EMIRATES FA CUP: LEO NANI KUUNGANA NA CHELSEA FAINALI, ARSENAL AU CITY?

EMIRATES-FACUP-2017-SIT-1LEO WEMBLEY STADIUM itazikutanisha Arsenal na Manchester City kuwania nafasi ya kucheza Fainali ya EMIRATES CUP hapo Mei 27 dhidi ya Chelsea ambayo Jana iliitoa Tottenham Hotspur 4-2 kwenye Nusu Fainali ya Kwanza.
Mechi hii inazikutanisha Timu ambazo zilianza Msimu kwa matarajio makubwa lakini hadi sasa Msimu wao wote umebaki kwenye hii FA CUP baada kupoteza mwelekeo kwenye Ligi Kuu England na pia kutupwa nje ya UEFA CHAMPIONZ LIGI na hata kulikosa Kombe la Ligi, EFL CUP, ambalo limebebwa na Man United.
Tayari Meneja wa Man City Pep Guardiola
ameshaungama kuwa Wamiliki wa Klabu hiyo hawatakuwa na furaha hata wakitwaa FA CUP.
Kwa Arsene Wenger kutwaa FA CUP ni jambo la kufa na kupona kwani Mashabiki wa Arsenal wamemsakama sana Msimu huu wakitaka ang'oke.
Kwenye Ligi Msimu huu City iliifunga Arsenal Mwezi Desemba na mapema Mwezi huu kutoka Sare.

+++++++++++++++++++

JE WAJUA?

-FA CUP 2016/17, ambalo pia hujulikana kama FA Challenge Cup, ni mara ya 136 kushindaniwa kila Mwaka tangu lilipoanzishwe na linatambuliwa kama ndio Mashindano ya kale kupita yote Duniani.

-Kombe hili linadhaminiwa na Kampuni ya Ndege ya Emirates na kwa sababu za kiudhamini linaitwa Emirates FA Cup.

-Timu 736 zilikubaliwa kushiriki Mashindano haya Msimu huu na yalianza kwa Raundi ya Awali na yatafikia Tamati kwa Fainali itakayochezwa Uwanjani Wembley Jijini London hapo Mei 27, 2017.

-Mshindi wa FA CUP ataingizwa Hatua ya Makundi ya UEFA EUROPA LIGI Msimu wa 2017/18.

KUANZIA MSIMU HUU – KUANZIA Robo Fainali:

-Hamna Marudiano ikiwa Timu zipo Sare baada ya Dakika 90. Sare itafuatia Dakika za Nyongeza 30 na kama Gemu bado Sare, zitafuatia Penati ili kupata Mshindi.

-Kila Timu inaruhusiwa kubadili Wachezaji si zaidi ya Wanne lakini huyo wa Nne ni pale tu Gemu ipo Dakika za Nyonfeza 30.

+++++++++++++++++++

Kwenye Mechi hii Arsenal inaweza kumkosa Danny Welbeck mwenye tatizo la Kidole cha Mguu huku Majeruhi wao waliothibitika ni Mustafi, Ospina, Pérez, Cazorla na Reine-Adélaïde.
Kwa upande wa City Majeruhi ni Jesus, Stones, Sagna na Gündogan. 
USO KWA USO:
ARSENAL - Ushindi 96
SARE - 45
MAN CITY - Ushindi 50
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA: 
ARSENAL: Cech, Gabriel, Koscielny, Holding, Ox-Chamberlain, Ramsey, Xhaka, Monreal, Sanchez, Giroud, Ozil
MAN CITY: Caballero, Navas, Kompany, Otamendi, Clichy, Fernandinho, De Bruyne, Sterling, Silva, Sane, Aguero
REFA: Craig Pawson
FA CUP

Ratiba

Nusu Fainali

**Saa za Bongo

Jumapili Aprili 23

1700 Arsenal v Man City

DROO MECHI ZA NUSU FAINALI UEFA CHAMPIONZ LIGI NA EUROPA LIGI IJUMAA!

=KUZAA EL DERBI MADRILENO REAL v ATLETICO?
DROO-UEFA-SITDROO za kupanga Mechi za Mashindano ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, na UEFA EUROPA LIGI zitafanyika Ijumaa Aprili 21 huko Nyon, Uswisi kwenye Makao Makuu ya UEFA.
Tayari Timu zilizotinga Nusu Fainali za UCL zilikamilka hapo Jana wakati 4 za EUROPA LIGI zitajulikana baadae Usiku wa Leo baada kukamilika Mechi 4 za Pili za Robo Fainali.
Kwenye Mechi hizo za Robo Fainali Man United watacheza na RSC Anderlecht (Mechi ya Kwanza 1-1), KRC Genk kuivaa Celta Vigo (2-3), Schalke na Ajax (0-2) na Besiktas kucheza na Lyon (1-2).
Kwenye Chungu cha Droo ya UCL Timu 4 ambazo zimo humo ni Mabingwa Watetezi Real Madrid, Atletico Madrid, Juventus na AS Monaco.
Droo hii haibagui Timu za Nchi moja na hivyo upo uwezekano wa kuwepo El Derbi Madrileno kwa Mahasimu Real na Atletico kupambanishwa.
Droo hizi 2, zile za UCL na EUROPA LIGI, zitaanza Saa 7 Mchana.
Mechi za Nusu Fainali za UCL zitachezwa Mei 2 na 3 na Marudiano Wiki 1 baadae hapo Mei 9 na 10 huku Fainali ikichezwa Cardiff, Wales Juni 3.
Mechi za Nusu Fainali za EUROPA LIGI zitachezwa Alhamisi Mei 4 na kurudiana ni Mei 11.
Fainali ni huko Stockholm, Sweden hapo Mei 24.

