ENGLAND-RATIBA MSIMU MPYA 2017/18: BIGI MECHI, DABI, PATA TAREHE ZAKE!

LEO EPL, LIGI KUU ENGLAND, imefyatua Ratiba yake ya Msimu Mpya wa 2017/18 wa Ligi hiyo ambayo itaanza Agosti 12 na kumalizika Mei 13 Mwakani.

EPL-17-18-SITKabla kuanza kwa Ligi, kutakuwa Mechi ya Kufungua Pazia Msimu ya kugombea Ngao ya Jamii kati ya Mabingwa Chelsea na waliobeba FA CUP, Arsenal, ambayo itachezwa Uwanja wa Wembley Jijini London hapo Agosti 6.

Wadau wengi wana hamu ya kujua Bigi Mechi, Dabi na baadhi ya Mechi za Mvuto zimepangwa lini.

Hapa chini tunakuletea Tarehe ya Mechi hizo zikiwemo Dabi ya London Kaskazini, Dabi ya Merseyside na Dabi ya Manchester.

FAHAMU: Baadhi ya Tarehe ya Mechi hizi zinaweza kubadilishwa kukidhi mahitaji ya Stesheni za TV kurusha Matangazo yao Mubashara kwa zile zenye Haki hizo.

2017

19/08/17: Tottenham v Chelsea

26/08/17: Liverpool v Arsenal & Chelsea v Everton

09/09/17: Everton v Tottenham & Man City v Liverpool

16/09/17: Chelsea v Arsenal & Man United v Everton

23/09/17: West Ham v Tottenham

30/09/17: Chelsea v Man City

14/10/17: Liverpool v Man United

21/10/17: Everton v Arsenal & Tottenham v Liverpool

28/10/17: Man United v Tottenham

04/11/17: Chelsea v Man United & Man City v Arsenal

18/11/17: Arsenal v Tottenham

25/11/17: Liverpool v Chelsea

28/11/17: Brighton v Crystal Palace

02/12/17: Arsenal v Man United

09/12/17: Liverpool v Everton, Man United v Man City & West Ham v Chelsea

12/12/17: West Ham v Arsenal

16/12/17: Man City v Tottenham

23/12/17: Arsenal v Liverpool & Everton v Chelsea

30/12/17: Tottenham v West Ham

2018

01/01/18: Arsenal v Chelsea

01/01/18: Everton v Man United

13/01/18: Liverpool v Man City & Tottenham v Everton

31/01/18: Tottenham v Man United

03/02/18: Liverpool v Tottenham

10/02/18: Tottenham v Arsenal

24/02/18: Arsenal v Man City

24/02/18: Man United v Chelsea

03/03/18: Man City v Chelsea

10/03/18: Man United v Liverpool

31/03/18: Chelsea v Tottenham & Everton v Man City

07/04/18: Chelsea v West ham, Everton v Liverpool & Man City v Man United

14/04/18: Tottenham v Man City & Crystal Palace v Brighton

21/04/18: Arsenal v West Ham

28/04/18: Man United v Arsenal

05/05/18: Chelsea v Liverpool

 

UKIMYA WA JAMES ‘BOND’ RODRIGUEZ.....NI DALILI KUTUA CHELSEA?

JAMES-RODRIGUEZHIVI sasa yupo Vakesheni, lakini James Rodriguez, Jina la Utani James Bond, anatafakari nini hatima yake huku akimaliza Msimu bila kunena lolote kwa wenzake wa Real Madrid n ahata Bodi ya Klabu.

Hadi sasa, si Mchezaji mwenyewe, wala Wakala wake Jorge Mendes, aliefunguka nini kitajiri licha kuwepo na minong’ono mingi kuhama kwake kutoka Real.

Hata Kocha Zinedine Zidane amefunga Ofisi nae kwenda Vakesheni hajatamka lololote kuhusu Rodriguez mbali ya kutaka Kikosi chake kilichotwaa Ubingwa La Liga na Ulaya kubaki vile vile.

Hata hivyo, Klabu ya Real imeliweka Dau la anaemtaka Rodriguez kuwa wazi na nalo ni EURO Milioni 75.

Dau hilo limekausha nia ya Klabu nyingi Ulaya kuingia mbioni kumsakaingawa duru za ndani ya Real Madrid zimedokeza kuwa ni Mabingwa wa England pekee, Chelsea, ndio wameonyesha nia ya kumnunua.

MAN UNITED WAAFIKIANA NA BENFICA DILI KUMSAINI VICTOR LINDELOF!

VICTOR-LINDELOFManchester United wamukubalina na Klabu ya Portugal Benfica dili ya Pauni Milioni 31 kumsaini Beki wa Kimataifa wa Sweden Victor Lindelof.

Lindelof, mwenye Miaka 22, hivi sasa yupo na Kikosi cha Sweden ambacho Ijumaa kiliifunga France 2-1 katika Mechi ya Kundi lao ya kusaka kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 zitakazochezwa Russia.

Lindelof ameichezea Timu ya Taifa ya Sweden mara 12.

Beki huyo, ambae hucheza kama Sentahafu na pia Beki wa Kulia, amekuwa na Benfica tangu Mwaka 2012 na Msimu uliopita aliichezea Benfica mara 47 na kuwasaidia kutwaa Mataji Dabo yaani Ubingwa na Kombe la FA la Portugal.

Huyu anakuwa Mchezaji wa Kwanza kusainiwa na Man United kuelekea Msimu Mpya wa 2017/18 utakaoanza Agosti 12.

