezaji wapya hutua Arsenal si kwa sababu yake, Wenger ametamka: “Arsenal ni Brandi ya Dunia hivi Leo, inaheshimika Dunia nzima. Jina la Arsenal ni kubwa kupita Jina langu na kuja Arsenal ni muhimu…huji kwa Arsene Wenger..unakuja kwa Arsenal!”

KOMBE LA DUNIA 2026: FIFA YATOA MGAO WA TIMU FAINALI ZA TIMU 48!

>AFRIKA YAPEWA 9 TOKA 5 ZA SASA!

FIFA-WC2026-TIMU48FIFA imetoboa mipango yake ya jinsi Nafasi 48 za kwenye Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2026 zitakavyogawiwa.

Fainali hizo, ambazo Mwenyeji wake hajaamuliwa, zitafuatia zile za 2018 zitakazochezwa Russia na zile za 2022 ambazo zitakuwa Qatar.

Mapendekezo haya ya FIFA, yaliyopitishwa na Rais wa FIFA pamoja na Mashirikisho yote 6 Mabara ya FIFA, yanatarajiwa kupata baraka za Baraza la FIFA hapo Mei 9.

Mwezi Januari, Wanachama wa FIFA walipiga Kura na kuamua kuzipanua Fainali za Kombe la Dunia kutoka Timu 32 za sasa hadi 48.

MGAO wa Nchi kwenye Fainali:

-Mashirikisho 6 ya Mabara ya FIFA [UEFA/CAF/CONMEBOL/CONCACAF/AFC/OCAENIA] yatakuwa na si chini ya Timu 1 kwenye Fainali huku kukiwa hamna Mechi za Mchujo kati ya Nchi za Mashirikisho hayo kama ilivyon sasa.

-Mwenyeji wa Fainali anatinga moja kwa moja Fainali na nafasi yake itatoka kwenye ile ya Shirikisho lake.

-Mgao wa Nafasi 46 [Bado 2 zitatoka Mchujo]:

Africa - 9 (toka 5)

Asia - 8 (toka 4 au 5)

Europe - 16 (toka 13)

North, Central America and Caribbean - 6 (toka 3 au 4)

Oceania - 1 (toka 0 au 1)

South America - 6 (toka 4 au 5)

Mechi za Mchujo za kupata Timu 2 za mwisho kucheza Fainali:

Timu 6 zitacheza Mechi za Mchujo ili kuamua Nafasi 2 za Fainali zilizobakia.

Kila Shirikisho la FIFA litatoa Nchi 1, isipokuwa UEFA, na moja itatoka kwenye Shirikisho la Nchi Mwenyeji wa Fainali za 2026.

Inapekezwa Mechi za Mchujo kuchezwa Novemba 2025 katika Nchi Mwenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2026.

NEYMAR 'STAA', MESSI 'JELA', BRAZIL YAPAA, ARGENTINA PWAAA!!!

=URUGUAY YAPIGWA TENA!

CONMEBOL

Kombe la Dunia – Russia 2018

Mechi za Makundi

Matokeo:

Jumanne Machi 28, 2017         

Bolivia 2 Argentina 0

Jumatano Machi 29, 2017         

Ecuador 2 Colombia 0

Chile 3 Venezuela 1    

Brazil 3 Paraguay 0   

Peru 2 Uruguay 1
++++++++++++++++++++++
WC-2018-SA-QUALIFIERS-1Brazil imeendelea kung'ara wakiongozwa na Staa wao mkubwa Neymar walipoifunga Paraguay 3-0 kwenye Mechi ya Kanda ya Nchi za Marekani ya Kusini kusaka kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia.
Wakati Brazil ikipaa kileleni na kuongoza kwa Pointi 9 mbele ya Timu ya Pili Colombia, Argentina waliporomoka hadi Nafasi ya 5 kutoka ya 3 Jana walipochapwa 2-0 na Bolivia huku wakicheza bila ya Kepteni wao Lionel Messi aliefungiwa Mechi 4 kwa kumtolea Matusi Refa Msaidizi Majuzi walipoifunga Chile 1-0.
++++++++++++++++++++++++
JE WAJUA?
-CONMEBOL itatoa Nchi 4 kutinga Fainali za Kombe la Dunia huko Russia Mwaka 2018.
-Nchi hizo zinaweza kuwa 5 ikiwa Timu itakayomaliza Nafasi ya 5 kwenye Kundi lao itashinda Mechi ya Mchujo dhidi ya Timu nyingine toka Bara jingine ambayo itakuwa ni moja toka Kanda ya Oceania yenye Nchi za Visiwani ambazo ni New Zealand, New Caledonia, Fiji, Papua New Guinea, Siolomon Islands na Tahiti.
++++++++++++++++++++++++
Philippe Coutinho ndie aliewapa Bao la Kwanza Brazil dhidi ya Paraguay katika Dakika ya 34 na Neymar kupiga la Pili Dakika ya 63 licha ya kukosa Penati huku Marcelo akifunga la 3 Dakika ya 86.
Huko Las Paz, Wenyeji Bolivia waliichapa Argentina 2-0 iliyocheza bila Nahodha wao Messi ambae Masaa kadhaa kabla Mechi hiyo alishushiwa Kifungo cha Mechi 4.
Mechi nyingine za Argentina waliobakisha Mechi 4 za Kanda hii kufuzu Russia ambazo Messi atazikosa ni zile dhidi ya Brazil, Uruguay na Venezuela baadae Mwaka huu.
 
