ATHIBITISHWA, SOUTHGATE NI MENEJA MPYA ENGLAND!

ENGLAND-SOUTHGATEFA, The Football Association, Chama cha Soka England, kimetangaza Gareth Southgate ndie Meneja Mpya wa Timu ya Taifa ya England.

Southgate, mwenye Miaka 46, amesaini Mkataba wa Miaka Minne.

Southgate aliteuliwa kuwa Meneja wa Muda wa England Mwezi Septemba baada ya kuondoka kwa Sam Allardyce na kusimamia Mechi 4 ambazo walishinda 2 na Sare 2.

Akiongea baada ya kuthibitishwa hii Leo, Southgate alisema: “Nasikia fahari kubwa kuwa Meneja wa England. Najua kupata kazi ni jambo moja na kuwa na mafanikio ni kitu kingine kabisa!”

Mkataba wa Southgate na FA haukuwekwa wazi lakini inaaminika atavuna Pauni Milioni 2 kwa Mwaka ikiwa ni mara 4 ya Mshahara aliokuwa akilipwa wakati akiwa Bosi wa Timu ya Taifa ya England ya Vijana chini ya Miaka 21, U-21.

Southgate hana uzoefu mkubwa kama Meneja baada ya kuiongoza Middlesbrough na hiyo U-21 tu na anakuwa Meneja wa kwanza Mwingereza wa Timu ya Taifa ya England tangu Kevin Keegan ajiuzulu Mwaka 2000.

Mechi zinazofuata kwa England ni Mwezi Machi Ugenini na Mabingwa wa Dunia Germany ikiwa ni Mechi ya Kirafiki na kufuatia na ile ya Uwanjani Wembley na Lithuania ikiwa ni ya Kundi lao kusaka kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia la Mwaka 2018n huko Russia.

 

 

 

KLABU YA BRAZIL YAANGUKA NA NDEGE HUKO COLOMBIA!

CHAPECOENSENDEGE iliyobeba Watu 81 wakiwemo Kikosi cha moja ya Timu kubwa Nchini Brazil imeanguka wakati ikikaribia Mji wa Medelin huko Nchini Colombia.
Ripoti toka huko zimedai Ndege hiyo ilipata hitilafu za kiufundi kwenye mfumo wake wa umeme na kuanguka eneo la Milimani.
Zipo ripoti zinazodai Watu 6 wamenusurika na ni pamoja na Wachezaji Wawili wa Klabu hiyo ya Brazil iitwayo Chapecoense iliyokuwa ikienda kucheza Fainali ya Copa Sudamericana dhidi ya Timu ya Mji wa Medellin, Atletico Nacional.
Mechi hiyo ya kwanza ya Fainali hiyo ya Mashindano ya Pili kwa ukubwa kwa Klabu huko Marekani ya Kusini ilikuwa ichezwe Jumatano.
Copa Sudamericana ni Mashindano ya Pili kwa ukubwa kwa Klabu huko Marekani ya Kusini na makubwa kabisa huitwa Copa Libertadores.
Shirikisho la Soka huko Marekani ya Kusini CONMEBOL limesema limesimamisha shughuli zote za Soka.
Wacheza hao Wawili wanaoripotiwa kunusurika wametajwa kuwa ni Alan Ruschel na Danilo.
Chapecoense, iliyoanzishwa Mwaka 1973 na kupanda hadi Daraja la juu la Ligi huko Brazil  Mwaka 2014, inatoka Mji wa Kusini mwa Brazil Chapeco na ilifika Fainali ya Copa Sudamericana baada ya Wiki iliyopita kuibwaga Klabu ya Argentina San Lorenzo.
Ndege hiyo iliyoanguka imesemwa ni aina ya  British Aerospace 146 na ilibeba Abiria 72 na Wafanyakazi 9 ikiwa ni ya Kampuni ya Ndege za Kukodi za Nchi ya Bolivia, Lamia.

ZAHA ‘KUIHAMA’ ENGLAND KWENDA IVORY COAST!

ZAHAWINGA wa Crystal Palace Wilfried Zaha ametuma Maombi FIFA ili akubaliwe kuikana England na kuichezea Timu ya Taifa ya Ivory Coast.

