WHITE HART LANE: AGUERO AICHIMBIA CITY 4 BORA, SPURS YAKATWA MAINI!

LIGI KUU ENGLAND
MATOKEO:
Jumapili Mei 3
Chelsea 1 Crystal Palace 0
Tottenham 0 Man City 1
===========================
BPL-2014-2015-LOGO-POABao la Dakika ya 29 la Sergio Aguero Ugenini huko White Hart Lane limewapa ushindi wa Bao 1-0 waliokuwa Mabingwa wa zamani wa England Manchester City walipocheza na Tottenham na kujihakikishia kuwemo 4 Bora ya Ligi Kuu England.
Kipigo hiki pengine pia kinamaliza matumaini ya Spurs kuwemo 4 Bora ingawa kimahesabu bado wamo kwenye kinyang'anyiro.
 ++++++++++++++++++++++++++++++++++
LIGI KUU ENGLAND
MSIMAMO-Timu za Juu:
1. Chelsea Mechi 35 Pointi 83
2. Man City Mechi 35 Pointi 70
3. Arsenal Mechi 33 Pointi 67
4. Man United Mechi 35 Pointi 65
++++++++++++++++++
5. Liverpool Mechi 35 Pointi 61
6. Tottenham Mechi 35 Pointi 58
7. Southampton Mechi 35 Pointi 57
8. Swansea City Mechi 35 Pointi 53
9. West Ham Mechi 35 Pointi 47
10. Stoke Mechi 35 Pointi 47
11. Everton Mechi 35 Pointi 44
+++++++++++++++++++++++++++++++++
VIKOSI:
Tottenham Hotspur: Lloris; Dier, Fazio, Vertonghen, Rose; Bentaleb, Mason; Lamela, Eriksen, Chadli; Kane.
Akiba: Chiriches, Paulinho, Soldado, Adebayor, Yedlin, Vorm, Stambouli. 
Manchester City: Hart; Zabaleta, Demichelis, Mangala, Kolarov; Fernando, Fernandinho; Milner, Lampard, Silva; Agüero.
Akiba: Sagna, Nasri, Dzeko, Caballero, Bony, Clichy, Boyata.
REFA: Andre Marriner
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA
**Saa za Bongo
Jumatatu Mei 4
2200 Hull v Arsenal
Jumamosi Mei 9
1445 Everton v Sunderland
1700 Aston Villa v West Ham
1700 Hull v Burnley
1700 Leicester v Southampton
1700 Newcastle v West Brom
1700 Stoke v Tottenham
1930 Crystal Palace v Man United
Jumapili Mei 10
1530 Man City v QPR
1800 Chelsea v Liverpool
Jumatatu Mei 11
2200 Arsenal v Swansea

RIO FERDINAND AFIWA NA MKEWE!

RIOFERDINAND-WIFEMke wa Mchezaji wa zamani wa Manchester United na Nahodha wa England Rio Ferdinand amefariki Dunia kutokana na Ugonjwa wa Kansa.
Rio, mwenye Miaka 36 na ambae sasa anachezea QPR, ametoa taarifa ya Kifo cha Mkewe kilichotokea kwenye Hospitali Jijini London.
Mkewe Rio, Rebecca Ellison, Miaka 34, alipatwa na tatizo la Kansa ya Ziwa.
Rio na Rebecca walioana Mwaka 2009 baada ya kuwa wakiishi pamoja na wana Watoto Watatu.
Klabu ya QPR imetangaza kuwa Kikosi chao Leo kitavaa Vitambaa Vyeusi Mikononi wakati wa Mechi yao ya Ligi Kuu England huko Anfield dhidi ya Liverpool.
Ferdinand alikulia huko Peckham, London ya Kusini Mashariki na aliichezea England mara 81 na pia kuzichezea Klabu za West Ham United na Leeds United.

WASHABIKI LIVERPOOL WATAKA BRENDAN RODGERS AFUKUZWE!

2015-05-01 09.10.16Baada ya Jumanne kupigwa Bao 1-0 na Hull City na kuwaacha Pointi 7 nyuma ya Manchester United walio Nafasi ya 4 kwenye Ligi Kuu England, Washabiki wa Liverpool wameibuka na kutaka Meneja wao Brendan Rodgers afukuzwe.
Liverpool wameshinda Mechi 2 tu kati ya 7 zilizopita na kuwaacha Nafasi ya 5 kwenye Ligi ambayo ni nje ya kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao na pia walitupwa nje kwenye FA CUP baada ya kutolewa na Aston Villa katika Nusu Fainali.
Msimu uliopita Brendan Rodgers nusura awape Liverpool Taji la Ubingwa wa England kwa mara ya kwanza katika Miaka 25 lakini wakateleza Mechi za mwishoni na Manchester City kutwaa Ubingwa na wao kubaki Nafasi ya Pili.
Gazeti moja huko England liliendesha Kura ambayo Watu 4,000 walipiga na Asilimia 65 walitaka Brendan Rodgers afukuzwe.

