FIFA KOMBE LA DUNIA KWA KLABU: WENYEJI KASHIMA WAWABWAGA MABINGWA WA AFRIKA MAMELODI NA KUTINGA NUSU FAINALI!

FIFA-CLUB-WC-KASHIMA-MAMELODIWENYEJI Kashima Antlers Leo wamesonga Nusu Fainali ya Mashindano ya FIFA ya Kombe la Dunia kwa Klabu huko Suita City Stadium Nchini Japan kwa kuwachapa Mabingwa wa Afrika Mamelodi Sundowns ya South Africa Bao 2-0.

Bao za Kashima zilifungwa na Ysushi Endo na Mu Kanazaki katika Dakika za 63 na 88.

Katika Mechi nyingine ya Robo Fainali iliyochezwa hapo hapo Suita City Stadium, Club America ya Mexico imeifunga Jeonbuk Hyundai Motors ya Korea Kusini Bao 2-1 na kutinga Nusu Fainali.

Bao la Jeonbuk Hyundai Motors lilifungwa Dakika ya 23 na Bo-Kyung Kim na Kipindi cha Pili Club America kujibu kwa Bao 2 za Dakika za 58 na 74 Mfungaji akiwa Silvio Romero.

++++++++++++++++++++++++++++++

JE WAJUA?
-
Kombe la Dunia kwa Klabu hushirikisha Klabu Bingwa za Mabara 6 ya Mashirikisho ya Soka Wanachama wa FIFA pamoja na Klabu Bingwa ya Nchi Wenyeji Japan.

++++++++++++++++++++++++++++++

Kwenye Nusu Fainali ambazo zitachezwa Jumatano na Alhamisi, Atlético Nacional ya itaivaa Kashima Antlers na Club America kucheza na Real Madrid.

Lakini kabla ya Mechi hizo itapigwa Mechi ya kusaka Mshindi wa 5 kati ya Jeonbuk Hyundai Motors na Mamelodi Sundowns.

FIFA KOMBE LA DUNIA KWA KLABU

Ratiba/Matokeo

**Saa za Bongo

Alhamisi Des 8

Kashima Antlers 2 Auckland City 1

Jumapili Des 11

Robo Fainali

Jeonbuk Hyundai Motors 1 América 2

Mamelodi Sundowns 0 Kashima Antlers 2

Jumatano Des 14

Mshindi wa 5

1030 Jeonbuk Hyundai Motors v Mamelodi Sundowns

Nusu Fainali

1330 Atlético Nacional v Kashima Antlers

Alhamisi Des 15

1300 Club América v Real Madrid

Jumapili Des 18

1000 Kusaka Mshindi wa 3

1300 Fainali

Habari MotoMotoZ