FIFA KOMBE LA MABARA - KUANZA JUMAMOSI RUSSIA: FIFA YAWEZESHA MAREFA KUSTOPU GEMU NA KUIVUNJA WAKIONA UBAGUZI!

FIFA Kombe la Mabara, Mashindano ambayo huandaliwa na FIFA Mwaka Mmoja kabla ya Fainali za Kombe la Dunia kwenye Nchi ambayo ndiyo Wenyeji wa Fainali hizo, yanaanza Jumamosi hii inayokuja huko Russia na kushirikisha Nchi 8 na moja ya mambo makubwa ambayo FIFA yamefanya ni kuwezesha Marefa kusimamisha Gemu endapo Mashabiki watakashifu na kunyanyasa Kibaguzi Uwanjani wakati wa Mechi.

FIFA-NORussia, ambao ndio Wenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018, hawana sifa nzuri ya kutenda haki Uwanjani na mara nyingi kumekuwa na karaha mbaya za Kibaguzi.

Sasa FIFA imewapa pawa Marefa kwenye Kombe la Mabara kusimamisha Gemu na hata kuivunja kabisa wakiona matukio ya kashfa na unyanyasaji Kibaguzi Uwanjani kutoka kwa Washabiki.

Mbali ya hilo, FIFA pia imesema Uwanjani watamwagwa Wasimamizi wa Vitendo vya Kibaguzi.

Akiongea kuhusu hatua hii, Rais wa FIFA, Gianni Infantino, amenena: “Haya ni mapya kwenye vita dhidi ya Ubaguzi. Hatua zote tulizochukua ni zana za ziada kwa Marefa na Maafisa wa Mechi kuzuia tabia za Kibaguzi na kuhakikisha Uwanjani kuna Mchezo wa Haki na Heshima!”

Hatua ya kuweka Wasimamizi wa Vitendo vya Kibaguzi ni mwendelezo wa maamuzi ya FIFA ambayo yalianzia kwenye Mechi za Mchujo za kutinga Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 zitakazochezwa Russia na baadhi ya Mechi za Kirafiki za Kimataifa.

FIFA Kombe la Mabara linaanza Jumamosi kwa Russia, ambao ndio Wenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018, kuanza kucheza na New Zealand katika Mechi ya Kundi A itakayochezwa Saint Petersburg Stadium, Saint Petersburg.

Nchi nyingine 7 zinazoshiriki ni Germany, ambao ni Mabingwa Watetezi wa Kombe la Dunia walilotwaa Mwaka 2014 huko Brazil, na Nchi nyingine ni Mabingwa wa Mabara ya Kisoka ya FIFA.

Kundi A lina Russia, New Zealand, Portugal na Mexico wakati Kundi B wapo Germany, Cameroon, Chile na Australia.

++++++++++++++++

MAKUNDI:

KUNDI A

KUNDI B

Russia (Wenyeji)

Cameroon (CAF)

New Zealand (OFC-Oceania Footbal Confederation)

Chile (CONMEBOL)

Portugal (UEFA)

Australia (AFC)

Mexico (CONCACAF)

Germany (Mabingwa Watetezi)

++++++++++++++++

Kabla ya Mechi ya ufunguzi kati ya Russia na Germany kutakuwa na Sherehe rasmi za Ufunguzi wa Mashindano haya zitakazodumu Dakika 20.

Mechi za Mashindano haya zitachezwa katika Miji minne ya Nchini Russia na hiyo ni Saint Petersburg, Kazan, Sochi na Moscow.

FIFA KOMBE LA MABARA

Hatua ya Kwanza

Jumamosi Juni 17

KUNDI A

Saint Petersburg Stadium, Saint Petersburg

1800 Russia v New Zealand

Jumapili Juni 18

KUNDI A

Kazan Arena, Kazan

1800 Portugal v Mexico

KUNDI B

Spartak Stadium, Moscow

2100 Cameroon v Chile 

Jumatatu Juni 19

KUNDI B

Fisht Stadium, Sochi

1800 Australia v Germany

Jumatano Juni 21

KUNDI A

Spartak Stadium, Moscow

1800 Russia v Portugal

Fisht Stadium, Sochi

2100 Mexico v New Zealand

Alhamisi Juni 22

KUNDI B

Saint Petersburg Stadium, Saint Petersburg

1800 Cameroon v Australia

Kazan Arena, Kazan

2100 Germany v Chile

Jumamosi Juni 24

KUNDI A

Kazan Arena, Kazan

1800 Mexico v Russia

Saint Petersburg Stadium, Saint Petersburg

1800 New Zealand v Portugal

Jumapili Juni 25

KUNDI B

Fisht Stadium, Sochi

1800 Germany v Cameroon

Spartak Stadium, Moscow

1800 Chile v Australia

Hatua ya Pili

Nusu Fainali

Jumatano Juni 28

Kazan Arena, Kazan

2100 Mshindi Kundi A v Mshindi wa Pili Kundi B [NF1]

Alhamisi Juni 29

Fisht Stadium, Sochi

2100 Mshindi Kundi B v Mshindi wa Pili Kundi A [NF2]

Mshindi wa 3

Jumapili Julai 2

Spartak Stadium, Moscow

1500 Atakaefungwa NF1 v Atakaefungwa NF2

FAINALI

Jumapili Julai 2

Saint Petersburg Stadium, Saint Petersburg

2100 Mshindi NF1 v Mshindi NF2

Habari MotoMotoZ