LISTI FIFA/COCA COLA UBORA DUNIANI: ARGENTINA BADO 1, BRAZIL 2, EGYPT JUU AFRIKA, TANZANIA MPOROMOKO TU, NI YA 158!

FIFA-RANKINGSFIFA Leo imetoa Listi mpya ya ubora Duniani kwa nchi Wanachama wake, ambayo huitwa Listi ya FIFA/Coca Cola Ubora Duniani, na Vinara wake bado ni Argentina wakifuatia Brazil na kwa Afrika Egypt ndio wapo juu kabisa huku Tanzania ikishuka Nafasi 2 na kukamata Namba 158.

5 Bora kwenye listi hiyo zimebaki zile zile bila mabadiliko na nazo ni Argentina (1), Brazil (2), Germany (3), Chile (4) na Belgium (5).

Kwa Afrika, Nchi ambayo iko juu kabisa ni Egypt, waliotolewa Fainali ya AFCON 2017, ambao sasa wapo Nafasi ya 23 baada kupanda Nafasi 12 wakifuata Senegal walio Nafasi ya 31 na Mabingwa Wapya wa Afrika ambao ndio waliwafunga Egypt, Cameroun, wapo Nafasi ya 33 baada kupaa Nafasi 29.

Listi nyingine ya FIFA/Coca Cola Ubora Duniani itatolewa itatolewa Tarehe 9 Machi 2017.

FIFA LIST YA UBORA DUNIANI – 20 BORA:

NAFASI

NCHI

NAFASI ILIZOPANDA AU KUSHUKA

1

Argentina

0

2

Brazil

0

3

Germany

0

4

Chile

0

5

Belgium

0

6

France

1

7

Colombia

-1

8

Portugal

0

9

Uruguay

0

10

Spain

0

11

Switzerland

0

12

Wales

0

13

England

0

14

Poland

1

15

Italy

1

16

Croatia

-2

17

Mexico

1

18

Peru

1

19

Costa Rica

-2

20

Iceland

1

SERIE A: JUVE YAIDUNDA INTER KATIKA DERBY D'ITALIA, YAZIDI KUPAA KILELENI!

Derby dItaliaBAO safi la Juan Cuadrado limewapa Vinara wa Serie A Juventus ushindi wa 1-0 dhidi ya Inter Milan na kuwaweka Pointi 6 mbele ya Timu ya Pili Napoli huku wakiwa na Mechi 1 mkononi.

Kipigo hicho cha Inter Milan kwenye Mechi inayobatizwa ‘Derby d'Italia’ kimevunja wimbi laoSERIEA-FEB5 la ushindi wa Mechi 7 mfululizo za Serie A.

Kwa Juve hiyo ilikuwa Mechi yao ya 28 kushinda mfululizo Uwanjani kwao.

Kwenye Mechi nyingine zilizochezwa Jana, Lazio waliitwanga Timu ya Mkiani Pescara Bao 6-2 huku Marco Parolo akipiga Bao 4.

Ushindi huo umewaweka Lazio Nafasi ya 4 wakiwa na Pointi 43, Pointi 4 nyuma ya Timu ya 3 AS Roma.

VIKOSI:

JUVENTUS: Buffon; Lichtsteiner (Dani Alves 80), Bonucci, Chiellini, Alex Sandro; Khedira, Pjanic; Cuadrado (Marchisio 70), Dybala (Rugani 84), Mandzukic; Higuain

INTER MILAN: Handanovic; Murillo, Medel, Miranda; Candreva (Eder 58), Gagliardini, Brozovic (Kondogbia 58), D'Ambrosio; Joao Mario (Palacio 79), Perisic; Icardi

REFA: Rizzoli

SERIE A

Matokeo

Jumapili Februari 5

AC Milan 0 Sampdoria 1

Atalanta 2 Cagliari 0

Chievo Verona 0 Udinese 0

Empoli 1 Torino 1

Pescara 2 Lazio 6

Genoa 0 Sassuolo 1

Palermo 1 Crotone 0

Juventus 1 Inter Milan 0

EVRA AREJEA KWAO FRANCE, KUKIPIGA MECHI YA KWANZA IJUMAA NA KLABU MPYA MARSEILLE!

