FIFA YATANGAZA TUZO ZAO ZA UBORA BAADA KUACHANA NA BALLON D’OR!

>>WAGOMBEA 23 WA TUZO YA MCHEZAJI BORA DUNIANI 2016 KUTAJWA IJUMAA HII!

FIFA-BESTLEO FIFA imetangaza Mfumo wake wa kutoa Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani kwa Mwaka 2016 baada ya kuachana na Ballon d’Or.

Tuzo ya Ballon d’Or ilibuniwa na Jarida la France Football kuanzia Mwaka 1956 na hasa ilikuwa Tuzo ya Mchezaji Bora Ulaya na kuanzia Mwaka 1991 FIFA wakaanzisha Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani na kuendelea hadi 2009 walipoiunganisha na Ballon d’Or na kuitwa FIFA Ballon d’Or kuanzia Mwaka 2010.

Lakini muungano huo umekufa Mwaka huu na Ballon d’Or kurejea mikononi mwa France Football ambao tayari washatangaza Listi ya Wagombea wao 30.

Leo FIFA imetangaza Tuzo zao ambazo zitakuwa 8 na Washindi kutangazwa rasmi kwenye Hafla maalum itakayofanyika huko Zurich Januari 9.

Kwenye Tuzo hizi za FIFA Kura za Makocha na Manahodha wa Timu za Taifa za Wanachama wa FIFA ndio zitakuwa Asilimia 50 na zilizobaki 50 zitatokana na Kura za Mtandaoni za Umma Duniani kote pamoja ambazo ni asilimia 25 na Asilimia iliyobaki 25 ni zile za Wanahabari maalum 200 toka kila Kona ya Dunia.

Listi ya Wagombea 23 wa Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani kwa Mwaka 2016 itatangazwa Ijumaa Novemba 4 na baadae utafanyika mchujo kubakisha Wagombea Watatu ambao watatangazwa Desemba 2.

FIFA – Tuzo za Ubora zitakazotolewa:

-Mchezaji Bora Duniani 2016 [The Best Fifa Men's Player 2016]

-Mchezaji Bora Duniani 2016 kwa Kinamama [The Best Fifa Women's Player 2016]

-Kocha Bora kwa Wanaume 2016 [The Best Fifa Men's Coach 2016]

-Kocha Bora kwa Wanawake 2016 [The Best Fifa Women's Coach 2016]

-Tuzo ya Puskas 2016 kwa Goli Bora [The Fifa Puskas Award 2016 for goal of the year]

-Tuzo ya Uchezaji wa Haki 2016 [The Fifa Fair Play Award 2016]

-Tuzo ya Mashabiki 2016 [The Fifa Fan Award 2016]

-Kikosi Bora 2016 [Fifa FifPro World11]

 

CAF KOMBE LA SHIRIKISHO-FAINALI: TP MAZEMBE YAPATA SARE MUHIMU YA UGENINI!

CAF-CC-MO-TPMechi ya kwanza ya Fainali ya Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho ilichezwa Jana Usiku huko Bilda Nchini Algeria ndani ya Stade Mustapha Tchaker nabWenyeji MO Bejaia kutoka Sare 1-1 na TP Mazembe ya Congo DR.
Bao za Mechi hiyo zilufungwa kila kipindi na Jonathan Bolingi ndie alieipa TP Mazembe Bao Dakika ya 43 na MO Bejaia kusawazisha Dakika ya 66 Mfungaji akiwa Yaya Faouzi.
Hii ni mara ya pili kwa Timu hizi kukutana kwenye Mashindano haya Mwaka huu kwani zilikuwa Kundi moja ambalo pia Yangavya Tanzania ilikuwemo na TP Mazembe ndio waliibuka Vinara na MO kushika Nafasi ya Pili huku zikitoka 0-0 huko Algeria na TP Mazembe kushinda 1-0 huko Lubumbashi kwa Bao la Dakika ya 62 la Mzambia Rainford Kalaba.
Mechi ya Marudiano ya Fainali hii itachezwa huko Stade TP Mazembe Mjini Lubumbashi Nchini Congo DR hapo Novemba 6.
VIKOSI:
MO Bejaia: Rahmani, Ferhat (Belkacemi 60), Rahal, Yaya, Khadir, Sidibe, Athmani, Betorangal, Benmelouka, Salhi, Bouali.
Mazembe: Sylvain Gbohouo - Issama Mpeko, Salif Coulibaly, Roger Assale, Merveille Bope, Nathan Sinkala, Jona.

CAF KOMBE LA SHIRIKISHO: LEO FAINALI YA WENZA WA YANGA, MO BEJAIA v TP MAZEMBE!

CAF-CC-MO-TPLEO ni Mechi ya kwanza ya Fainali ya Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho zikihusisha Timu 2 ambazo zilikuwa Kundi moja na Mabingwa wa Tanzania Bara Yanga awali kwenye Mashindano hayo.

Leo huko Bilda Nchini Algeria ndani ya Stade Mustapha Tchaker Wenyeji MO Bejaia watawakaribisha TP Mazembe ya Congo DR.

Mechi hii, ambayo itarushwa moja kwa moja na TV ya SuperSport kwenye SS9, itaanza Saa 4 na Nusu Usiku Saa za Tanzania na kuchezeshwa na Refa kutoka Seychelles Bernard Camille.

Timu zote hizi mbili zilitinga Fainali kwa faida ya Goli la Ugenini baada ya Sare kwenye Nusu Fainali wakati MO Bejaia walipotoka 1-1 na FUS Rabat ya Morocco na TP Mazembe kufungana na Etoile du Sahel ya Tunisia.