Bao za Bolivia zilifungwa na Juan Carlos Arce nq Marcelo Martins wakati Argentina wakimpoteza Beki wa Everton Ramiro Funes Mori alietolewa nje kwa Machela baada kuumia Goti.
Nao Colombia wamepaa hadi Nafasi ya Pili baada kuichapa Ecuador 2-0 kwa Bao za James Rodriguez na Juan Cuadrado.
Uruguay nao wamechezea kichapo cha pili mfululuzo baada Juzi kupigwa 4-1 na Brazil na Asubuhi hii kufungwa 2-1 na Peru.
Bao za Mechi hii zilufungwa Dakika za 35 na 62 kwa Peru kupitia Paolo Guerrero  na Uruguay kufunga Dakika ya 30 kwa Bao la Carlos Sanchez Arcosa lakini wakawa Mtu 10 kuanzia Dakika ya 76 baada ya Jonathan Urretaviscaya kupewa Kadi Nyekundu.
 

KOMBE LA DUNIA 2018: JUMANNE MAREKANI KUSINI ‘VITANI’ KUGOMBEA POINTI MUHIMU, BRAZIL YA KWANZA KWENDA RUSSIA?

WC-2018-SA-QUALIFIERS-1UKIWAONDOA VINARA BRAZIL, Nchi kadhaa za Kanda ya Marekani ya Kusini Jumanne zitakuwa kwenye ‘Vita Kuu’ kugombea Pointi muhimu zitakazowaweka relini ili kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Brazil.

Brazil, baada ya kushinda Mechi 7 mfululizo tangu Kocha Tite atwae wadhifa Mwaka Jana, wako raha mustarehe kileleni mwa Kanda hii wakiwa na Pointi 30 wakifuatia Uruguay 23 na Argentina wenye 22, Colombia 21 na Ecuador 20.

Ikiwa Brazil watashinda Mechi yao ya Jumanne na Matokeo mengine kuwapendelea wao, basi wanaweza  kuwa Nchi ya Kwanza kufuzu kwenda Russia kucheza Fainali za Kombe la Dunia Mwaka 2018 huku wakiwa wamebakiza Mechi 4.

++++++++++++++++++++++++

JE WAJUA?

-CONMEBOL itatoa Nchi 4 kutinga Fainali za Kombe la Dunia huko Russia Mwaka 2018.

-Nchi hizo zinaweza kuwa 5 ikiwa Timu itakayomaliza Nafasi ya 5 kwenye Kundi lao itashinda Mechi yaWC-2018-SA-TEBO-MAR24 Mchujo dhidi ya Timu nyingine toka Bara jingine ambayo itakuwa ni moja toka Kanda ya Oceania yenye Nchi za Visiwani ambazo ni New Zealand, New Caledonia, Fiji, Papua New Guinea, Siolomon Islands na Tahiti.

++++++++++++++++++++++++

Vita Kuu

Kwenye Mechi hizi za Jumanne, Mechi ambayo itakuwa na mvutano mkubwa ni ile ya Ecuador na Colombia ambayo kila mmoja anataka kumng’oa mwenzake Nafasi ya Nne ambayo ndiyo ya mwisho kufuzu moja kwa moja kwenda Fainali Russia.

Mechi hii ambayo itachezwa Nyumbani kwa Ecuador huko Estadio Olimpico Atahualpa, Mjini Quito, ni wazi inaipa faida kubwa Ecuador kwani Uwanja huo ni ‘kaburi’ la Timu ngeni kutokana na hali yake kwani upo juu mno kutoka Usawa wa Bahari na kuwakosesha Wageni pumzi ya kucheza kwa nguvu Dakika zote 90.

Ecuador, chini ya Kocha Gustavo Quinteros, itawakosa Christian Noboa na Miller Bolanos waliofungiwa Mechi 1 kutokana na kulimbikiza Kadi za Njano wakati Colombia chini ya Kocha, Jose Pekerman, wanasaka ushindi wao wa kwanza huko Quito tangu Mwaka 1996 lakini watamkosa Majeruhi Staa wao Luis Muriel ingawa mbadala wake anaweza kuwa Miguel Angel Borja.

Kwingineko

Huko Mjini Lima, Peru watakuwa Wenyeji wa Uruguay ambao Juzi walitandikwa 4-1 na Brazil huko kwao Montevideo lakini wana kibarua kigumu kuifunga Uruguay ambayo wamewahi kuifunga mara 1 tu kwenye Mechi za Kombe la Dunia.

Tena safari hii ni ngumu zaidi kwa Peru kwani kwenye Mechi hii Uruguay watakuwa nao tena Mastaa wao Fernando Muslera na Luis Suarez walioikosa Mechi iliyopita na Brazil.

Nao Bolivia, ambao wako Nafasi ya 9 wakiwa na Pointi 7, wataikaribisha Argentina walio Nafasi ya 3 na wana Pointi 22 na ambao watawakosa Wachezaji wao Javier Mascherano na Gonzalo Higuain ambao wako Kifungoni na pia kuwa na Majeruhi.

Chile, ambao wako Nafasi ya 6 wakiwa na Pointi 20, wako Nyumbani kucheza na Timu ya Mkiani Venezuela huku wakitegemea ushindi laini hasa baada ya Staa wao Arturo Vidal kurejea Kikosini.

Nao Vinara Brazil, ambao watakuwa Nyumbani kucheza na Paraguay, wanaweza kuwa Timu ya Kwanza kutinga Fainali Russia ikiwa watashinda huku Ecuador na Chile zikifungwa.

Paraguay hawajawahi kuifunga Brazil huko kwao na mara ya mwisho kuambua Pointi 1 ni Mwaka 1985.

CONMEBOL

Kombe la Dunia – Russia 2018

Mechi za Makundi

Ratiba:

**Saa za Bongo

Jumanne Machi 28, 2017         

2330 Bolivia v Argentina

Jumatano Machi 29, 2017         

0001 Ecuador v Colombia

0100 Chile v Venezuela     

0345 Brazil v Paraguay     

O515 Peru v Uruguay