FIFA KOMBE LA DUNIA KWA KLABU: YAANZA WENYEJI KASHIMA WASHINDA, KUIVAA MAMELODI SUNDOWNS JUMAPILI!

FIFA-CLUB-WC-KASHIMAWENYEJI Kashima Antlers Leo wamefungua Mashindano ya FIFA ya Kombe la Dunia kwa Klabu huko International Stadium Yokohama, Jijini Yokohama Nchini Japan kwa kuichapa Auckland City ya New Zealand Bao 2-1.

Hii ilikuwa ni Mechi ya Raundi ya Awali na sasa Kashima wanaingia Robo Fainali ambapo Jumapili watacheza na Mamelodi Sundowns huko Suita City Football Stadium Mjini Osaka.

Auckland City walitangulia kufunga kwa Bao la Kichwa la Kim Daewook alieunganisha Frikiki ya Emiliano katika Dakika ya 50 minutes na Dakika 17 baadae Shuhei Akasaki akaisawazishia Kashima.

Huku Gemu ikiwa inayoyoma, Mu Kanazaki wa Kashima akafunga Bao la Pili na la ushindi katika Dakika ya 88.FIFA-CLUB-WC2016

++++++

JE WAJUA?
-
Kombe la Dunia kwa Klabu hushirikisha Klabu Bingwa za Mabara 6 ya Mashirikisho ya Soka Wanachama wa FIFA pamoja na Klabu Bingwa ya Nchi Wenyeji Japan.

++++++

Gemu hii ilikuwa ni ya Kihistoria kwa mambo Mawili.

Kwanza ni Gemu ya 100 kwa Mashindano ya FIFA ya Kombe la Dunia kwa Klabu na pia Leo Marefa wa Mechi hiI waLIpata msaada wa maamuzi yao kwa kutumia Video kutoka kwa Mfumo wa Majaribio uitwao VARs, Video Assistant Referees.

Kwenye Mfumo huo wa Video, Refa Msaidizi anakuwepo pembeni mwa Uwanja na anakuwa na Mawasiliano na Refa wa Mechi wakati wote wa Mechi hiyo akipitia Video bila kusitisha Mechi.

Ikiwa litatokea tukio ambalo Refa Msaidizi ameliona atamtonya Refa wa Mechi ambae ana ruksa ya kuukubali ushauri huo au au akaamua mwenyewe kwenda pembeni kutizama Marudio ya Video na kulipitia tukio na kutoa uamuzi wake.

Ama Refa huyo anaweza kumuomba Refa Msaidizi kulipitia tukio lenyewe ili ampe ushauri.

FIFA KOMBE LA DUNIA KWA KLABU

Ratiba/Matokeo

**Saa za Bongo

Alhamisi Des 8

Kashima Antlers 2 Auckland City 1

Jumapili Des 11

Robo Fainali

1000 Jeonbuk Hyundai Motors v América

1330 Mamelodi Sundowns v Kashima Antlers

Jumatano Des 14

Mshindi wa 4

1030 Aliefungwa Robo Fainali 1 v Aliefungwa Robo Fainali 2

Nusu Fainali

1330 Atlético Nacional v Mshindi Robo Fainali 1

Alhamisi Des 15

1300 Mshindi Robo Fainali 2 v Real Madrid

Jumapili Des 18

1000 Kusaka Mshindi wa 3

1300 Fainali

Habari MotoMotoZ