EVRA-NYUMBANIMCHEZAJI wa zamani wa Manchester United Patrice Evra Ijumaa anatarajiwa kuichezea Timu yake mpya huko kwao France Marseille wakati wakiikaribisha Montpellier kwenye Mechi ya Ligi 1.

Evra, mwenye Miaka 35, ameihama Juventus na kurejea kwao France kujiunga na Marseille ambayo sasa inaimarishwa vilivyo na Mmiliki wake kutoka Marekani, Frank McCourt, ambae ashamsimika Kocha Mpya Rudi Garcia na yupo kwenye harakati kubwa kumsaini Mchezaji wa Kimataifa wa France anaechezea West Ham Dimitri Payet.

Akiongelea kuhusu kuondoka kwa Evra, Kocha wa Juventus Massimiliano Allegri ametamka: “Ni Bingwa mkubwa, Mchezaji wa Kulipwa mwenye kila kitu!”

Hivi sasa Marseille wapo Nafasi ya 7 wakiwa Pointi 15 nyuma ya zile Nafasi za Timu kuichezea UEFA CHAMPIONZ LIGI.

Mbali ya mvuto huo wa Evra, Ligi 1 itavutia zaidi hapo Jumapili wakati Mabingwa Watetezi Paris Saint-Germain wakiwavaa Vinara wa Ligi hiyo kwa sasa AS Monaco.

Baada ya kumnasa Julian Draxler Siku ya Mwaka Mpya, PSG watamkaribisha Straika wa Portugal mwenye Miaka 20 kutoka Benfica Goncalo Guedes.

AS Monaco wanaongoza Ligi 1 wakiwa na Pointi 48 wakifuata Nice wenye Pointi 46 na PSG ni wa 3 wakiwa na Pointi 45.

France -LIGI 1

RATIBA

Ijumaa Januari 27

Marseille v Montpellier

Jumamosi Januari 28

Lyon v Lille

Angers v Metz

Bastia v Caen

Lorient v Dijon

Nancy v Bordeaux

Rennes v Nantes

Jumapili Januari 29

Nice v Guingamp

Toulouse v Saint Etienne

Paris Saint-Germain v Monaco

FAINALI KOMBE LA DUNIA - RUSSIA 2018: DROO KUFANYIKA DESEMBA 1 HUKO KREMLIN!

WC-RUSSIA2018-LOGOFIFA imethibitisha kuwa Droo za kupanga Makundi na Mechi za Fainali za Kombe la Dunia la Mwaka 2018 huko Russia itafanyika Ijumaa Desemba 1 huko Kremlin Jijini Moscow.
Wakati Tarehe ya Droo ilikuwa ishajulikana, mahali pa kuifanyia palikuwa bado hapajatangazwa.
Kwa kuichagua Kremlin, Russia imeonyesha jinsi inavyoipa kipaumbele Fainali hizo.
Kremlin ni Ngome kubwa ya Urusi ambayo inatambuliwa na UNESCO kama moja ya Sehemu za Urithi wa Dunia (UNESCO World Heritage Site).
Kremlin ni eneo ambalo lina Makanisa ya Kiasili na Majumba ya Kifalme na mojawapo ni yale Makazi Rasmi ya Rais wa Urusi Vladimir Putin.
Huko Kremlin Droo yenyewe itafanyika kwenye Jengo la Kifalme liliokuwa likitumika kwa ajili ya Mikutano ya Chama cha Kikomunisti cha Soviet Union na baadae kugeuzwa kuwa Ukumbi wa Burudani.
Ukumbi huo una uwezo wa kuchukua Watazamaji 6,000.
Russia walishinda Kura za kuwa Mwenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 zilizofanyika Desemba 2010 kwa kuwabwaga Wagombea wengine ambao ni Belgium/Netherlands (Waliotaka kuwa Wenyeji wenza), England na Portugal/Spain (Waliotaka kuwa Wenyeji wenza).
Kuanzia Juni 17 na Julai 2 Mwaka huu, Russia watakuwa Wenyeji wa Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara, FIFA CONFEDERATION CUP, ambalo washindani wake ni Russia, kama Mwenyeji, Mabingwa wa Dunia Germany na Mabingwa wa Mabara 6 Duniani amvao ni Australia, Chile, Mexico, New Zealand, Portugal na Bingwa wa AFCON 2017, Kombe la Mataifa ya Afrika ambazo Fainali zake zinaendelea hivi sasa huko Gabon.
Ni desturi kwa Mashindano hayo kufanyika kwa Nchi Mwenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia Mwaka mmoja kabla Fainali zenyewe ili kupima uwezo wao kuandaa Mashindano makubwa.

