SPURS KUTOUZA STAA YEYOTE, SANCHEZ KUTOUZWA KWA MPINZANI ENGLAND!

PATA ZILIZOBAMBA ENGLAND:
SPURS KUBAKISHA MASTAA WAKE
DELE-ALLITottenham itahakikisha Mastaa wao wote wanabakia Klabuni hapo na kuwauza tu wale ambao hawawahitaji kwa mujibu wa Meneja wao Mauricio Pochettino.
Spurs, ambao wako Nafasi ya Pili kwenye EPL, Ligi Kuu England, wanasakamwa na Klabu nyingine zinazowawinda Mastaa wao wakubwa wanaofanya vizuri Msimu huu.
Lakini Pochettino ambae amedai Mwenyekiti wa Klabu Daniel Levy wana uhusiano mzuri amesema Mkuu huyo amemhakikishia hawatauza Staa wao yeyote kwa sababu hawana shida na Fedha.
Pochettino amesisitiza: "Wachezaji tunaotaka wabaki watabaki!"
Miongoni mwa wanaosakwa na Klabu pinzani huko England ni Mabeki Kyle Walker na Danny Rose, Viungo Christian Eriksen na Dele Alli na Fowadi Harry Kane.
SANCHEZ HAUZWI KWA MPINZANI ENGLAND!
FOWADI hatari wa Arsenal Alexis Sanchez hatauzwa kwa Mpinzani yeyote wa Arsenal huko England kwa mujibu wa Meneja wa Klabu hiyo Arsene Wenger.
Sanchez, Mchezaji wa Kimataifa kutoka Chile ambae Majuzi Jumapili aliifungia Arsenal Bao la ushindi walipowafunga Man City na kutinga Fainali ya FA CUP, amebakiza Mwaka mmoja tu kwenye Mkataba wake wa sasa huku akigomea kusaini Mkataba mpya.
Wenger ameeleza: "Sidhani kama unaweza kumuuza kwa Klabu nyingine ya Ligi Kuu England, huo ndio ukweli! Lakini kama nlivyosema nadhani atabaki na kusaini Mkataba!"
Ingawa yeye binafsi hajathibitisha kubaki Arsenal kwa Msimu ujao huku Mkataba wake ukiisha Juni, Wenger amesisitiza anashughulikia ununuaji Wachezaji wapya kwa ajili ya Msimu ujao.
Ameeleza: "Nipo kazini hadi Siku ya mwisho ya Msimu nkishughulikia ya sasa na baadae. Ununuzi wa Wachezaji wapya hatima ya Klabu na ni muhimu. Hatima yangu si muhimu, ya Klabu ndio muhimu!"

N'GOLO KANTE AZOA TUZO YA PFA, NDIE BORA ENGLAND!

>>DELE ALLI BORA KWA VIJANA MSIMU WA PILI MFULULIZO!
KANTE-TWITTERKIUNGO wa Chelsea N'Golo Kante amezoa Tuzo ya Mchezaji Bora kwa Msimu wa 2016/17 inayotolewa na PFA ( Professional Footballers Association), Chama cha Wachezaji Soka wa Kulipwa huko England.
Kiungo huyo wa Chelsea wa Miaka 26 anaetoka France aliwabwaga Eden Hazard, Harry Kane, Romelu Lukaku, Zlatan Ibrahimovic na Alexis Sanchez katika Kura iliyopigwa na Wachezaji wenzake wa Kulipwa.
Kwenye Tuzo ya Mchezaji Kijana Dele Alli wa Tottenham Hotspur ameizoa tena kwa Msimu wa Pili mfululizo.
Akiongelea ushindi wa Tuzo hii, Kante alisema: "Ni heshima kubwa mno kuchaguliwa na Wachezaji wengine!"