JOSE MOURINHO AUNGAMA: 'HAKUNA KLABU ITATAWALA LIGI KUU ENGLAND!'

MOURINHO-MIMACHOJose Mourinho anaamini kuwa hamna Klabu yeyote yenye uwezo wa kutawala Ligi Kuu England katika Miaka michache ijayo.
Klabu ya Mourinho, Chelsea, wanakaribia kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England Msimu huu lakini Meneja huyo, licha ya kutarajia Klabu yake kuwemo kwenye mbio za Ubingwa Msimu ujao, ameungama kuwa Klabu nyingine kadhaa zitaleta upinzani mkali.
Mourinho amesema: "Kwa sasa ni ngumu kwa Klabu moja kutawala. Hapa si Germany, ipo Bayern. Hapa si Uswisi, ipo Basle, Na hii si Scotland ikiwepo Celtic."
"Ni ngumu zaidi kwa sasa kupita nyuma. Utazungumzaje kutawala wakati kila Mtu anajua nini kitatokea mwishoni mwa Msimu?"
Mourinho amefafanua: "Arsenal wana Kikosi cha ajabu. Thierry Henry amesema wanahitaji Wachezaji Wanne wa kiwango cha Dunia. Ukiwapa Arsenal hao Wanne nadhani watarudia ile Timu isiyofungwa Msimu mzima."
"Man United wana Kikosi cha ajabu ambacho kina Mchezaji wa Bei ghali katika Historia ya Ligi Kuu England ambae hachezi! [Akimaanisha Angel Di Maria]"
Mourinho amesisitiza kuwa anajua Man United na Man City zitatumia nguvu yao ya Kifedha kuimarisha Vikosi vyao na hilo litampa kazi ngumu.
 
 
 
 
 

HAZARD NDIE MCHEZAJI BORA WA MWAKA WA PFA, HARRY KANE NI BORA KWA VIJANA!

HAZARD-PFA-TUZOEden Hazard wa Chelsea amechaguliwa kuwa ndie Mchezaji Bora wa Mwaka wa PFA, Professional Footballers Association, ambacho ni Chama cha kutetea maslahi ya Wachezaji wa Kulipwa huko England.
Tuzo ya Mchezaji Bora Kijana wa Mwaka wa PFA imekwenda kwa Straika wa Tottenham, Harry Kane mwenye Miaka 21.
Msimu huu, Hazard, mwenye Miaka 24, amefunga Mabao 13 kwa Chelsea na kutengeneza Bao 8 katika Mechi 33 za Ligi Kuu England na kuisaidia Timu yake kuukaribia Ubingwa.
Mshindi wa Tuzo za PFA huchaguliwa kwa Kura za Wachezaji wenzake wa Kulipwa.
Hazard, ambae Msimu uliopita ndie alikuwa Mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora Kijana wa PFA, alikabidhiwa Tuzo yake Jana huko Grosvenor Hotel Jijini London.
Awali Jana, Hazard alichaguliwa mmoja wa Wachezaji 6 wa Chelsea kwenye Kikosi cha PFA, cha Timu Bora ya Mwaka.
Wachezaji wengine wa Chelsea kwenye Kikosi hicho ni Mabeki Branislav Ivanovic, John Terry na Gary Cahill na Viungo Nemanja Matic pamoja na Straika Diego Costa.
Wachezaji wengine waliounda Kikosi hicho cha Wachezaji 11 ni Fulbeki wa Southampton Ryan Bertrand, Straika wa Tottenham Harry Kane, Philippe Coutinho wa Liverpool, Alexis Sanchez wa Arsenal na Golikipa wa Manchester United David De Gea.
LISTI KAMILI YA WAGOMBEA:
-MCHEZAJI BORA WA MWAKA 
Diego Costa (Chelsea)
David De Gea (Manchester United)
Philippe Coutinho (Liverpool)
Eden Hazard (Chelsea)
Harry Kane (Tottenham Hotspur)
Alexis Sanchez (Arsenal)
-MCHEZAJI BORA KIJANA WA MWAKA
Thibaut Courtois (Chelsea)
Philippe Coutinho (Liverpool)
David De Gea (Manchester United)
Eden Hazard (Chelsea)
Harry Kane (Tottenham Hotspur)
Raheem Sterling (Liverpool)