FIFA KOMBE LA DUNIA KWA KLABU: LEO NUSU FAINALI WENYEJI KASHIMA NA ATLETICO!

==ALHAMISI RONALDO NA REAL DIMBANI KUIVAA CLUB AMERICA!
FIFA-CLUB-WC2016LEO Nusu Fainali ya kwanza ya Mashindano ya FIFA ya Kombe la Dunia kwa Klabu itachezwa huko Suita City Football Stadium Nchini Japan kati ya Wenyeji Kashima Antlers na Atletico National ya Colombia.
Wakati Atletico wakianzia hatua hii, Kashika walitoka Raundi za Awali na kwenye Robo Fainali kuwabwaga Klabu Bingwa ya Afrika Mamelodi Sundowns ta Afrika Kusini.
Nusu Fainali nyingine itachezwa Kesho Alhamisi huko International Stadium Mjini Yokohama Nchini Japan kati ya Club America ya Mexico na Real Madrid wanaoanzia hatua hii.
Mvuto mkubwa wa Mechi hiyo ni kumuona Staa wa Real Cristiano Ronaldo akicheza Mechi yake ya kwanza tangu Juzi atwae Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani kwa Mwaka 2016 ijulikanayo kama Ballon D'oR.
++++++++++++++++++++++++++++++
JE WAJUA?
-Kombe la Dunia kwa Klabu hushirikisha Klabu Bingwa za Mabara 6 ya Mashirikisho ya Soka Wanachama wa FIFA pamoja na Klabu Bingwa ya Nchi Wenyeji Japan.
++++++++++++++++++++++++++++++
Lakini kabla ya Mechi hiyo ya Nusu Fainali ya Leo itapigwa Mechi ya kusaka Mshindi wa 5 kati ya Jeonbuk Hyundai Motors na Mamelodi Sundowns.
FIFA KOMBE LA DUNIA KWA KLABU
Ratiba/Matokeo
**Saa za Bongo
Alhamisi Des 8
Kashima Antlers 2 Auckland City 1
Jumapili Des 11
Robo Fainali
Jeonbuk Hyundai Motors 1 América 2
Mamelodi Sundowns 0 Kashima Antlers 2
Jumatano Des 14
Mshindi wa 5
1030 Jeonbuk Hyundai Motors v Mamelodi Sundowns
Nusu Fainali
1330 Atlético Nacional v Kashima Antlers
Alhamisi Des 15
1300 Club América v Real Madrid
Jumapili Des 18
1000 Kusaka Mshindi wa 3
1300 Fainali

Habari MotoMotoZ