MAN CITY, CHELSEA KWA PILATO FA KWA VURUGU ZA WACHEZAJI WAO!

CITY-CHE-VITAManchester City na Chelsea zimefunguliwa Mashitaka na FA, Chama cha Soka England, kwa kushindwa kudhibiti Wachezaji wao kufuatia vurugu za Wachezaji hao mwishoni mwa Mechi yao ya EPL, Ligi Kuu England, iliyochezwa Jumamosi Uwanjani Etihad na Chelsea kushinda 3-1.

Rabsha hiyo ya Wachezaji wa Timu hizo ilitokea Dakika za Majeruhi, Dakika ya 95, wakati Fowadi wa City, Sergio Aguero, alipomchezea Rafu mbaya Beki wa Chelsea David Luis na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu na tukio kusababisha Wachezaji kuvaana na Kiungo wa City Fernandinho kutolewa kwa Kadi Nyekundu baada kuvamiana na Mchezaji wa Chelsea Cesc Fabregas ambae hatachukuliwa hatua yeyote.

Wote, Aguero na Fernandinho, watakuwa Kifungoni kwa Aguero kuwa ‘Jela’ Mechi 4 na Fernandinho Mechi 3.

Lakini kwa vile Aguero alishawahi kufungiwa Mechi 3 Mwezi Agosti kwa kumpiga kiwiko Mchezaji wa West Ham Winston Reid, Kifungo cha sasa kimeongezwa Mechi 1 zaidi.

Kifungo hicho cha Aguero kitamfanya azikose Mechi za City dhidi ya Leicester, Watf ord, Arsenal na Hull.

Man City na Chelsea zimepewa hadi Saa 3 Usiku Desemba 8 kujibu Mashitaka yao.

EPL, LIGI KUU ENGLAND

Ratiba:

**Saa za Bongo

Jumatatu Desemba 5

2300 Middlesbrough v Hull City   

Jumamosi Desemba 10

1530 Watford v Everton    

1800 Arsenal v Stoke City           

1800 Burnley v Bournemouth      

1800 Hull City v Crystal Palace    

1800 Swansea City v Sunderland 

2030 Leicester City v Manchester City             

Jumapili Desemba 11

1500 Chelsea v West Bromwich Albion  

1715 Manchester United v Tottenham Hotspur           

1715 Southampton v Middlesbrough               

1930 Liverpool v West Ham United                 

Jumanne Desemba 13

2245 Bournemouth v Leicester City       

2245 Everton v Arsenal     

Jumatano Desemba 14

2245 Middlesbrough v Liverpool  

2245 Sunderland v Chelsea         

2240 West Ham United v Burnley

2300 Crystal Palace v Manchester United

2300 Manchester City v Watford            

2300 Stoke City v Southampton            

2300 Tottenham Hotspur v Hull City               

2300 West Bromwich Albion v Swansea City              

Jumamosi Desemba 17

1530 Crystal Palace v Chelsea               

1800 Middlesbrough v Swansea City     

1800 Stoke City v Leicester City  

1800 Sunderland v Watford                  

1800 West Ham United v Hull City          

2030 West Bromwich Albion v Manchester United      

Jumapili Desemba 18

1630 Bournemouth v Southampton       

1900 Manchester City v Arsenal   

1900 Tottenham Hotspur v Burnley                 

Jumatatu Desemba 19

2300 Everton v Liverpool  

         

Habari MotoMotoZ