Habari za Dili hii pia zimethibitishwa na Tovuti rasmi ya Man United ambayo imeeleza Dili hii itakamilika baada ya Lindelof kupimwa Afya, kupata Kibali cha Kimataifa na kuafikiana na Maslahi yake binafsi.

IBRAHIMOVIC RUKSA KWENDA, SHAKESPEARE MENEJA KUDUMU LEICESTER, KIPA EDERSON ASAINI CITY KWA £35M TOKA BENFICA!

PATA FUPI ZILIZOBAMBA:

IBRAHIMOVIC RUKSA KWENDA,

IBRA-UELManchester United wanatarajiwa kutompa Straika wao Zlatan Ibrahimovic Mkataba Mpya baada wa sasa kwisha hapo Juni 30.

Straika huyo toka Sweden mwenye Miaka 35 alisaini Mkataba wa Mwaka Mmoja wenye Nyongeza ya Mwaka Mmoja wakiafikiana, mwanzoni mwa Msimu uliopita.

Lakini Nyongeza hiyo imeshindwa kutumika baada Ya Mwezi Aprili Ibrahimovic kuumia vibaya Goti lake ambalo litamweka nje kwa muda mrefu.

Leo EPL, LIGI KUU ENGLAND, inatarajiwa kutoa Listi ya Wachezaji wa Klabu zote za Ligi hiyo ambayo itaanika nani watabakia kwenye Timu zao na nani wataondoka.

Hivyo hili la Ibrahimovic litathibitika hii Leo.

Akiwa na Man United, Ibrahimovic alicheza Mechi 46 na kufunga Bao 28 akiwasaidia mno kubeba Ngao ya Jamii, LEICESTER-SHAKESPEAREEFL CUP na UEFA EUROPA LIGI katika Msimu wa Kwanza tu wa Meneja Jose Mourinho.

SHAKESPEARE MENEJA WA KUDUMU LEICESTER!

Meneja wa Muda wa Leicester City, Craig Shakespeare, amepewa Mkataba wa Kudumu na Mabingwa hao wa zamani wa England ambao ni wa Miaka Mitatu.

Shakespeare, mwenye Miaka 53, aliteuliwa Meneja wa Muda Mwezi Februari baada ya kufukuzwa Claudio Ranieri.

Hiki ndicho kitakuwa kibarua cha kwanza kwake kama Meneja kamili baada ya kufanya kazi kama Msaidizi wa Meneja chini ya Ranieri na kabla chini ya Meneja aliepita hapo Leicester, Nigel Pearson.

Tangu ashike hatamu hapo Leicester, Shakespeare alishinda Mechi 8 kati ya 16 na kuwawezesha kuwa Timu pekee ya England kutinga Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI kabla CITY-EDERSON-DUNIAkutolewa na Atletico Madrid Mwezi Aprili.

KIPA EDERSON MORAES ASAINI CITY KWA £35M TOKA BENFICA!

Manchester City rasmi imemsaini Kipa Ederson Moraes kwa Dau la Pauni Milioni 35 kutoka Klabu ya Portugal Benfica.

Ederson, Mbrazil mwenye Miaka 23, alianza kuichezea Timu ya Kwanza ya Benfica Mwezi Machi na kuwasaidia kubeba Ubingwa na Kombe la FA Msimu ulioisha Mei.

Ederson atatambulika rasmi kama Mchezaji wa City kuanzia Julai Mosi.

Dau hili la kumnunua Ederson limevunja Rekodi ya Dunia kwa Bei ya Kipa ambalo liliwekwa Mwaka 2001 wakati Juventus ikimnunua kutoka Parma Gianluigi Buffon.

Habari hizi za Kipa huyo kusaini City pia zimethibitishwa Jana na Benfica ambao pia wametoboa kuwa Dau la kumnunua Kipa huyo Mgao wake wa Asilimia 50 utakwenda ‘Upande wa Tatu’ kitu ambacho ni tata kwa FIFA n ahata FA, Chama cha Soka England ambao Kanuni zao wanataka Mchezaji amelimikiwe na Klabu na si Klabu na ‘Upande wa Tatu’.

Hilo sasa litafanya FA, na EPL, Ligi Kuu England, wapitie Uhamisho huu na kujiridhisha unakidhi Kanuni zao na ndipo wauthibitishe.

GIROUD ATAFAKARI KUNG'OKA ARSENAL KWA KUSAGA BENCHI!

GIROUDBAADA kuanzia Benchi mara 23 na baadae kuingizwa kucheza Msimu uliokwisha Mei, Straika wa France Olivier Giroud sasa anatafakari kuondoka Arsenal.

Giroud, mwenye Miaka 30, alianza Mechi 11 tu Msimu uliopita licha kufunga Bao 12 na kujikuta mara nyingi akipigwa Benchi huku Meneja Arsene Wenger akimpanga Alexis Sanchez na pia Danny Welbeck.

Sasa Giroud, ambae ndie aliesuka Bao la ushindi alilofunga Aaron Ramsey na kuwabebesha FA CUP Wiki 2 zilizopita, anahisi sasa ni wakati sahihi kuangalia hatima yake.

Ameeleza: "Nitaongea na Wenger. Sikupata nafasi nyingi kucheza lakini utafika wakati kuna vitu sitakubali na hasa Mwaka mwingine wa kucheza Mechi chache."

Giroud pia ameeleza atakaa chini na Familia yake na Washauri wake kutafakari maamuzi yoyote yale.

Hata hivyo, Straika huyo amedokeza kuwa bado ana Miaka Mitatu ya Mkataba na Arsenal na angependa zaidi kutwaa Ubingwa wa England na Klabu hiyo.

Habari MotoMotoZ