Zaha, mwenye Miaka 24, ni Mzaliwa wa Abidjan huko Ivory Coast aliekulia England na tayari ameichezea Timu ya Taifa ya England mara 2 lakini kwa sababu Mechi hizo ni za Kirafiki FIFA inaweza kubariki ‘Uhamisho’ wake.

Shirikisho la Soka la Ivory Coast limethibitisha kupeleka Barua yao kwa FIFA kumuombea Zaha abarikiwe kuichezea Nchi yao.

Ikiwa FIFA itakubali Maombi hayo, Zaha anaweza kucheza Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2017, linaloanza huko Gabon Januari 14 na hilo kuwa pigo kwa Klabu yake Crystal Palace kwani atakosekana kwa Wiki 6 kwa Klabu hiyo inayosuasua kwenye EPL, Ligi Kuu England.

Meneja wa Palace, Alan Pardew, amesikitishwa na hatua hii ya Zaha na amedai Mchezaji huyo ameburuzwa na Wakala wake au Watu wanaomzunguka ingawa amekiri pengine kutoitwa kuichezea England nako kumechangia.

Zaha, ambae alijiunga kwa kudumu na Palace akitokea Manchester United Februari 2015, aliichezea England U-21 mara 13.

FIFA LISTI YA UBORA DUNIANI: ARGENTINA BADO NAMBARI WANI LAKINI BRAZIL YAINYEMELEA, TANZANIA YAPOROMOKA NAFASI 16, NI YA …!

FIFA-RANKINGSINGAWA Argentina bado ndio Timu Bora Duniani kwa mujibu wa Listi ya FIFA ya Ubora Duniani iliyotolewa Leo, Brazil, chini ya Kocha wao mpya, inakuja moto na kuinyemelea kwa kasi.
Kwenye Mechi za Kanda ya Marekani ya Kusini chini ya Mwamvuli wa CONMEBOL, Brazil inaongoza Nchi 10 katika kuwania kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia baada ya kushinda Mechi 5 mfululizo chini ya Kocha Tite huku Argentina ikisuasua na kuporomoka hadi Nafasi ya 5 kwenye Kanda hiyo.
Hilo limeifanya Brazil ipande Nafasi 1 kwenye Listi ya FIFA ya Ubora Duniani na kushika Nafasi ya Pili nyuma ya Argentina huku Mabingwa wa Dunia Germany wakishuka hadi Nafasi ya 3.
England wao wamezidi kushuka, safari hii Nafasi 1, na sasa ni wa 13.
Kwa Afrika Nchi ya Juu kabisa ni Senegal ambayo ipo Nafasi ya 33 wakifuata Mabingwa wa Afrika Ivory Coast ambao ni wa 34 baada kushuka Nafasi 3 lakini wanafungana na Tunisia kwenye Nafasi hiyo na wa 36 ni Egypt.
Tanzania ni ya 160 baada ya kuporomoka Nafasi 16 toka Mwezi uliopita walipokuwa Nafasi ya 144.
Listi nyingine ya FIFA ya Ubora Duniani itatolewa Desemba 22.
10 BORA:
1        Argentina                                   
2        Brazil [Imepanda Nafasi 1]
3        Germany [Imeshuka 1]     
4        Chile [Imepanda 2]
5        Belgium [Imeshuka 1]
6        Colombia [Imeshuka 1]
7        France                   
8        Portugal                 
9        Uruguay                 
10      Spain

FIFA YATANGAZA WAGOMBEA 10 GOLI BORA LA MWAKA!

FIFA-BESTHII Leo FIFA imetangaza Magoli 10 Bora kwa Mwaka 2016 ambayo yatapigiwa Kura ili kupata Goli Bora la Mwaka litakaloshinda Tuzo ya Puskas.

Wagombea hawa 10 sasa wanajumuika pia na Wagombea 23 wa Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani kwa Mwaka 2016 pamoja na Wagombea wengine wa Tuzo mbalimbali zikiwemo za Kocha Bora kwa Waume na Wake na Mchezaji Bora kwa Wanawake.

