ALEXIS SANCHEZ AKIRI UDANGANYIFU KODI SPAIN, FAINI, PENGINE LUPANGO VYAMNGOJA!!

SANCHEZ-SEP26FOWADI wa Arsenal Alexis Sanchez amekiri kwa Mamlaka ya Kodi huko Spain wa kukwepa Kodi ya €983 443 wakati akiichezea Barcelona.
Sanchez, Mchezaji wa Kimataifa wa Chile mwenye Miaka 28, sasa anakabiliwa na kupigwa Faini na pengine Kifungo ambacho kinaweza kuwa cha nje.
Akitoa ushahidi wake kwa Video akiwa Jijini London, England, Sanchez alikubali 'kosa katika stahili ya Malipo ya Kodi yake' ambayo sasa amelipa yote.
Sanchez amekiri kuwa hesabu za Kodi yake za Miaka ya 2012 na 2013 hazikujumuisha Faida iliyotokana na Umiliki wake wa Picha na Matangazo yake ambayo yalilipwa kupitia Kampuni yake iliyokuwa huko Malta.
Pia Sanchez alikiri kumiliki Kampuni hiyo Numidia Trading Limited ambayo hakuibanisha kwenye Malipo ya Kodi zake huko Spain.
Kesi hii inafanana na ile ya Mchezaji wa Barcelona Javier Mascherano ambae Januari 2016 alipigwa Faini €815 000 na Kifungo cha Mwaka Mmoja alichotumikia nje ya Gereza kwa udanganyifu wa Malipo ya Kodi huko Spain.
Wengine waliokumbwa na kadhia kama hiyo ni Staa wa Barcelona na Argentina Lionel Messi na Baba yake Mzazi kutwangwa Faini ya Euro Milioni 2 hapo Julai 2016 na pia kuhukumiwa kufungwa Jela Miezi 21 Kifungo ambacho kilifanywa kiwe cha nje badala ya Gerezani.
Huko Spain Vifungo vya chini ya Miaka Miwili hutumikiwa nje ya Gereza.

PAYET AGOMA KUCHEZEA WEST HAM, ATAKA KUHAMA JANUARI HII!

WESTHAM-PAYETMFARANSA Dimitri Payet ameiambia Klabu yake West Ham kwamba anataka kuondoka Januari hii kwa mujibu wa habari alizotoboa Meneja wa Klabu hiyo Slaven Bilic.

Akiongea na Wanahabari hii Leo kuelekea Mechi yao ya EPL, Ligi Kuu England, Jumamosi na Crystal Palace, Bilic amesema Mchezaji huyo amegoma kucheza Mechi hiyo ya Jumamosi.

Lakini Bilic amesisitiza licha ya Mchezaji huyo alienunuliwa na West Ham Mwaka 2015 kutoka Marseille kwa Pauni Milioni 10 kukataa kucheza, Klabu yao haina nia kumuuza.

Bilic amepasua kuwa Payet, mwenye Miaka 29, amesimamishwa kujiunga na Mazoezi ya Timu hadi sakata lake liishe.

Bilic amesema: “Hatumuuzi. Tumempa kila kitu lakini ametuangusha. Nimekasirika sana!”

Zipo ripoti kuwa Mchezaji huyo, ambae Februari Mwaka Jana alipewa Mkataba Mpya wa Miaka 5 na Nusu, anatakiwa huko kwao France huku Klabu za Marseille na Paris Saint-Germain zikitajwa sana.

Bilic mwenyewe amekiri kuwa anajua Payet amesharubuniwa na Klabu nyingine lakini yeye hajakata tamaa kubaki kwa Mchezaji huyo hapo West Ham.

Bilic amesema: “Natarajia atarudi na kuonyesha ari kwa Timu kama vile Timu ilivyomwonyesha yeye. Nimeongea na Klabu, Mwenyekiti na Makamu wake. Si suala la Fedha. Tunataka abaki!”

HAKUNA UBISHI, MCHEZAJI BORA DUNIANI NI CRISTIANO RONALDO PEKEE!

>>RONALDO AZOA TUZO YA FIFA, KOCHA BORA DUNIANI CLAUDIO RANIERI!