LEO BARCELONA INAHITAJI UFANISI WA JUU KUPINDUA 3-0 ZA JUVENTUS - INIESTA

UEFA CHAMPIONZ LIGI

Robo Fainali

Marudiano

***Mechi zote kuanza Saa 3 Dak 45 Usiku

Jumatano Aprili 19

**Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza

Barcelona v Juventus [0-3]

Monaco v Borussia Dortmund [3-2]

++++++++++++++++++++++++++++

UCL-16-17-SITKIUNGO MKONGWE wa Barcelona Andres Iniesta amekiri itakuwa ngumu mno lakini si kitu kisichowezekana kuiga walichowatenda PSG kwa Juventus ambao wanarudiana nao Leo Usiku huko Nou Camp Jijini Barcelona Nchini Spain.
Kwenye Mechi ya kwanza ya Robo Fainali ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, iliyochezwa huko Turin, Italy, Juve waliichapa Barca 3-0.
Lakini katika Raundi iliyopita ya UCL Barca walijikuta kwenye hali kama hii walipotwangwa na PSG 4-0 katika Mechi ya kwanza iliyochezwa huko Paris lakini kwenye Marudiano huko Nou Camp Barca walishusha ngoma kali na kuichabanga PSG 6-1 na wao kusonga kwa Jumla ya Bao 6-5.
Iniesta ameeleza: "Kuna vingi vinafanana kwenye Gemu hii na ile ya PSG. Tunatakiwa tuwe na fikra zilezile tangu Dakika ya kwanza. Ni ngumu kuleta miujiza mingine lakini inawezekana. Lazima tutengeneze nafasi nyingi na kucheza Gemu bora kupita yeyote Msimu huu!"
Ameongeza: "Goli la mapema litatupa nguvu lakini lazima tuwe wavumilivu. Tusipopata Goli tutulie tusiweweseke. Nadhani Juve wamefungwa Bao 2 au 3 Msimu huu wa UCL!"

UEFA CHAMPIONZ LIGI: LEO LEICESTER-ATLETICO, REAL-BAYERN, NANI KWENDA NUSU FAINALI? PATA VIKOSI, DONDOO!

UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI

Robo Fainali

Marudiano

***Mechi zote kuanza Saa 3 Dak 45 Usiku

Jumanne Aprili 18

**Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza

Leicester City v Atletico Madrid [0-1]

Real Madrid v Bayern Munich [2-1]

++++++++++++++++++++++++++++

UCL-2016-17-1-1JUMANNE na Jumatano Usiku ni Mechi za Marudiano za Robo Fainali za UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, ili kupata Washindi wa kusonga Nusu Fainali.

Jumanne zipo Mechi Mbili ambapo huko King Power Stadium, Mabingwa wa England Leicester City wanarudiana na Klabu ya Spain Atletico Madrid ambao Wiki iliyopita walishinda 1-0.

LEICESTER CITY v ATLETICO MADRID

-King Power Stadium, Leicester, England

Leicester City wanapaswa kupindua kipigo cha 1-0 walichopewa Wiki iliyopita huko Vicente Calderon Jijini Madrid ili wasonge kutinga Nusu Fainali.

Leicester wanakabiliwa na upungufu huku Nahodha wao Wes Morgan akiwa bado ana hatihati kucheza hii Leo baada ya kuzikosa Mechi 6 zilizopita akiuguza Mgongo wake huku pia Sentahafu mwenzake Robert Huth akikosekana kwa kuwa Kifungoni.

Kwa upande wa Atletico wao watajumuika nae Straika wa France Kevin Gameiro ambae alizikosa Mechi 5 zilizopita akiuguza Nyonga na pia Koke, Saul Niguez, Gabi na Antoine wote watarejea Uwanjani baada ya Wikiendi iliyopita kupumzishwa kwenye Mechi waliyowafunga Osasuna 3-0 kwenye La Liga.

VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:

LEICESTER: Schmeichel; Simpson, Morgan, Benalouane, Fuchs; Mahrez, Ndidi, Drinkwater, Albrighton; Okazaki; Vardy.

