KIMATAIFA KIRAFIKI: MTU 10 FRANCE WAIPIGA ENGLAND, VARANE NYEKUNDU KWA MSAADA WA VARs!

Jumanne Juni 13

Matokeo:

Australia 0 Brazil 4           

Singapore 0 Argentina 6             

Indonesia 0 Puerto Rico 0           

South Africa 1 Zambia 2             

Norway 1 Sweden 1         

Romania 3 Chile 2            

Cameroon 0 Colombia 4             

France 3 England 2

++++++++++++++++++++++

FRANCE-ENGLANDHuko Stade de France, Saint Denis, Wenyeji Mtu 10 France wameichapa England 3-2 katika Mechi ya Kimataifa ya Kirafiki chini ya Kalenda ya FIFA iliyochezwa Jana.

Hadi Mapumziko France walikuwa mbele 2-1 kwa Bao za Dakika ya 22 na 43 za Samuel Umtiti na Djibril Sidibe lecha England kutangulia Dakika ya 9 kwa Bao la Harry Kane.

England walisawazisha Dakika 3 baada ya Kipindi cha Pili kuanza kupitia Penati ya Harry Kane ambayo ilitolewa baada ya Beki Raphael Varane wa France kugongana na Dele Alli wa England.

Awali Refa Davide Massa wa Italy alitoa Penati hiyo lakini akaomba Msaada wa VAR, Video Assistant Referee, ambayo ilithibitisha Penati na pia kuamua Varane apewe Kadi Nyekundu.

++++++++++++++FIFA-VARS2

JE WAJUA?

-VARs=Video Assistant Referee:

-Kwenye Mfumo huo wa Video, Refa Msaidizi atakuwepo pembeni mwa Uwanja na atakuwa na Mawasiliano na Refa wa Mechi wakati wote wa Mechi hiyo akipitia Video bila kusitisha Mechi.

-Ikiwa litatokea tukio ambalo Refa Msaidizi ameliona atamtonya Refa wa Mechi ambae ana ruksa ya kuukubali ushauri huo au akaamua mwenyewe kwenda pembeni kulipitia na kutoa uamuzi wake.

-Ama Refa anaweza kumuomba Refa Msaidizi wa VARs kulipitia tukio ili ampe ushauri.

++++++++++++++

Licha France kubaki Mtu 10, iliendelea kuwa juu na hasa kung’ara kwa Kiungo wa Man United Paul Pogba, Fowadi wa Borussia Dortmund Ousmane Dembele na Chipukizi wa Miaka 18 wa AS Monaco Kylian Mbappe.

Zikibaki Dakika 12 Mpira kwisha, France walipiga Bao la 3 na la ushindi kupitia Ousmane Dembele alipopokea Pasi ya Mbappe.

VIKOSI:

FRANCE: Lloris; Sidibé, Varane, Umtiti, Mendy; Dembélé, Kanté, Pogba, Lemar; Giroud, Mbappé

Akiba: Areola, Jallet, Kimpembe, Griezmann, Payet, Matuidi, Rabiot, Digne, Sissoko, Lacazette, Koscielny, Tolisso, Zouma, Thauvin, Costil.

ENGLAND: Heaton; Jones, Stones, Cahill; Trippier, Dier, Alli, Bertrand; Sterling, Kane, Oxlade-Chamberlain

Akiba: Butland, Walker, Cresswell, Gibson, Smalling, Livermore, Defoe, Lallana, Rashford, Lingard, Forster, Hart.

REFA: Davide Massa (Italy)

Habari MotoMotoZ