FIFA-BEST-RONALDOHAFLA ya FIFA ya kutunuku Tuzo za FIFA za Ubora Duniani kwa Mwaka 2016 zimefanyika Usiku huu huko Zurich, Uswisi na Cristiano Ronaldo kuibuka ndio Mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani.

Akitwaa Tuzo hii, Ronaldo, anaechezea Real Madrid na Nchi yake Portugal, aliwashinda kwa Kura Lionel Messi na Antoine Griezmann.

Ronaldo pia alitwaa, mapema Mwezi Desemba, Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani kwa 2016, Ballon d’Or, inayotolewa na Jarida la France, France Football, Tuzo ambayo kabla ya hapo, kwa Miaka 6, iliunganishwa na FIFA na kuitwa FIFA Ballon d’Or, lakini kuanzia safari hii wametengana.

Kwa upande wa Kinamama, Mchezaji Bora ni Carli Lloyd wa USA.

Kocha Bora Duniani kwa Wanaume ni Claudio Ranieri baada ya kuiwezesha Leicester City, bila kutegemewa, kutwaa Ubingwa wa England kwa mara ya kwanza katika Historia yao.

Nae Mohd Faiz Subri wa Penang, Malaysia ndie alitwaa Tuzo ya Puskas ya Goli Bora la Mwaka.

Kwenye Tuzo ya Mashabiki, Mashabiki wa Timu za Liverpool na Borussia Dortmund, kwa pamoja, wameshinda Tuzo hii kwa tukio la kuimba wote ‘Wimbo wa Taifa wa Liverpool’ -'You'll Never Walk Alone'- Uwanjani Anfield kabla ya Mechi yao ya Robo Fainali ya UEFA EUROPA LIGI Msimu uliopita.

FIFA-BEST-RANIERI

FIFA TUZO ZA UBORA – WAGOMBEA NA MSHINDI:

MCHEZAJI BORA WANAUME:

-Wagombea: Cristiano Ronaldo, Antoine Griezmann, Lionel Messi

-Mshindi: Cristiano Ronaldo

MCHEZAJI BORA WANAWAKE:

-Wagombea: Melanie Behringer, Carli Lloyd, Marta

-Mshindi: Carli Lloyd wa USA.

KOCHA BORA WANAUME:

-Wagombea: Claudio Ranieri, Fernando Santos, Zinedine Zidane

-Mshindi: Claudio Ranieri wa Mabingwa wa England Leicester City

KOCHA BORA WANAWAKE:

-Wagombea: Jill Ellis, Silvia Neid, Pia Sundhage

-Mshindi: Silvia Neid [Germany]

GOLI BORA [Tuzo ya Puskas]:

-Wagombea: Marlone, Daniuska Rodriguez, Mohd Faiz Subri

-Mshindi: Mohd Faiz Subri wa Penang, Malaysia.

**Tuzo hii inatokana na Kura za Mashabiki Duniani kote.

TUZO TOKA KWA MASHABIKI:

-Wagombea: Mashabiki wa Den Haag, Borussia Dortmund & Liverpool na Iceland.

-Mshindi: Mashabiki wa Borussia Dortmund & Liverpool

TUZO YA UCHEZAJI WA HAKI

-Mshindi: Atletico Nacional ya Colombia

FIFA FIFPro World11 2016 – Kikosi Bora cha Mwaka 2016:

-Kipa: Neur

-Mabeki: Alves, Pique, Ramos, Marcelo

-Viungo: Modric, Kroos, Iniesta

-Mafowadi: Suarez, Ronaldo, Messi

++++++++++++++++++++++++++

KURA KUPATA WASHINDI:

-Washindi wa Tuzo hizi watapatikana kwa Kura:

-Asilimia 50 ni ile ya Makepteni na Makocha wa Timu za Taifa za Nchi Wanachama FIFA

-Asilimia 25 ya Kura itatoka kwa Kura za Mtandaoni za Mashabiki

-Asilimia 25 ni Kura za Wawakilishi 200 wa Wanahabari kutoka Mabara yote 6 Duniani.

 

FIFA MCHEZAJI BORA DUNIANI: LEO RONALDO KUZOA TUZO, KUWAANGUSHA MESSI, GRIEZMANN?