Magoli hayo 10 yanaweza kuangaliwa kwenye Mitandao ya FIFA FIFA.com/the-best na ule wa FIFA kwenye YouTube.

Magoli haya ni yale yaliyofungwa kuanzia Septemba 2015 hadi Septemba 2016.

Mashabiki wanaweza kupigia Kura Goli wanaloona ni Bora kati ya hayo 10 hadi Desemba 2 na baada ya hapo Magoli 3 Bora yataenda Fainali na Kura kwa Mashabiki zitaanza upya na kuendelea hadi Januari 9 na Mshindi kutangazwa huko Zurich hapo Januari 9, 2017 kwenye Hafla maalum ya kutoa Tuzo za FIFA za Ubora wa Mwaka.

Tuzo ya FIFA ya Puskas ilibuniwa Mwaka 2009 kumuenzi Ferenc Puskás, Nahodha na Staa wa Timu ya Taifa ya Hungary ya Miaka ya 1950.

MAGOLI 10 BORA YA MWAKA:

-Mario Gaspar (Spain) - 13.11.2015, Spain v. England, Kirafiki

-lompho Kekana (South Africa) - 26.03.2016, Cameroon v. South Africa, AFCON

-Marlone (Brazil) - 21.04.2016, Corinthians v. Cobresal, Copa Libertadores

-Lionel Messi (Argentina) - 21.06.2016, USA v. Argentina, Copa América

-Neymar (Brazil) - 08.11.2015, Barcelona v. Villarreal, La Liga (Spain)

-Saúl Ñíguez (Spain) - 27.04.2016, Atlético Madrid v. Bayern Munich, UCL

-Hal Robson-Kanu (Wales) - 01.07.2016, Wales v. Belgium, UEFA EURO 2016

-Daniuska Rodríguez (Venezuela) - 14.03.2016, Venezuela v. Colombia, South American U-17 Women’s Football Championship

-Simon Skrabb (Finland) - 31.10.2015, Gefle v. Åtvidaberg, Ligi Allsvenskan, Sweden

-Mohd Faiz Subri (Malaysia) - 16.02.2016, Penang v. Pahang, Malaysia Super League​

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

HABARI ZA AWALI:

FIFA MCHEZAJI BORA DUNIANI 2016: WAGOMBEA 23 WATAJWA, RONALDO, MESSI, IBRA, AGUERO, OZIL, ALEXIS..NDANI YA NYUMBA!

Friday, 04 November 2016 17:49

http://www.sokaintanzania.com/za-duniani/3341-fifa-mchezaji-bora-duniani-2016-wagombea-23-watajwa-ronaldo-messi-ibra-aguero-ozil-alexis-ndani-ya-nyumba

FIFALeo imetangaza Majina ya Wachezaji 23 Wagombea wa Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani kwa Mwaka 2016 na mbali ya wale wa kawaida, Cristiano Ronaldo na Lionel , pia wamoi Wachezaji 10 toka EPL, Ligi Kuu England, na Watatu kati yao wanatoka kwa Mabingwa wa England Leicester City.

Watatu hao ni Jamie Vardy, Riyad Mahrez na N'Golo Kante.

Wengine toka EPL ni Sergio Aguero, Kevin de Bruyne (Manchester City), Alexis Sanchez, Mesut Ozil (Arsenal), Paul Pogba, Zlatan Ibrahimovic (Manchester United) and Dimitri Payet (West Ham).

Listi hii ya Wagombea 23 itapungua na kubakizwa Wagombea Watatu watakaotangazwa Desemba 3.

Mshindi wa Tuzo hii atatajwa Januari 9 huko Zurich, Uswisi kwenye Hafla maalum.

Jana na Juzi FIFA ilitoa Majina ya Wagombea wa Tuzo za Ubora kwa Wanawake na pia Makocha Bora kwa Kinamama na Kinababa.