×××××××××

MJUE KANTE:

KUZALIWA: Paris, France

UMRI: Miaka 26

KLABU ALIZOCHEZA: Boulogne (2011-13), Caen (2013-15), Leicester (2015-16), Chelsea (2016-)

MATAJI: EPL 2015/16

×××××××××

Hivi sasa Kante yuko mbioni kutwaa Ubingwa wa England akiwa na Chelsea ambao ndio Vinara wa EPL, Ligi Kuu England, baada ya Msimu uliopita kutwaa Ubingwa huo akiwa na Leicester City.Kante anaweza kuweka Rekodi ya kuwa Mchezaji wa Kwanza kutwaa Ubingwa wa England Misimu Miwili mfululizo akiwa na Klabu Mbili tofauti ikiwa Chelsea itafanya vyema Mechi zake 6 zilizobaki.

EMIRATES FA CUP: LEO NANI KUUNGANA NA CHELSEA FAINALI, ARSENAL AU CITY?

EMIRATES-FACUP-2017-SIT-1LEO WEMBLEY STADIUM itazikutanisha Arsenal na Manchester City kuwania nafasi ya kucheza Fainali ya EMIRATES CUP hapo Mei 27 dhidi ya Chelsea ambayo Jana iliitoa Tottenham Hotspur 4-2 kwenye Nusu Fainali ya Kwanza.
Mechi hii inazikutanisha Timu ambazo zilianza Msimu kwa matarajio makubwa lakini hadi sasa Msimu wao wote umebaki kwenye hii FA CUP baada kupoteza mwelekeo kwenye Ligi Kuu England na pia kutupwa nje ya UEFA CHAMPIONZ LIGI na hata kulikosa Kombe la Ligi, EFL CUP, ambalo limebebwa na Man United.
Tayari Meneja wa Man City Pep Guardiola
ameshaungama kuwa Wamiliki wa Klabu hiyo hawatakuwa na furaha hata wakitwaa FA CUP.
Kwa Arsene Wenger kutwaa FA CUP ni jambo la kufa na kupona kwani Mashabiki wa Arsenal wamemsakama sana Msimu huu wakitaka ang'oke.
Kwenye Ligi Msimu huu City iliifunga Arsenal Mwezi Desemba na mapema Mwezi huu kutoka Sare.

+++++++++++++++++++

JE WAJUA?

-FA CUP 2016/17, ambalo pia hujulikana kama FA Challenge Cup, ni mara ya 136 kushindaniwa kila Mwaka tangu lilipoanzishwe na linatambuliwa kama ndio Mashindano ya kale kupita yote Duniani.

-Kombe hili linadhaminiwa na Kampuni ya Ndege ya Emirates na kwa sababu za kiudhamini linaitwa Emirates FA Cup.

-Timu 736 zilikubaliwa kushiriki Mashindano haya Msimu huu na yalianza kwa Raundi ya Awali na yatafikia Tamati kwa Fainali itakayochezwa Uwanjani Wembley Jijini London hapo Mei 27, 2017.

-Mshindi wa FA CUP ataingizwa Hatua ya Makundi ya UEFA EUROPA LIGI Msimu wa 2017/18.

KUANZIA MSIMU HUU – KUANZIA Robo Fainali:

-Hamna Marudiano ikiwa Timu zipo Sare baada ya Dakika 90. Sare itafuatia Dakika za Nyongeza 30 na kama Gemu bado Sare, zitafuatia Penati ili kupata Mshindi.

-Kila Timu inaruhusiwa kubadili Wachezaji si zaidi ya Wanne lakini huyo wa Nne ni pale tu Gemu ipo Dakika za Nyonfeza 30.

+++++++++++++++++++

Kwenye Mechi hii Arsenal inaweza kumkosa Danny Welbeck mwenye tatizo la Kidole cha Mguu huku Majeruhi wao waliothibitika ni Mustafi, Ospina, Pérez, Cazorla na Reine-Adélaïde.
Kwa upande wa City Majeruhi ni Jesus, Stones, Sagna na Gündogan. 
USO KWA USO:
ARSENAL - Ushindi 96
SARE - 45
MAN CITY - Ushindi 50
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA: 
ARSENAL: Cech, Gabriel, Koscielny, Holding, Ox-Chamberlain, Ramsey, Xhaka, Monreal, Sanchez, Giroud, Ozil
MAN CITY: Caballero, Navas, Kompany, Otamendi, Clichy, Fernandinho, De Bruyne, Sterling, Silva, Sane, Aguero
REFA: Craig Pawson
FA CUP

Ratiba

Nusu Fainali

**Saa za Bongo

Jumapili Aprili 23

1700 Arsenal v Man City

DROO MECHI ZA NUSU FAINALI UEFA CHAMPIONZ LIGI NA EUROPA LIGI IJUMAA!