Wakati MO Bejaia wanawania Taji la Kwanza la CAF Barani Afrika, TP Mazembe ni Maveterani wa Mataji hayo wakiwa wamezoa Ubingwa wa CAF CHAMPIONZ LIGI mara 5, Kombe la Washindi mara 1 na CAF Super Cup mara 3.

Wakiwa chini ya Kocha wao Nasser Sendjack, MO Bejaia wamejitayarisha vyema na wakitegemea matokeo mema.

Nae Kocha wa TP Mazembe, Hubert Velud, anaamini Gemu hii ni ngumu kutabirika hasa kufuatia Matokeo yao ya awali kwenye Kundi lao ambalo TP Mazembe ndio walikuwa Kinara na MO kushika Nafasi ya Pili huku zikitoka 0-0 huko Algeria na TP Mazembe kushinda 1-0 huko Lubumbashi kwa Bao la Dakika ya 62 la Mzambia Rainford Kalaba.

Mechi ya Marudiano ya Fainali hii itachezwa huko Stade TP Mazembe Mjini Lubumbashi Nchini Congo DR hapo Novemba 6.

 

LEJENDARI WA BRAZIL CARLOS ALBERTO AFARIKI!

CARLOS-ALBERTOLEJENDARI wa Brazil Carlos Alberto ambae alikuwa Kepteni wa Brazil iliyotwaa Kombe la Dunia Mwaka 1970 amefariki Dunia akiwa na Miaka 72.
Kwenye Fainali ya Kombe la Dunia Mwaka 1970 alifunga Bao safi sana toka Pasi murua ya Pele wakati Brazil inaitwanga Italy 4-1 na kubeba Kombe.
Bao hilo lipo kwenye Hazina ya Mabao murua na ya kumbumkumbu Duniani ambayo yamehifadhiwa kwenye Makumbusho ya Soka.
Brazil hiyo ya Mwaka 1970 ndiyo inayodaiwa kuwa ni Kikosi chao Bora kupita vyote na mbali ya kuwa na Alberto na Pele walikuwemo Masupastaa Jairzinho, Tostao na Rivelino.
Alberto, alieichezea Brazil mara 53, alikuwa Fulbeki wa Kulia aliechezea Klabu za Brazil za Fluminense na Santos. 
Alberto ni mmoja wa Wachezaji walioteuliwa kwenye Kikosi Bora cha Karne hapo Mwaka 1998 na pia Mwaka 2004 alikuwemo kwenye Wachezaji 100 Bora Duniani katika Historia ya Soka
Baada kustaafu uchezaji, Carlos Alberto alikuwa Kocha wa Klabu huko Oman na Azerbaijan.
MOLA AILAZE ROHO YAKE MAHALA PEMA PEPONI.
AMIN.

BALLON D'OR: LA LIGA YATAWALA, INA WAGOMBEA 13 KATI YA 30!

BALLONDORLA LIGA, Ligi ya Spain, imezipita Ligi nyingine kubwa za Ulaya kwa kutoa Wagombea 13 kati ya 30 wa Tuzo ya Ballon D’Or.

Ligi Kuu England imetoa 8, Bundesliga 5 Serie A 3 na ile ya Ureno, Primeira Liga, ina Mmoja tu.

Wachezaji wanaocheza La Liga ambao wapo kwenye kinyang’anyiro cha Ballon D’Or ni Lionel Messi, Cristiano Ronaldo, Neymar, Luis Suarez, Gareth Bale, Antoine Griezmann, Diego Godin, Andres Iniesta, Koke, Toni Kroos, Luka Modric, Pepe na Sergio Ramos.

Lakini Spain sio Taifa lenye Wagombea wengi, wanao Watatu tu,na hao Wagombea wanaoongoza kwa Utaifa ni wale kutoka Argentina na France wenye Wanne Wanne kila mmoja.

Wagombea kutoka Spain ni wakati Wagombea wa Argentina ni Messi, Gonzalo Higuain, Paulo Dybala na Sergio Aguero na wale wa France ni Griezmann, Hugo Lloris, Dimitri Payet na Paul Pogba.

Kitaifa, England ina Mgombea Mmoja tu ambae ni Jamie Vardy ambae anatoka Ligi Kuu England ambako Wagombea wengine toka Ligi hiyo ni Lloris, Payet, Pogba, Aguero, Kevin De Bruyne, Zlatan Ibrahimovic na Riyad Mahrez.

MAJINA YA WAGOMBEA 30:

1

Sergio Aguero (Manchester City)

Pierre-Emerick Aubameyang (Borussia Dortmund)

Gareth Bale (Real Madrid)

Gianluigi Buffon (Juventus)

Cristiano Ronaldo (Real Madrid)

Kevin De Bruyne (Manchester City)

Paulo Dybala (Juventus)

Diego Godin (Atlético Madrid)

Antoine Griezmann (Atlético Madrid)

10 

Gonzalo Higuain (Napoli/Juventus)

11 

Zlatan Ibrahimovic (PSG/Manchester United)

12 

Andrés Iniesta (Barcelona)

13 

Koke (Atletico Madrid)

14 

Toni Kroos (Real Madrid)

15 

Robert Lewandowski (Bayern Munich)

16 

Hugo Lloris (Tottenham)

17 

Riyad Mahrez (Leicester)

18 

Lionel Messi (Barcelona)

19 

Luka Modric (Real Madrid)

20 

Thomas Muller (Bayern Munich)

21 

Manuel Neuer (Bayern Munich)

22 

Neymar (Barcelona)

23 

Dimitri Payet (West Ham United)

24 

Pepe (Real Madrid)

25 

Paul Pogba (Manchester United)

26 

Rui Patricio (Sporting Portugal)

27 

Sergio Ramos (Real Madrid)

28 

Luis Suarez (Barcelona)

29 

Jamie Vardy (Leicester City)

30 

Arturo Vidal (Bayern Munich)