UEFA CHAMPIONZ LIGI: DIMBANI JUMANNE NA JUMATANO, 11 ZAWEZA KUFUZU ZIKIWA NA MECHI 2 MKONONI!

>>ZIMO ARSENAL, BARCA, PSG, REAL….

UCL-2016-17-1-1UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, Jumanne Novemba 1 na Jumatano Novemba 2 inaingia Mechi zake za 4 za Makundi na kubakisha Mechi 2 na zipo Timu 11 ambazo zinaweza kufuzu Wiki hii ikiwa matokeo yatawapendelea.

Timu hizo 11 ambazo zinaweza kufuzu zikibakisha Mechi 2 ni:

Arsenal, Paris Saint-Germain, Napoli, Barcelona, Atlético Madrid, Bayern München, Borussia Dortmund, Real Madrid, Leciester, Juventus na Sevilla.

FUATILIA MAHESABU YAKE ILI 11 HIZO ZIWEZE KUFUZU WIKI HII:

Jumanne Novemba 1

KUNDI A: Ludogorets Razgrad (Pointi 1) v Arsenal (7), Basel (1) v Paris Saint-Germain (7)

-Ikiwa Arsenal au PSG itashinda na mwingine kutofungwa basi Timu zote 2 zitafuzu.

KUNDI B: Beşiktaş (5) v Napoli (6), Benfica (4) v Dynamo Kyiv (1)

-Napoli watasonga wakishinda na ikiwa Gemu nyingine ni Sare basi Benfica na Besiktas haziwezi kuipita Napoli hata kama zote hizo zitapata Pointi 9.

-Ikiwa Dynamo watafungwa na Gemu nyingine ni Sare, Dynamo watatupwa nje ya UCL.

KUNDI C: Manchester City (4) v Barcelona (9), Borussia Mönchengladbach (3) v Celtic (1)

-Ikiwa Barca watatoka Sare watafuzu na wakishinda huku Mönchengladbach wasishinde

basi Barca watatwaa Nafasi ya Kwanza ya Kundi.

-Ikiwa Celtic watafungwa na City hawafungwi basi Celtic hawawezi kumaliza nafasi 2 za juu za Kundi.

KUNDI D: Atlético Madrid (9) v Rostov (1), PSV Eindhoven (1) v Bayern München (6)

-Ikiwa Atletico watashinda watakuwa wamefuzu.

-Ikiwa Bayern watashinda na Gemu nyingine kuwa Sare au Atletico kushinda basi Bayern watafuzu.

-Ikiwa watafungwa, PSV hawawezi kumaliza kwenye 2 Bora za Kundi.

Jumatano Novemba 2

KUNDI E: Monaco (5) v CSKA Moskva (2), Tottenham Hotspur (4) v Bayer Leverkusen (3)

-Hakuna Timu inayoweza kufuzu Wiki hii.

KUNDI F: Borussia Dortmund (7) v Sporting CP (3), Legia Warszawa (0) v Real Madrid (7)

-Ikiwa Dortmund watashinda, watafuzu.

-Real watafuzu kwa ushindi ikiwa pia Dortmund watashinda.

-Ikiwa Legia watafungwa hawawezi kumaliza ndani ya 2 Bora za Kundi na wakitoka Sare itabidi waombee Dortmund ifungwe ili wabaki kwenye kinyang’anyiro.

KUNDI G: FC København (4) v Leicester City (9), Porto (4) v Club Brugge (0)

-Leicester watafuzu kwa ushindi na kutwaa Nafasi ya Kwanza ikiwa Porto hawashindi.

-Sare kwa Leicester itawatosha kufuzu ikiwa Porto hawashindi.

-Brugge watatupwa nje wakifungwa au wakitoka Sare na FC København kushinda.

KUNDI H: Juventus (7) v Lyon (3), Sevilla (7) v Dinamo Zagreb (0)

 -Ikiwa Juve watashinda watafuzu.

-Sevilla watasonga wakishinda ili mradi Juve nao washinde.

-Ikiwa Dinamo watafungwa hawataweza kumaliza ndani ya 2 Bora ya Kundi na wakitoka Sare inabidi waombee Juve ifungwe.

UEFA CHAMPIONZ LIGI

Ratiba

Mechi za 4 za Makundi

**Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku, Bongo Taimu [Isipokuwa inapotajwa]

Jumanne Novemba 1

KUNDI A

Basel v Paris St Germain                 

Ludogorets Razgrad v Arsenal                  

KUNDI B

2045 Besiktas v Napoli          

Benfica v Dynamo Kiev          

KUNDI C

Borussia Monchengladbach v Celtic         

Man City v Barcelona   

KUNDI D

Atletico Madrid v FC Rostov            

PSV Eindhoven v Bayern Munich     

Jumatano Novemba 2

KUNDI E

Monaco v CSKA   

Tottenham v Bayer Leverkusen                

KUNDI F

Borussia Dortmund v Sporting                  

Legia Warsaw v Real Madrid           

KUNDI G

FC Copenhagen v Leicester             

FC Porto v Club Brugge          

KUNDI H

Juventus v Lyon            

Sevilla v Dinamo Zagreb        

TAREHE MUHIMU:

MECHI ZA MAKUNDI:

Mechi ya Kwanza: 13 na 14 Septemba

Mechi ya Pili: 27 na 28 Septemba

Mechi ya Tatu: 18 na 19 Oktoba

Mechi ya Nne: 1 na 2 Novemba

Mechi ya Sita: 22 na 23 Novemba

Mechi ya Sita: 6 na 7 Desemba

MECHI ZA MTOANO:

11–12/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Kwanza

18–19/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Pili

02–03/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Kwanza

09–10/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Pili

03/06/17: Fainali (National Stadium of Wales, Cardiff)

LA LIGA: RAFINHA AIPA BARCA USHINDI MWEMBAMBA DHIDI YA TIMU YA MKIANI!

BARCA-SHANGILIA-1KIUNGO wa Barcelona Rafinha Alcantara 
Jana alufungia Timu yake Bao la aDakika ya 49 na kuipa ushindi wa 1-0 dhidi ya Timu ta mkiani ya La Liga Granada.
Ushindi huo umeipandisha Barca hadi Nafasi ya Pili wakiwa Pointi 2 nyuma ya Vinara Real Madrid ambao Jana walifunga Ugenini Alaves 4-1 huku Cristiano Ronaldo akipiga Hetitriki.
Wakicheza chini ya kiwango huku Mafowadi wao hatari, Lionel Messi, Neymar na Luis Suarez, wakihaha bila tija, Barca walishindwa kuifunga Timu hiyo ya mkiani.
LA LIGA
Ratiba/Matokeo:
**Saa za Bongo
Ijumaa Oktoba 28
CD Leganes 0 Real Sociedad 2
Jumamosi Oktoba 29
Sporting Gijon 1 Sevilla FC 1
Deportivo Alaves 1 Real Madrid CF 4
Atletico de Madrid 4 Malaga CF 2
FC Barcelona 1 Granada CF 0
Jumapili Oktobo 30
1400 SD Eibar v Villarreal CF
1815 Athletic de Bilbao v Osasuna
2030 Real Betis v RCD Espanyol
2245 Las Palmas v Celta de Vigo
Jumapili Oktoba 30
2245 Deportivo La Coruna v Valencia C.F

EPL: ARSENAL WAITANDIKA ‘MKIANI’ SUNDERLAND NA KUKAA KILELENI!

EPL - LIGI KUU ENGLAND

Jumamosi Oktoba 29

Ratiba/Matokeo:

**Saa za Bongo

Sunderland 4 Arsenal 1              

1700 Man United v Burnley

1700 Middlesbrough v Bournemouth                

1700 Tottenham v Leicester        

1700 Watford v Hull

1700 West Brom v Man City       

1930 Crystal Palace v Liverpool             

++++++++++++++++++++++++++++++++

SUN-ARSEArsenal wakicheza Ugenini huko Stadium of Light kwenye Mechi yakwanza ya EPL, Ligi Kuu England, hii Leo waliitandika Timu ya Mkiani Sunderland Bao 4-1 na kutwaa uongozi wa Ligi hiyo wakiiacha Sunderland ikiwa mkiani.

Uongozi huu wa Arsenal huenda ukadumu hadi Mechi ya Manchester City ambao wakishinda zaidi ya Bao 3 dhidi ya West Bromwich Albion watatwaa tena uongozi wa EPL.

Arsenal walifunga Bao lao la kwanza Dakika ya 19 kwa Krosi ya Oxlade-Chamberlain kuunganishwa kwa Kichwa na Alexis Sanchez.EPL-OKT29B

Bao hilo lilidumu hadi Mapumziko.

Kipindi cha Pili Krosi ndefu ya Ndong wa Sunderland ilimkuta Watmore aliemhadaa Sentahafu Mustafi na kumzunguka Kipa Cech ambae alimwangusha Watmore na Refa Atkinson kutoa Penati iliyofungwa na Jermaine Defoe katika Dakika ya 65.

Dakika ya 70, Arsene Wenger aliamua kumtoa Alex Iwobi na kumwingiza Olivier Giroud ambae alifunga Bao 2 Dakika za 71 na 75.

Arsenal walifunga Bao lao la 4 Dakika ya 78 kupitia Alexis Sanchez.

VIKOSI:

Sunderland (Mfumo 4-3-3): Pickford, Jones, Kone, O’Shea [Djilobodji, 42'], Van Aanholt. Rodwell, Ndong, Pienaar [Januzaj, 70'], Watmore [Gooch, 84'], Defoe, Khazri.

Akiba: Mika, Djilobodji, Manquillo, Love, Gooch, Januzaj, Anichebe.

Arsenal (Mfumo 4-2-3-1): Cech, Bellerin, Mustafi, Koscielny, Gibbs; Coquelin [Maitland-Niles, 89'], Elneny; Oxlade-Chamberlain [Ramsey,77’], Ozil, Iwobi [Giroud, 69'], Alexis.

Akiba: Ospina, Gabriel, Holding, Jenkinson, Ramsey, Giroud, Maitland-Niles.