=KUZAA EL DERBI MADRILENO REAL v ATLETICO?
DROO-UEFA-SITDROO za kupanga Mechi za Mashindano ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, na UEFA EUROPA LIGI zitafanyika Ijumaa Aprili 21 huko Nyon, Uswisi kwenye Makao Makuu ya UEFA.
Tayari Timu zilizotinga Nusu Fainali za UCL zilikamilka hapo Jana wakati 4 za EUROPA LIGI zitajulikana baadae Usiku wa Leo baada kukamilika Mechi 4 za Pili za Robo Fainali.
Kwenye Mechi hizo za Robo Fainali Man United watacheza na RSC Anderlecht (Mechi ya Kwanza 1-1), KRC Genk kuivaa Celta Vigo (2-3), Schalke na Ajax (0-2) na Besiktas kucheza na Lyon (1-2).
Kwenye Chungu cha Droo ya UCL Timu 4 ambazo zimo humo ni Mabingwa Watetezi Real Madrid, Atletico Madrid, Juventus na AS Monaco.
Droo hii haibagui Timu za Nchi moja na hivyo upo uwezekano wa kuwepo El Derbi Madrileno kwa Mahasimu Real na Atletico kupambanishwa.
Droo hizi 2, zile za UCL na EUROPA LIGI, zitaanza Saa 7 Mchana.
Mechi za Nusu Fainali za UCL zitachezwa Mei 2 na 3 na Marudiano Wiki 1 baadae hapo Mei 9 na 10 huku Fainali ikichezwa Cardiff, Wales Juni 3.
Mechi za Nusu Fainali za EUROPA LIGI zitachezwa Alhamisi Mei 4 na kurudiana ni Mei 11.
Fainali ni huko Stockholm, Sweden hapo Mei 24.

LEO BARCELONA INAHITAJI UFANISI WA JUU KUPINDUA 3-0 ZA JUVENTUS - INIESTA

UEFA CHAMPIONZ LIGI

Robo Fainali

Marudiano

***Mechi zote kuanza Saa 3 Dak 45 Usiku

Jumatano Aprili 19

**Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza

Barcelona v Juventus [0-3]

Monaco v Borussia Dortmund [3-2]

++++++++++++++++++++++++++++

UCL-16-17-SITKIUNGO MKONGWE wa Barcelona Andres Iniesta amekiri itakuwa ngumu mno lakini si kitu kisichowezekana kuiga walichowatenda PSG kwa Juventus ambao wanarudiana nao Leo Usiku huko Nou Camp Jijini Barcelona Nchini Spain.
Kwenye Mechi ya kwanza ya Robo Fainali ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, iliyochezwa huko Turin, Italy, Juve waliichapa Barca 3-0.
Lakini katika Raundi iliyopita ya UCL Barca walijikuta kwenye hali kama hii walipotwangwa na PSG 4-0 katika Mechi ya kwanza iliyochezwa huko Paris lakini kwenye Marudiano huko Nou Camp Barca walishusha ngoma kali na kuichabanga PSG 6-1 na wao kusonga kwa Jumla ya Bao 6-5.
Iniesta ameeleza: "Kuna vingi vinafanana kwenye Gemu hii na ile ya PSG. Tunatakiwa tuwe na fikra zilezile tangu Dakika ya kwanza. Ni ngumu kuleta miujiza mingine lakini inawezekana. Lazima tutengeneze nafasi nyingi na kucheza Gemu bora kupita yeyote Msimu huu!"
Ameongeza: "Goli la mapema litatupa nguvu lakini lazima tuwe wavumilivu. Tusipopata Goli tutulie tusiweweseke. Nadhani Juve wamefungwa Bao 2 au 3 Msimu huu wa UCL!"