FIFA-BESTCRISTIANO RONALDO, Mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani Ballon d'Or kwa Mwaka 2016 aliyopewa Mwezi uliopita Leo anapewa nafasi kubwa kuzoa Tuzo kama hiyo inayotolewa na FIFA.
Leo huko Zurich, Uswisi, FIFA wanaendesha Hafla ya Tuzo za Ubora kwa Mwaka 2016.
Kabla Mwaka 2016, FIFA walishirikiana na Jarida la France Football kutoa Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani iliyoitwa FIFA Ballon d'Or lakini kuanzia Tuzo za 2016 washirika hao wametengana na kila Mtu kuenda kivyake.
Mwezi uliopita Ronaldo, Mchezaji wa Real Madrid kutoka Portugal, alimbwaga Lionel Messi, Mchezaji wa Barcelona kutoka Argentona, na kutwaa Ballon d'Or kwa mara ya 4 huku akiwa ameitwaa mara 5.
 Safari hii Wawili hao watachuana na Antoine Griezmann kutoka Atletico Madrid na France kugombea FIFA Tuzo ya Mchezaji Bora kwa Mwaka 2016.
Sambamba na Tuzo hiyo pia Tuzo kadhaa zikigombewa ikiwemo.ile ya Kocha Bora Duniani kwa Mwaka 2016 na Wagombea wake ni Claudio Ranieri, alieiongoza Leicester City kutwaa Ubingwa wa EPL, Ligi Kuu England, Fernando Santos wa Portugal kwa kuiongoza Nchi hiyo kutwaa EURO 2016 na Zinedine Zidane, alieipa Real Madrid UEFA Championz Ligi.
Tuzo nyingine ni za Kinamama Mchezaji Bora Duniani, Tuzo ya Puskas kwa Goli Bora na Timu Bora ya Mwaka.
++++++++++++++++++++++++++
KURA
KUPATA WASHINDI:
-Washindi
wa Tuzo hizi watapatikana kwa Kura:
-Asilimia
50 ni ile ya Makepteni na Makocha wa Timu za Taifa za Nchi Wanachama FIFA
-Asilimia
25 ya Kura itatoka kwa Kura za Mtandaoni za Mashabiki
-Asilimia
25 ni Kura za Wawakilishi 200 wa Wanahabari kutoka Mabara yote 6 Duniani.
++++++++++++++++++++++++++
Wagombea Watatu wa Goli Bora la Mwaka ni Marlone (Brazil/Corinthians), Daniuska Rodriguez (Venezuela/Venezuela Timu ya
Taifa ya Wanawake U-17) na Mohd Faiz Subri (Malaysia/Penang). 
Kwa apande wa Kinamama Wagombea ni Jill Ellis (USA/Timu ya Taifa ya USA), Silvia Neid (Germany/Timu ya Taifa ya Germany) na Pia Sundhage (Sweden/Timu ya Taifa ya Sweden).
FIFPro World11 2016
LISTI
YA WACHEZAJI 55 WAGOMBEA WA KIKOSI BORA:
GoalkeepersMAKIPA
(5): Claudio Bravo (Chile/FC Barcelona/Manchester City), Gianluigi Buffon
(Italy/Juventus), David de Gea (Spain/Manchester United), Keylor Navas (Costa
Rica/Real Madrid) na Manuel Neuer (Germany/FC Bayern Munich).
MABEKI
(20): David Alaba (Austria/FC Bayern Munich), Jordi Alba (Spain/FC Barcelona),
Serge Aurier (Côte d’Ivoire/Paris Saint-Germain), Héctor Bellerìn
(Spain/Arsenal), Jérôme Boateng (Germany/FC Bayern Munich), Leonardo Bonucci
(Italy/Juventus), Daniel Carvajal (Spain/Real Madrid), Giorgio Chiellini
(Italy/Juventus), Dani Alves (Brazil/FC Barcelona/Juventus), David Luiz
(Brazil/Paris Saint-Germain/Chelsea), Diego Godín (Uruguay/Atlético Madrid),
Mats Hummels (Germany/Borussia Dortmund/FC Bayern Munich), Philipp Lahm
(Germany/FC Bayern Munich), Marcelo (Brazil/Real Madrid), Javier Mascherano
(Argentina/FC Barcelona), Pepe (Portugal/Real Madrid), Gerard Piqué (Spain/FC Barcelona),
Sergio Ramos (Spain/Real Madrid), Thiago Silva (Brazil/Paris Saint-Germain) na
Raphaël Varane (France/Real Madrid).
VIUNGO
(15): Xabi Alonso (Spain/FC Bayern Munich), Sergio Busquets (Spain/FC
Barcelona), Kevin De Bruyne (Belgium/Manchester City), Eden Hazard
(Belgium/Chelsea), Andrés Iniesta (Spain/FC Barcelona), N’Golo Kanté
(France/Leicester City/Chelsea) Toni Kroos (Germany/Real Madrid), Luka Modrić
(Croatia/Real Madrid), Mesut Özil (Germany/Arsenal), Dimitri Payet (France/West
Ham United), Paul Pogba (France/Juventus/Manchester United), Ivan Rakitić
(Croatia/FC Barcelona), David Silva (Spain/Manchester City), Marco Verratti (Italy/Paris
Saint-Germain) na Arturo Vidal (Chile/FC Bayern Munich).MASTRAIKA
(15): Sergio Agüero (Argentina/Manchester City), Gareth Bale (Wales/Real
Madrid), Karim Benzema (France/Real Madrid), Cristiano Ronaldo (Portugal/Real
Madrid), Paulo Dybala (Argentina/Juventus), Antoine Griezmann (France/Atlético
Madrid), Gonzalo Higuaín (Argentina/Napoli/Juventus), Zlatan Ibrahimović
(Sweden/Paris Saint-Germain/Manchester United), Robert Lewandowski (Poland/FC
Bayern Munich), Lionel Messi (Argentina/FC Barcelona), Thomas Müller
(Germany/FC Bayern Munich), Neymar (Brazil/FC Barcelona), Alexis Sánchez
(Chile/Arsenal), Luis Suárez (Uruguay/FC Barcelona) na Jamie Vardy
(England/Leicester City). 
 

