CHAMPIONSHIP - NI READING AU HUDDERSFIELD KUPANDA LIGI KUU ENGLAND!

==KUUNGANA NA NEWCASTLE, BRIGHTON!
CHAMPIONSHIP-PLAY-OFFJANA Huddersfield Town wametinga Fainali ya Mechi za Mchujo za Championship kupata Timu 1 itakayopanda kwenda EPL, LIGI KUU ENGLAND, Msimu ujao.
Tayari Newcastle na Brighton, zilishapanda moja kwa moja EPL kwa kumaliza Nafasi za Kwanza na za Pili na ya 3 hupatikana kwa Mechi za Mchujo unaoshirikisha Timu za Nafasi za 3 hadi 6.
Kwenye Mechi ya Kwanza Huddersfield na Sheffield Wednesday zilitoka 0-0 na Jana kuwa 1-1 na Huddersfield kutinga Fainali kwa Penati 4-3.
Kwenye Fainali, Huddersfield watacheza na Reading ambao Juzi waliwabwaga Sheffield Wednesday 1-0 baada ya Sare ya 1-1 katika Mechi ya Kwanza.
Fainali itachezwa huko Wembley Jijini London hapo Mei 29.
MECHI ZA MCHUJO
Ratiba

***Saa za Bongo

Mechi za Kwanza

Jumamosi Mei 13

Fulham 1 Reading 1

Jumapili Mei 14

Huddersfield Town 0 Sheffield Wednesday 0

Mechi za Pili

Jumanne Mei 16

Reading 1 Fulham 0

Jumatano Mei 17

Sheffield Wednesday 1 Huddersfield Town 1 (Penati 3-4)

FAINALI

Jumatatu Mei 29

Wembley, London

1700 Reading v Huddersfield Town

CHAMPIONSHIP: 2 ZIPO LIGI KUU ENGLAND YA 3 ITATOKA MCHUJO!

CHAMPIONSHIP-PLAY-OFFTAYARI Newcastle na Brighton zimepanda Daraja kutoka Championship na Msimu ujao zitacheza EPL, LIGI KUU ENGLAND.

Timu ya 3 itayoungana nao kupanda Daraja itapatikana kutoka Mechi maalum za Mchujo itakazoshirikisha Timu zilizomaliza Nafasi za 3 hadi ya 6.

Timu hizo 4 ni Fulham, Reading, Huddlesfield Town na Sheffield Wednesday.

Droo maalum ya kupanga Mechi 2 za Mchujo imefanyika na Fulham.kupangwa kucheza na Reading wakati Huddersfield Town itacheza na Sheffield Wednesday.

Mechi hizi ni za Nyumbani na Ugenini na Washindi kucheza Fainali Uwanjani Wembley Jijini London na Mshindi kwenda EPL.

MECHI ZA MCHUJO

Ratiba

***Saa za Bongo

Mechi za Kwanza

Jumamosi Mei 13

1930 Fulham v Reading

Jumapili Mei 14

1400 Huddersfield Town v Sheffield Wednesday

Mechi za Pili

Jumanne Mei 16

2145 Reading v Fulham

Jumatano Mei 17

2145 Sheffield Wednesday v Huddersfield Town

FAINALI

Jumatatu Mei 29

Wembley, London

1700 Reading/Fulham v Sheffield Wednesday v Huddersfield Town

UEFA CHAMPIONZ LIGI: JUMANNE JUVE v MONACO, KIPA MKONGWE BUFFON KUIONGOZA JUVE FAINALI?

>>BUFFON ALILIA TAJI HILI AMBALO HAJATWAA!

UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI

Nusu Fainali – Mechi za Marudiano

**Mechi kuanza Saa 3 Dakika 45 Usiku, Saa za Bongo

***Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza

Jumanne Mei 9

Juventus v Monaco [2-0]

Jumatano Mei 10

Atletico Madrid v Real Madrid [0-3]

