KIMATAIFA KIRAFIKI: JUMANNE AUSTRALIA v BRAZIL, FRANCE v ENGLAND

Jumanne Juni 13

**Saa za Bongo

1305 Australia v Brazil                

1500 Singapore v Argentina                 

1730 Indonesia v Puerto Rico               

2000 South Africa v Zambia                  

2045 Norway v Sweden              

2100 Romania v Chile                

2130 Cameroon v Colombia                 

2200 France v England

++++++++++++++++++++++

BRA-ARGMECHI za Kimataifa za Kirafiki chini ya Kalenda ya FIFA zinaendelea Jumanne kwa Mechi kadhaa zikiwemo zile za Australia na Brazil na ile ya France na England.

Brazil, ambao Ijumaa walipoteza Rekodi yao ya kutofungwa chini ya Kocha Tite walipopigwa 1-0 na Argentina huko Melbourne, Australia, watabaki Uwanja ule ule wa Melbourne Cricket Ground na kucheza na Wenyeji Australia.

Argentina wao wameruka na watakuwa huko Singapore kuwavaa Wenyeji Singapore.

Nao England, baada ya kutoka 2-2 Juzi na Scotland katika Mechi ya Kundi lao la kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia, wako Stade de France, Saint-Denis, kucheza na Wenyeji France ambao Juzi walifungwa 2-1 na Sweden kwenye Mechi ya Kundi lao la Kombe la Dunia 2018.

Kwenye Mechi hii, Kocha wa England Gareth Southgate ameshatangaza Kipa Joe Hart hatakaa Golini na badala yake Tom Heaton ataanza na kisha Jack Butland kucheza Kipindi cha Pili.

Pia, Straika wa Tottenham, Harry Kane, ataendelea kuwa Nahodha kama alivyokuwa kwenye Mechi na Scotland.

Habari MotoMotoZ