Ballon d'Or 2016: LEO NI CRISTIANO RONALDO AU LIONEL MESSI KUZOA?

IMG-20161212-WA0000LEO MCHEZAJI BORA WA SOKA DUNIANI KWA MWAKA 2016 atakaezoa Tuzo ya Ballon d'Or atapatikana toka Listi ya Wagombea 30.
Masupastaa Cristiano Ronaldo na Lionel Messi ndio wanaopewa nafasi kubwa kuwini Tuzo hii.
Fowadi wa Barcelona Messi, ndie anaeshikilia Tuzo hii na pia kuitwaa mara 5 katika Miaka 7 iliyopita.
Ballon d'Or inasimamiwa na Jarida maarufu France Football na Mshindi wake hupatikana kwa Kura za Wanahabari 173 toka kila pembe ya Dunia.
France Football imekuwa ikisimamia Ballon d'Or kila Mwaka tangu 1956 lakini kwa Miaka 6 iliyopita wamekuwa wakishirikiana na FIFA na Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani wa Mwaka kuitwa FIFA Ballon d'Or 
Lakini Mwezi Septemba FIFA ikajitoa na kuanzisha Tuzo yao ikuwemo zile za Kinamama, Timu ya Mwaka na Washindi wake wanategemewa kutangazwa kwenye Hafla maalum hapo Januari 9 huko Zurich.
WAGOMBEA 30 WA 2016 Ballon d'Or:
Sergio Aguero (Manchester City), Pierre-Emerick Aubameyang (Borussia Dortmund), Gareth Bale (Real Madrid), Gianluigi Buffon (Juventus), Cristiano Ronaldo (Real Madrid), Kevin de Bruyne (Manchester City), Paulo Dybala (Juventus), Diego Godin (Atletico Madrid), Antoine Griezmann (Atletico Madrid), Gonzalo Higuain (Juventus), Zlatan Ibrahimovic (Manchester United), Andres Iniesta (Barcelona), Koke (Atletico Madrid), Toni Kroos (Real Madrid), Robert Lewandowski (Bayern Munich), Hugo Lloris (Tottenham Hotspur), Riyad Mahrez (Leicester City), Lionel Messi (Barcelona), Luka Modric (Real Madrid), Thomas Muller (Bayern Munich), Manuel Neuer (Bayern Munich), Neymar (Barcelona), Dimitri Payet (West Ham), Pepe (Real Madrid), Paul Pogba (Manchester United), Rui Patricio (Sporting Lisbon), Sergio Ramos (Real Madrid), Luis Suarez (Barcelona), Jamie Vardy (Leicester City), Arturo Vidal (Bayern Munich).

Habari MotoMotoZ