++++++++++++++++

BUFFON-ALILIA-TAJIKIPA Mkongwe wa Vigogo wa Italy Juventus, Gianluigi Buffon, anaota kutwaa Kombe la UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, ambalo hajawahi kulibeba.
Baada ya kupoteza Fainali 2 za UCL, Jumanne Usiku Buffon ataiongoza Juve wakiwa kwao Mjini Turin kucheza Mechi ya Pili ya Nusu Fainali ya UCL dhidi ya AS Monaco ambayo waliichapa 2-0 Wiki iliyopita huko Monaco.
Mshindi wa Mechi hiyo atakumbana na Mshindi wa Mechi nyingine ya Nusu Fainali kati ya Atletico Madrid na Real Madrid ambao walishinda 3-0 katika Mechi ya Kwanza kwa Bao zote 3 kupigwa na Mchezaji Bora Duniani Cristiano Ronaldo.
Msimu huu, Buffon ameisaidia mno Juve kusonga hadi Nusu Fainali ya Mashindano haya wakiwa hawajafungwa Bao hata Moja kwa Mechi 6 sasa.
Kipa huyo ashawahi kutinga Fainali za UCL mara 2 akiwa na Juve na Mwaka 2003 kutolewa na AC Milan na Miaka Miwili iliyopita kubwagwa na FC Barcelona.
Inaelekea hii ndio nafasi ya mwisho kwa Buffon mwenye Miaka 39 kuwania Ubingwa huu wa Klabu Barani Ulaya na mwenyewe amekiri hilo mbali ya kusema bado anafurahia kushindani na Chipukizi kama Straika wa Monaco Kylian Mbappe mwenye Miaka 18.
Buffon ameeleza: “Mbappe amezaliwa Desemba 1998 wakati mie tayari nshacheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 1998 huko France!”
Akicheza Mechi ya Jumanne na AS Monaco, Buffon atafikisha Mechi 150 za UCL.

UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI

TAREHE MUHIMU:

MECHI ZA MTOANO:

02–03/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Kwanza

09–10/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Pili

03/06/17: Fainali (National Stadium of Wales, Cardiff)

 

 

 

FIFA YAMKOMBOA MESSI, RUKSA KOMBE LA DUNIA ARGENTINA!

MESSI-CAPT-ARGENAHODHA wa Timu ya Taifa ya Argentina Lionel Messi amefutiwa Kifungo cha Mechi 4 na FIFA.

Messi, Fowadi wa Barcelona mwenye Miaka 29, alifungiwa Mechi 4 kwa Kosa la kumtusi Refa Msaidizi kwenye Mechi ya Kanda ya Nchi za Marekani ya Kusini, CONMEBOL, za kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia, Argentina walipofungwa 1-0 na Chile Mwezi Machi.

Messi tayari alikuwa ameikosa Mechi Moja ya Argentina walipofungwa 2-0 na Bolivia.

Leo Kamati ya Rufaa imesema licha ya kutoridhika na kitendo cha Messi lakini ushahidi haukutosheleza kwa Adhabu yake.

Hivyo FIFA imefuta Adhabu hiyo pamoja na Faini ya Pauni 7,800.

++++++++++++++++++++++++

JE WAJUA?

-CONMEBOL itatoa Nchi 4 kutinga Fainali za Kombe la Dunia huko Russia MwakaWC-SA-TEBO-MEI5 2018.

-Nchi hizo zinaweza kuwa 5 ikiwa Timu itakayomaliza Nafasi ya 5 kwenye Kundi lao itashinda Mechi ya Mchujo dhidi ya Timu nyingine toka Bara jingine ambayo itakuwa ni moja toka Kanda ya Oceania yenye Nchi za Visiwani ambazo ni New Zealand, New Caledonia, Fiji, Papua New Guinea, Solomon Islands na Tahiti.

++++++++++++++++++++++++

Hivi sasa Argentina wapo Nafasi ya 5 kwenye Kundi la CONMEBOL lenye Timu 10 ambalo linaoongozwa na Brazil ambayo tayari ishafuzu kwenda Fainali Russia.

ARGENTINA – Mechi zilizobaki:

31 Agosti - Uruguay (Ugenini)

5 Septemba - Venezuela (Nyumbani)

5 Oktoba - Peru (Nyumbani)

10 Oktoba - Ecuador (Ugenini)

CRISTIANO RONALDO - NAMBA ZINAZOMBATIZA ULEJENDARI!

CRISTIANO RONALDO ndie Mchezaji Bora Duniani.
Juzi Usiku ndani ya Estadio Santiago Bernabeu alionyesha tena umahiri wake alipopiga Hetitriki wakati Real Madrid ikiitandika Atletico Madrid 3-0 katika Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Hetitriki hiyo imeweka Rekodi na kumfanya Ronaldo awe Mchezaji wa Kwanza kufunga Hetitriki 2 mfululizo kwenye UCL.
Kwenye Raundi iliyopita, Ronaldo alifunga Bao 5 kati ya 6 wakati Real Madrid ikiitoa Bayern Munich ya Germany kwa Jumla ya Bao 6 katika Mechi 2.
Ronaldo pia ndie Mfungaji Bora katika Historia ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, akiwa na Jumla ya Mabao 103.
PATA PICHA INAYOONYESHA NAMBA ZAKE:
RONALDO-NAMBA-LEJENDARIpHabari MotoMotoZ