CRISTIANO RONALDO - NAMBA ZINAZOMBATIZA ULEJENDARI!

CRISTIANO RONALDO ndie Mchezaji Bora Duniani.
Juzi Usiku ndani ya Estadio Santiago Bernabeu alionyesha tena umahiri wake alipopiga Hetitriki wakati Real Madrid ikiitandika Atletico Madrid 3-0 katika Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Hetitriki hiyo imeweka Rekodi na kumfanya Ronaldo awe Mchezaji wa Kwanza kufunga Hetitriki 2 mfululizo kwenye UCL.
Kwenye Raundi iliyopita, Ronaldo alifunga Bao 5 kati ya 6 wakati Real Madrid ikiitoa Bayern Munich ya Germany kwa Jumla ya Bao 6 katika Mechi 2.
Ronaldo pia ndie Mfungaji Bora katika Historia ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, akiwa na Jumla ya Mabao 103.
PATA PICHA INAYOONYESHA NAMBA ZAKE:
RONALDO-NAMBA-LEJENDARIpDABI LONDON KASKAZINI, SPURS YAIWASHA ARSENAL 2-0!

EPL, LIGI KUU ENGLAND

Matokeo:

Jumapili Aprili 30

Manchester United 1 Swansea City 1               

Everton 0 Chelsea 3         

Middlesbrough 2 Manchester City 2                 

Tottenham Hotspur 2 Arsenal 0   

+++++++++++++++++++++++++++               

SPURS-JUUBAO 2 ndani ya Dakika 3 Leo zimewapa ushindi wa 2-0 Tottenham Hotspurs kwa kuwabwaga Mahasimu wao Arsenal kwenye Mechi yaEPL, Ligi Kuu England, iliyochezwa huko White Hart Lane ikiwa ni Dabi ya Jiji London Kaskazini.Hadi Haftaimu Gemi hii ilikuwa 0-0 lakini Dakika ya 55 kizaazaa Golini mwa Arsenal kulifanya Mpira umfikie Dele Alli alieukwamisha Mpira wavuni.

Chini ya Dakika 3 baadae, Gabriel alimwangusha Harry Kane ndani ya Boksi na Refa Michael Oliver kutoa Penati iliyofungwa na Harry Kane.

Ushindi huu umewachimbia Spurs Nafasi ya Pili wakiwa Pointi 4 nyuma ya Vinara Chelsea huku Gemu zikibaki.

Arsenal wanabika Nafasi ya 6 wakiwa Pointi 5 nyuma ya Timu ya 5 Man United.

VIKOSI:

TOTTENHAM:Lloris; Trippier [Walker 88'], Alderweireld, Vertonghen, Davies; Dier, Wanyama; Son EPL-APR30B[Dembélé 79'], Eriksen; Dele [Sissoko 91'], Kane

Akiba: Vorm, Walker, Wimmer, Dembele, Sissoko, Nkoudou, Janssen.

ARSENAL:Cech; Gabriel [Bellerín 75'], Koscielny, Monreal; Oxlade-Chamberlain, Ramsey, Xhaka [Welbeck 65'], Gibbs; Ozil, Sanchez; Giroud [Walcott 81']

Akiba: Ospina, Bellerin, Coquelin, Holding, Iwobi, Walcott, Welbeck.

REFA: Michael Oliver

EPL, LIGI KUU ENGLAND

Ratiba:

Jumatatu Mei 1

2200 Watford v Liverpool            

Ijumaa Mei 5

2200 West Ham United V Tottenham Hotspur

Jumamosi Mei 6

1430 Manchester City V Crystal Palace

1700 Bournemouth V Stoke City

1700 Burnley V West Bromwich Albion

1700 Hull City V Sunderland

1700 Leicester City V Watford

1930 Swansea City V Everton

Jumapili Mei 7

1530 Liverpool V Southampton

1800 Arsenal V Manchester United

Jumatatu Mei 8

2200 Chelsea V Middlesbrough

LEO DABI LONDON KASKAZINI SPURS v ARSENAL!

EPL, LIGI KUU ENGLAND

Ratiba:

Jumapili Aprili 30

1400 Manchester United v Swansea City         

1605 Everton v Chelsea              

1605 Middlesbrough v Manchester City           

1830 Tottenham Hotspur v Arsenal       

=============================

DABI-SPURS-GANAZLEO WHITE HART LANE Jijini London ipo Dabi ya Timu za Eneo la Kaskazini wakati Tottenham Hotspur itakapoikaribisha Arsenal kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England.
Wakati Spurs wako Nafasi ya Pili Pointi 4 nyuma ya Vinara Chelsea huku wakiwa wamebakiza Mechi 5 na kuwepo matumaini ya kupata Ubingwa, Arsenal wapo Nafasi ya 6 wakipigania tu kumaliza 4 Bora ili Msimu ujao wacheze UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Arsenal wapo Pointi 5 nyuma ya Timu ya 4 Man City lakini wana Mechi 1 mkononi.
Arsene Wenger, Meneja wa Arsenal, ametaka Kikosi chake kishuke White Hart Lane kikipigana ili kuhakikisha ushindi.
Chini ya Wenger, Arsenal imecheza Dabi hii na Spurs mara 49 na kushinda 22, Sare 20 na Kufungwa 7.
Lakini hivi sasa Tottenham hawajafungwa katika Mechi 5 za Ligi zilizopita zote zikiwa chini ya Meneja Mauricio Pochettino.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
TOTTENHAM HOTSPUR: Hugo Lloris, Jan Vertonghen, Toby Alderweireld, Eric Dier, Danny Rose, Mousa Dembele, Victor Wanyama, Kyle Walker, Dele Alli, Christian Eriksen, Harry Kane
ARSENAL: Petr Cech, Gabriel Paulista, Laurent Koscielny, Rob Holding, Alex Oxlade-Chamberlain, Aaron Ramsey, Granit Xhaka, Nacho Monreal, Alexis Sanchez, Mesut Ozil, Danny Welbeck
REFA: Michael Oliver

