FIFA KOMBE LA DUNIA KWA KLABU: VARs YATUMIKA KWA MARA YA KWANZA KUTOA PENATI, WENYEJI KASHIMA WATINGA FAINALI!

VARS-REFA-KASSAIWENYEJI Kashima Antlers Leo wametinga Fainali ya Mashindano ya FIFA ya Kombe la Dunia kwa Klabu huko Suita City Stadium Nchini Japan kwa kuwachapa Atletico Nacional Bao 3-0 huku Bao lao la Kwanza likifungwa kutokana Msaada wa Teknolojia ya VARs kuwapa Penati.

Refa Msaidizi aliekuwa nje ya Uwanja akichambua Mechi kwenye Video alimbonyeza Refa wa Mechi hiyo Viktor Kassai kutoka Hungary kuhusu Kosa la Orlando Berrio Mchezaji wa Attletico ndani ya Boksi na Kassai kwenda pembeni ya Uwanja kuliangalia tukio hilo kwenye Kompyuta na kuafiki ni Penati.

Penati hiyo ilitolewa kwenye Dakika ya 33 na Shoma Doi kufunga na Kashima kuongoza 1-0.

Bao nyingine za Kashima zilifungwa Dakika za 83 na 85 Wafungaji wakiwa Yasushi Endo na Yuma Suzuki.

 ++++++++++++++++++++++++++++++

JE WAJUA?
-
Kombe la Dunia kwa Klabu hushirikisha Klabu Bingwa za Mabara 6 ya Mashirikisho ya Soka Wanachama wa FIFA pamoja na Klabu Bingwa ya Nchi Wenyeji Japan.

VARS:

- Mfumo wa Majaribio uitwao VARs, Video Assistant Referees.

Mfumo wa Video kusaidia maamuzi ya Marefa Uwanjani, VARs [Video Assistant Referes] umefanyiwa Majaribio rasmi ya FIFA kwa mara ya kwanza katika Mechi ya Kimataifa hapo Septemba 1 wakati Italy ilipocheza na France huko Bari.

Kwenye Mfumo huo wa Video, Refa Msaidizi anakuwepo pembeni mwa Uwanja na anakuwa na Mawasiliano na Refa wa Mechi wakati wote wa Mechi hiyo akipitia Video bila kusitisha Mechi.

Ikiwa litatokea tukio ambalo Refa Msaidizi ameliona atamtonya Refa wa Mechi ambae ana ruksa ya kuukubali ushauri huo au au akaamua mwenyewe kwenda pembeni kutizama na kuliptia tukio na kutoa uamuzi wake.

Ama Refa huyo anaweza kumuomba Refa Msaidizi kulipitia tukio ili ampe ushauri.

++++++++++++++++++++++++++++++

Katika Mechi nyingine iliyochezwa mapema Leo huko huko Japan kusaka Mshindi wa 5, Jeonbuk Hyundai Motorsya Korea iliwafumua Mabingwa wa Afrika Mamelodi Sundowns kutoka Afrika Kusini Bao 4-1.

Kwenye Nusu Fainali iliyobaki na ambayo itachezwa Alhamisi, Club America watacheza na Real Madrid na Mshindi

FIFA KOMBE LA DUNIA KWA KLABU

Ratiba/Matokeo

**Saa za Bongo

Alhamisi Des 8

Kashima Antlers 2 Auckland City 1

Jumapili Des 11

Robo Fainali

Jeonbuk Hyundai Motors 1 América 2

Mamelodi Sundowns 0 Kashima Antlers 2

Jumatano Des 14

Mshindi wa 5

Jeonbuk Hyundai Motors 4 Mamelodi Sundowns 1

Nusu Fainali

Atlético Nacional 0 Kashima Antlers 3

Alhamisi Des 15

1300 Club América v Real Madrid

Jumapili Des 18

1000 Atletico Nacional v Club America/Real Madrid

1300 Kashima Antlers v Club America/Real Madrid