FIFA KOMBE LA DUNIA KWA KLABU: LEO LAANZA, VIDEO KUTUMIKA KUSAIDIA MAREFA!

FIFA-CLUB-WC2016Mashindano ya FIFA ya Kombe la Dunia kwa Klabu yanaanza Leo huko Japan na Marefa wa Mechi hizo watapata msaada wa maamuzi yao kwa kutumia Video kutoka kwa Mfumo wa Majaribio uitwao VARs, Video Assistant Referees.
Mfumo wa Video kusaidia maamuzi ya Marefa Uwanjani, VARs [Video Assistant Referes] umefanyiwa Majaribio rasmi ya FIFA kwa mara ya kwanza katika Mechi ya Kimataifa hapo Septemba 1 wakati Italy ilipocheza na France huko Bari.
Kwenye Mfumo huo wa Video, Refa Msaidizi anakuwepo pembeni mwa Uwanja na anakuwa na Mawasiliano na Refa wa Mechi wakati wote wa Mechi hiyo akipitia Video bila kusitisha Mechi.
Ikiwa litatokea tukio ambalo Refa Msaidizi ameliona atamtonya Refa wa Mechi ambae ana ruksa ya kuukubali ushauri huo au au akaamua mwenyewe kwenda pembeni kutizama na kuliptia tukio na kutoa uamuzi wake.
Ama Refa huyo anaweza kumuomba Refa Msaidizi kulipitia tukio ili ampe ushauri.
VARs imekuwa ikitumika kwa Majaribio huko USA kwenye Ligi Daraja la 3 na sasa FIFA, ikishirikiana na IFAB, ambacho ndicho chombo pekee kinachoweza kubadili Sheria za Soka, vimeafika Majaribio hayo na sasa yameingia hatua mpya ya Majaribio kwenye IMG-20161208-WA0002Mechi za Kimataifa.
Hivi sasa, kwenye Soka, inatumika Teknloji ya Kuamua kama Mpira umevuka Mstari wa Goli, GLT [Goal Line Technology] ambayo humsaidia Refa kuamua kama ni Goli au si Goli.
Kombe la Dunia kwa Klabu hushirikisha Klabu Bingwa za Mabara 6 ya Mashirikisho ya Soka Wanachama wa FIFA pamoja na Klabu Bingwa ya Nchi Wenyeji Japan.
Mashindano hayo yanaanza Leo huko Yokohama kwa Wenyeji Kashima Antlers kucheza na Auckland City ya New Zealand.
Mabingwa wa Ulaya Real Madrid watacheza Mechi yao ya kwanza Desemba 15.
Barcelona ndio waliotwaa Ubingwa huu Mwaka Jana kwa kuifunga Klabu ya Argentina River Plate 3-0.
FIFA KOMBE LA DUNIA KWA KLABU
Ratiba
**Saa za Bongo
Alhamisi Des 8
1330 Kashima Antlers V Auckland City
Jumapili Des 11
Robo Fainali
1000 Jeonbuk Hyundai Motors V América
1330 Mamelodi Sundowns V  Mshindi wa Mechi ya Kwanza
Jumatano Des 14
Mshindi wa 4
1030 Aliefungwa Robo Fainali 1 V Aliefungwa Robo Fainali 2
Nusu Fainali
1330 Atlético Nacional V Mshindi Robo Fainali 1
Alhamisi Des 15
1300 Mshindi Robo Fainali 2 V Real Madrid
Jumapili Des 18
1000 Kusaka Mshindi wa 3
1300 Fainali