EPL, LIGI KUU ENGLAND

Ratiba:

Jumatatu Mei 1

2200 Watford v Liverpool       

SPURS KUTOUZA STAA YEYOTE, SANCHEZ KUTOUZWA KWA MPINZANI ENGLAND!

PATA ZILIZOBAMBA ENGLAND:
SPURS KUBAKISHA MASTAA WAKE
DELE-ALLITottenham itahakikisha Mastaa wao wote wanabakia Klabuni hapo na kuwauza tu wale ambao hawawahitaji kwa mujibu wa Meneja wao Mauricio Pochettino.
Spurs, ambao wako Nafasi ya Pili kwenye EPL, Ligi Kuu England, wanasakamwa na Klabu nyingine zinazowawinda Mastaa wao wakubwa wanaofanya vizuri Msimu huu.
Lakini Pochettino ambae amedai Mwenyekiti wa Klabu Daniel Levy wana uhusiano mzuri amesema Mkuu huyo amemhakikishia hawatauza Staa wao yeyote kwa sababu hawana shida na Fedha.
Pochettino amesisitiza: "Wachezaji tunaotaka wabaki watabaki!"
Miongoni mwa wanaosakwa na Klabu pinzani huko England ni Mabeki Kyle Walker na Danny Rose, Viungo Christian Eriksen na Dele Alli na Fowadi Harry Kane.
SANCHEZ HAUZWI KWA MPINZANI ENGLAND!
FOWADI hatari wa Arsenal Alexis Sanchez hatauzwa kwa Mpinzani yeyote wa Arsenal huko England kwa mujibu wa Meneja wa Klabu hiyo Arsene Wenger.
Sanchez, Mchezaji wa Kimataifa kutoka Chile ambae Majuzi Jumapili aliifungia Arsenal Bao la ushindi walipowafunga Man City na kutinga Fainali ya FA CUP, amebakiza Mwaka mmoja tu kwenye Mkataba wake wa sasa huku akigomea kusaini Mkataba mpya.
Wenger ameeleza: "Sidhani kama unaweza kumuuza kwa Klabu nyingine ya Ligi Kuu England, huo ndio ukweli! Lakini kama nlivyosema nadhani atabaki na kusaini Mkataba!"
Ingawa yeye binafsi hajathibitisha kubaki Arsenal kwa Msimu ujao huku Mkataba wake ukiisha Juni, Wenger amesisitiza anashughulikia ununuaji Wachezaji wapya kwa ajili ya Msimu ujao.
Ameeleza: "Nipo kazini hadi Siku ya mwisho ya Msimu nkishughulikia ya sasa na baadae. Ununuzi wa Wachezaji wapya hatima ya Klabu na ni muhimu. Hatima yangu si muhimu, ya Klabu ndio muhimu!"

N'GOLO KANTE AZOA TUZO YA PFA, NDIE BORA ENGLAND!

>>DELE ALLI BORA KWA VIJANA MSIMU WA PILI MFULULIZO!
KANTE-TWITTERKIUNGO wa Chelsea N'Golo Kante amezoa Tuzo ya Mchezaji Bora kwa Msimu wa 2016/17 inayotolewa na PFA ( Professional Footballers Association), Chama cha Wachezaji Soka wa Kulipwa huko England.
Kiungo huyo wa Chelsea wa Miaka 26 anaetoka France aliwabwaga Eden Hazard, Harry Kane, Romelu Lukaku, Zlatan Ibrahimovic na Alexis Sanchez katika Kura iliyopigwa na Wachezaji wenzake wa Kulipwa.
Kwenye Tuzo ya Mchezaji Kijana Dele Alli wa Tottenham Hotspur ameizoa tena kwa Msimu wa Pili mfululizo.
Akiongelea ushindi wa Tuzo hii, Kante alisema: "Ni heshima kubwa mno kuchaguliwa na Wachezaji wengine!"

×××××××××

MJUE KANTE:

KUZALIWA: Paris, France

UMRI: Miaka 26

KLABU ALIZOCHEZA: Boulogne (2011-13), Caen (2013-15), Leicester (2015-16), Chelsea (2016-)

MATAJI: EPL 2015/16

×××××××××

Hivi sasa Kante yuko mbioni kutwaa Ubingwa wa England akiwa na Chelsea ambao ndio Vinara wa EPL, Ligi Kuu England, baada ya Msimu uliopita kutwaa Ubingwa huo akiwa na Leicester City.Kante anaweza kuweka Rekodi ya kuwa Mchezaji wa Kwanza kutwaa Ubingwa wa England Misimu Miwili mfululizo akiwa na Klabu Mbili tofauti ikiwa Chelsea itafanya vyema Mechi zake 6 zilizobaki.