NJE: Huth (Kifungoni), Mendy (Majeruhi), Wague (Majeruhi)

ATLÉTICO MADRID: Oblak; Juanfran, Savić, Godín, Filipe Luís; Carrasco, Saúl, Gabi, Koke; Griezmann, Gameiro.

NJE - Majeruhi: Vrsjalko, Augusto Fernández

REFA: Gianluca Rocchi (Italy)

REAL MADRID v BAYERN Munich

-Santiago Bernabeu, Madrid, Spain

Real Madrid wapo kwenye usukani kutinga Nusu Fainali baada ya Wiki iliyopita kuifunga Bayern Munich 2-1 huko Allianz Arena Jijini Munich Germany.

Kwenye Mechi hiyo, Bayern walitangulia 1-0 lakini Mchezaji Bora Duniani Cristiano Ronaldo akafunga Bao 2 na kuwapa ushindi wa 2-1 Real huku yeye binafsi akiweka Rekodi ya kuwa Mchezaji wa Kwanza kabisa kufikisha Bao 100 katika Mashindano ya Klabu Ulaya.

Kwenye Mechi hii, Real watamkosa Fowadi wao Gareth Bale alieumia Enka Wiki iliyopita lakini Bayern watakuwa nae Straika wao Robert Lewandowski baada ya kuikosa Mechi ya Wiki iliyopita kutokana na maumivu ya Bega.

+++++++++++++

JE WAJUA?

-Bayern wamefungwa Mechi 8 kati ya 10 walizocheza mwisho na Bayern Uwanjani Santiago Bernabeu wakishinda 2 na mara ya mwisho ni 2001 huku wakipoteza 5 zilizopita.

-Real wametinga Nusu Fainali ya UCL kwa Misimu 6 mfululizo iliyopita na safari hii wakisonga hii itakuwa ni Rekodi.

+++++++++++++

Lewandowski ndie tegemezi kubwa la Bayern kwa Mabao akiwafungia Bao 38 katika Mechi 40 Msimu huu.

VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:

REAL MADRID: Navas; Carvajal, Ramos, Nacho, Marcelo; Kroos, Casemiro, Modrić; Isco, Benzema, Ronaldo.

NJE - Majeruhi: Pepe, Varane, Bale

BAYERN MUNICH: Neuer; Lahm, Alonso, Alaba, Bernat; Vidal, Thiago; Robben, Ribéry; Lewandowski, Müller.

NJE - Kifungo:  Javi Martínez

REFA: Viktor Kassai (Hungary)

UEFA CHAMPIONZ LIGI

Robo Fainali

Marudiano

***Mechi zote kuanza Saa 3 Dak 45 Usiku

Jumatano Aprili 19

**Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza

Barcelona v Juventus [0-3]

Monaco v Borussia Dortmund [3-2]

++++++++++++++++++++++++++++

TAREHE MUHIMU:

MECHI ZA MTOANO:

11–12/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Kwanza

18–19/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Pili

02–03/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Kwanza

09–10/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Pili

03/06/17: Fainali (National Stadium of Wales, Cardiff)

 

 

 

FAINALI KOMBE LA DUNIA 2026: USA, CANADA & MEXICO KUOMBA UENYEJI WENZA!

FIFA-WC2026-TIMU48United States, Canada na Mexico zimetangaza kuwa wataombankuwa Wenyeji Wenza wa Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2026.

Fainali hizo ndio zitakuwa ndio za kwanza kushirikisha Timu 48 kutoka 32 za sasa.

Baada kuchezwa huko Brazil Mwaka 2014 na Germany kuibuka Mabingwa wa Dunia, Fainali zijazo zitachezwa huko Russia Mwaka 2018 na zifuatazo ni 2022 huko Qatar.

Ikiwa maombi hayo yatapita hii itakuwa mara ya kwanza kwa Nchi 3 kuwa Wenyeji Wenza wa Fainali za Kombe la Dunia.

Mwaka 2000 Korea Kusini na Japan waliendesha kwa pamoja Fainali za Kombe la Dunia na Brazil kuibuka Bingwa.

Mapendekezo ya Nchi hizo 3 ni kuwa USA itakuwa na Mechi 60 wakati huko Canada na Mexico zitachezwa Mechi 10 kwa kila mmoja.

Uamuzi wa nani atakuwa Mwenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2026 utafanywa Mwaka 2020.

Wakati Canada haijawahi kuwa Mwenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia, USA ilikuwa Mwenyeji Mwaka 1994 na Mexico kuwa Mwenyeji mara mbili, 1970 na 1986, na kuwa Nchi ya kwanza kuwa Mwenyeji mara mbili.

Kwa mujibu wa taratibu za FIFA, Fainali za 2016 haziwezi kuombwa na Nchi za Mabara ya Ulaya na Asia kwa sababu zile za kabla yake, 2018 na 2022, zitachezwa Barani humo. Qatar.