MWENZAKE MBWANA SAMATTA KUTUA LEICESTER CITY!

LEICESTER-NDIDI-SAMATTA2MABINGWA wa England Leicester City wameshaafiki dili ya kumsaini Wilfred Ndidi kutoka Klbu ya Genk ya Belgium kwa Malipo ya Pauni Milioni 15 yenye nyongeza ya Pauni Milioni 3 juu.

Ndidi, Mnigeria mwenye Miaka 20 ambae ni Kiungo, tayari amefanyiwa awamu ya kwanza ya upimwaji afya ambao unatarajiwa kukamilika kabla Januari 1 ili Uhamisho wake ukamilike.

Hivi sasa Leicester wamemwombea Mchezaji huyo Kibali cha Kazi cha Uingereza na mara baada ya hilo kwisha Mabingwa hao wanatarajiwa kumtangaza rasmi kutua King Power Stadium.

Meneja wa Leicester, Claudio Ranieri, anamchukulia Ndidi kama ni mbadala halisi wa Kiungo kutoka France, N’Golo Kanté, aliehamia Chelsea mwanzoni mwa Msimu.

Msimu wote huu Leicester wameyumba sana kwa kumkosa Kiungo Kante na ujio huu wa Ndidi utawafanya wajinasue toka karibu na mkia wa EPL, Ligi Kuu England, ambako Nafasi ya 16.

Leicester pia wapo Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI ambako watacheza na Sevilla ya Spain.

Ndidi ni Mzaliwa wa Lagos, Nigeria na kipaji chake kuvumbuliwa na Msaka Vipaji wa Manchester United, Roland Janssen, ambae alimwona kwenye Mashindano ya Vijana Mwaka 2013.

Mwaka 2015, Ndidi akajiunga na Genk, Klabu ya Belgium ambayo ni maarufu Tanzania kwa vile Straika na Nahodha wa Nchi hiyo, Mbwana Samatta, anaichezea.

Akiwa na Genk, Ndidi amechezea Mechi 62 za Ligi na kufunga Bao 4.