++++++++++++++++++++++++++

KURA KUPATA WASHINDI:

-Washindi wa Tuzo hizi watapatikana kwa Kura:

-Asilimia 50 ni ile ya Makepteni na Makocha wa Timu za Taifa za Nchi Wanachama FIFA

-Asilimia 25 ya Kura itatoka kwa Kura za Mtandaoni za Mashabiki

-Asilimia 25 ni Kura za Wawakilishi 200 wa Wanahabari kutoka Mabara yote 6 Duniani.

++++++++++++++++++++++++++

WAGOMBEA 30 - Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani 2016:

Sergio Aguero (Manchester City), Gareth Bale (Real Madrid), Gianluigi Buffon (Juventus), Cristiano Ronaldo (Real Madrid), Kevin De Bruyne (Manchester City), Antoine Griezmann (Atletico Madrid), Zlatan Ibrahimovic (Manchester United), Andres Iniesta (Barcelona), N'Golo Kante (Chelsea), Toni Kroos (Real Madrid), Robert Lewandowski (Bayern Munich), Riyad Mahrez (Leicester City), Lionel Messi (Barcelona), Luka Modric (Real Madrid), Manuel Neuer (Bayern Munich), Neymar (Barcelona), Mesut Ozil (Arsenal), Dimitri Payet (West Ham), Paul Pogba (Manchester United), Sergio Ramos (Real Madrid), Alexis Sanchez (Arsenal), Luis Suarez (Barcelona), Jamie Vardy (Leicester City).

WACHEZAJI –  WANAWAKE, Wagombea 10:

Camille Abily: Kiungo; 31; France and Lyon

Melanie Behringer: Kiungo; 30; Germany and Bayern Munich

Sara Dabritz; Kiungo, 21; Germany and Bayern Munich

Amandine Henry; Kiungo; 27; France and Portland Thorns

Saki Kumagai: Beki; 26; Japan and Lyon

Carli Lloyd; Kiungo; 34; USA and Houston Dash

Dzsenifer Marozsan; Kiungo; 24; Germany and Lyon

Marta; Fowadi; 34; Brazil and FC Rosengard

Lotta Schelin; Fowadi, 32, Sweden and FC Rosengard

Christine Sinclair; Fowadi; 33; Canada and Portland Thorns

MAKOCHA –  WANAUME, Wagombea 10:

* Chris Coleman (Wales/Welsh national team)

* Didier Deschamps (France/French national team)

* Pep Guardiola (Spain/FC Bayern Munich/Manchester City)

* Jürgen Klopp (Germany/Liverpool)

* Luis Enrique (Spain/FC Barcelona)

* Mauricio Pochettino (Argentina/Tottenham Hotspur)

* Claudio Ranieri (Italy/Leicester City)

* Fernando Santos (Portugal/Portuguese national team)

* Diego Simeone (Argentina/Atlético Madrid)

* Zinédine Zidane (France/Real Madrid).

MAKOCHA –  WANAWAKE, Wagombea 10:

* Philippe Bergeroo (France/French national team)

* Jill Ellis (USA/US national team)

* John Herdman (England/Canadian national team)

* Silvia Neid (Germany/German national team)

* Vera Pauw (Netherlands/South African national team)

* Gérard Prêcheur (France/Olympique Lyonnais)

* Pia Sundhage (Sweden/Swedish national team)

* Oswaldo Vadão (Brazil/Brazilian national team)

* Martina Voss-Tecklenburg (Germany/Swiss national team)

* Thomas Wörle (Germany/FC Bayern Munich).

FIFA – Tuzo za Ubora zitakazotolewa:

-Mchezaji Bora Duniani 2016 [The Best Fifa Men's Player 2016]

-Mchezaji Bora Duniani 2016 kwa Kinamama [The Best Fifa Women's Player 2016]

-Kocha Bora kwa Wanaume 2016 [The Best Fifa Men's Coach 2016]

-Kocha Bora kwa Wanawake 2016 [The Best Fifa Women's Coach 2016]

-Tuzo ya Puskas 2016 kwa Goli Bora [The Fifa Puskas Award 2016 for goal of the year]

-Tuzo ya Uchezaji wa Haki 2016 [The Fifa Fair Play Award 2016]

-Tuzo ya Mashabiki 2016 [The Fifa Fan Award]