COSTA, CAHILL WAIPAISHA JUU ZAIDI VINARA CHELSEA!

>>IJAYO NI JAN 31 HUKO ANFIELD, LIVERPOOL-CHELSEA!

EPL – Ligi Kuu England

Ratiba/Matokeo:

Jumapili Januari 22

Southampton 3 Leicester City 0   

Arsenal 2 Burnley 1

Chelsea 2 Hull City 0        

++++++++++++++++++++++++++++++++  

CHELSEA-COSTA-SITVINARA wa EPL, Ligi Kuu England, Chelsea, Jana wamezidi kujizatiti kileleni baada ya kuichapa Hull City 2-0 huko Stamford Bridge.

Ushindi huu umeiweka Chelsea kuwa Pointi 8 mbele ya Timu ya Pili Arsenal.

Bao za ushindi wa Chelsea zilifungwa na Diego Costa na Garry Cahill katika Dakika za 52 ya Kipindi cha EPL-JAN23Kwanza na 81.

Kipindi cha Kwanza cha Mechi hii kilirefushwa kwa Dakika 7 baada ya kusimama kumtibu Majeruhi Mason wa Hull City kwenye Dakika ya 21.

Mechi inayofuata kwa Chelsea ni Ugenini huko Anfield hapo Jumanne Januari 31.

VIKOSI:

Chelsea (Mfumo 3-4-3): Courtois; Azpilicueta, David Luiz, Cahill; Moses, Kante, Matic, Alonso; Pedro, Diego Costa, Hazard.

Akiba: Begovic, Ake, Zouma, Chalobah, Fabregas, Willian, Batshuayi.

Hull (Mfumo 3-5-1-1): Jakupovic; Maguire, Dawson, Davies; Elabdellaoui, Mason, Huddlestone, Clucas, Robertson; Evandro; Hernandez.

Akiba: Marshall, Meyler, Diomande, Maloney, Niasse, Tymon, Bowen.

REFA: Neil Swarbrick.

EPL – Ligi Kuu England

Ratiba

**Saa za Bongo

[Zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku isipokuwa inapotajwa]

Jumanne Januari 31

Arsenal v Watford            

Bournemouth v Crystal Palace               

Burnley v Leicester City              

Middlesbrough v West Bromwich Albion          

Sunderland v Tottenham Hotspur          

Swansea City v Southampton               

2300 Liverpool v Chelsea            

Jumatano Februari 1

West Ham United v Manchester City               

2300 Manchester United v Hull City                

2300 Stoke City v Everton 

Jumamosi Februari 4

1530 Chelsea v Arsenal               

1800 Crystal Palace v Sunderland          

1800 Everton v Bournemouth               

1800 Hull City v Liverpool           

1800 Southampton v West Ham United           

1800 Watford v Burnley              

1800 West Bromwich Albion v Stoke City         

2030 Tottenham Hotspur v Middlesbrough                

Jumapili Februari 5

1630 Manchester City v Swansea City             

1900 Leicester City v Manchester United