REFA: Martin Atkinson

EPL - LIGI KUU ENGLAND

**Saa za Bongo

Jumapili Oktoba 30

1630 Everton v West Ham 

1900 Southampton v Chelsea                

Jumatatu Oktoba 31

2300 Stoke v Swansea                

         

ROONEY – KUNG’OKA MAN UNITED: MOURINHO ASISITIZA HAENDI POPOTE!

MANUNITED-ROONEY-MOUMAPEMA Jana huko England kuliibuka stori kuwa Kepteni wa Manchester United Wayne Rooney yupo mbioni kurejea Klabu yake ya zamani Everton huku Meneja wa Klabu hiyo Ronald Koeman ‘akimkaribisha’, lakini baadae hiyo Jana Meneja wa Man United Jose Mourinho amesisitiza Kepteni huyo haendi popote.

Kwa mara ya kwanza tangu atinge Soka la juu akiwa na Umri wa Miaka 16, hivi sasa Rooney hana namba ya kudumu huko Man United na hata Timu ya Taifa ya England ambayo yeye ni Nahodha pia.

Rooney amezikosa Mechi 2 za Man United akiwa na maumivu ya Musuli za Mguu lakini katika Mechi 5 kati ya 7 zilizopita za kabla ya hapo kwa Man United na England, Rooney alianzia Benchi.

Hali hiyo imefanya Magazeti yaandike kila aina ya habari kuhusu Rooney, ambae Jumatatu iliyopita alitimiza Miaka 31, na Wiki hii kukavuja habari kuwa Mourinho amemwambia Rooney anaweza kuhama ikiwa atataka namba ya kudumu Kikosini.

Lakini Jana, kuelekea Mechi yao ya EPL, Ligi Kuu England, dhidi ya Burnley Uwanjani Old Trafford Jumamosi, Mourinho amesisitiza stori zote kuhusu Rooney ni uongo na kuviponda sana Vyombo vya Habari vinavyozitengeneza.

Kuhusu Umri kumtupa mkono Rooney, Mourinho amesisitiza Mchezaji huyo bado ni Staa wa kiwango cha juu na ni muhimu kwa Timu yao.

Mourinho ametamka: “Ninachoweza kusema yeye ni Mchezaji mzuri sana, Mchezaji muhimu mno kwetu, haendi popote. Tunampenda, Anatupenda!”

Aliongeza: “Yeye ni Kepteni wangu. Kepteni wa Timu. Ni kiongozi!”

EPL - LIGI KUU ENGLAND

**Saa za Bongo

Jumamosi Oktoba 29

1430 Sunderland v Arsenal         

1700 Man United v Burnley

1700 Middlesbrough v Bournemouth                

1700 Tottenham v Leicester        

1700 Watford v Hull

1700 West Brom v Man City       

1930 Crystal Palace v Liverpool             

Jumapili Oktoba 30

1630 Everton v West Ham 

1900 Southampton v Chelsea                

Jumatatu Oktoba 31

2300 Stoke v Swansea      

GOIGOI KUWA NGANGARI: MOURINHO AWAPA CHANGAMOTO WACHEZAJI MANCHESTER UNITED

MOU-CARRINGTONBAADA ya kubondwa 4-0 huko Stamford Bridge na Chelsea kwenye EPL, Ligi Kuu England, Juzi Jumapili, Manchester United sasa wanarudi kwao Old Trafford kujikusanya upya ili kuwavaa Mahasimu wao wakubwa Man City Jumatano kwenye Mechi ya Raundi ya 4 ya EFL CUP.
Kuelekea kwenye Dabi hii ya Jiji la Manchester, Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho, amewataka Wachezaji wake kujibu mapigo na kuonyesha wao ni ‘Wanaume’.
Akiongea na MUTV, Kituo cha TV cha Man United, Mourinho ameeleza: “Ningependelea tucheze kwenye EPL. Tuna usongo na Ligi. Imetuweka hapa lakini pengo na Vinara ni Pointi 6.”
Amesema: “Tumekuwa na Mechi ngumu mfululizo. Tumepoteza Pointi Wikiendi hii na hata ile Mechi tulicheza na Stoke tulicheza vizuri na kupoteza Pointi kwa Droo ya 1-1. Sasa tunahitaji kushinda Mechi!”
Aliongeza: “Sisemi ni Mechi rahisi lakini sasa tuna Mechi na Burnley, tunao Swansea, West Ham, Sunderland, Middlesbrough…tunahitaji kushinda hizi!”
Mourinho alifafanua: “Timu 4 za juu, au 5 za juu, inabidi zicheze zenyewe kwa zenyewe kama sisi tulipocheza na Chelsea na Liverpool. Watapoteza Pointi, kwa hiyo bado tupo kwenye mbio za Ubingwa lakini hatuna pa kujificha!”
Alimalizia: “Tunasikitika sana sana lakini haya si ya Watoto, haya ni kwa Wanaume…lazima tuwe Wanaume na kuifanyia kazi Mechi ijayo!”

Habari MotoMotoZ