UEFA CHAMPIONZ LIGI – ROBO FAINALI: JUVE YAIPIGA BARCA 3-0!

>MILIPUKO YAAHIRISHA MECHI DORTMUND NA MONACO, SASA KUCHEZWA LEO!

UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI

Robo Fainali

Jumanne Aprili 11

Juventus 3 Barcelona 0

Borussia Dortmund v Monaco [Mechi imeahirishwa kwa Dharura ya Milipuko]

++++++++++++++++++++++++++++

JUVE-JUU-BARCAMechi za Robo Fainali za UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, zimeanza kuchezwa lakini ni moja tu iliyochezwa Jumanne Usiku baada ya ile ya kule Jijini Dortmund, Germany kati ya Borussia Dortmund na AS Monaco kulazimika kuahirishwa kutokana na Mlipuko karibu na Basi lambalo lilibeba Wachezaji wa Timu ya Dortmund wakiwa Hotelini na kujeruhi.

Mechi nyingine ilichezwa kama ilivyopangwa huko Turin, Italy Uwanjani Juventus Stadium na Wenyeji Juventus kuanza vyema mno kwa kuitandika Barcelona 3-0.

Matokeo ya Mechi hii yamekumbusha nini kiliwatokea Barca katika Raundi iliyopita kwani walichapwa 4-0 na PSG huko Paris lakini waliporudiana huko Nou Camp Jijini Barcelona, Barcelona wakaibuka kidedea kwa kushinda 6-1.

Sasa na Robo Fainali hii kwao inahitaji miujiza kama hiyo ili watinge Nusu Fainali.

Hapo Jana Juve walikwenda Bao 2 mbele kwa Bao za Paulo Dybala za Dakika za 7 na 22 na Beki Giorgio Chiellini kufungwa kwa Kichwa Kipindi cha Pili Dakika ya 55.

Kutoka huko Jijini Dortmund, Taarifa zimedai Milipuko Matatu ilitokea karibu na Basi hilo ambalo lilitakiwa kuwasafirisha Wachezaji wa Dortmund kwenda Uwanjani Signal Iduna Park na kumjeruhi Mchezaji mmoja, Marc Bartra, aliekimbizwa Hospitalini baada ya kukatwa Mkononi.

UEFA imesema Mechi hii itachezwa Jumatano.

VIKOSI:

Juventus: Buffon, Dani Alves, Bonucci, Chiellini, Alex Sandro, Pjanic, Khedira, Cuadrado, Dybala, Mandzukic, Higuain.

Akiba: Neto, Marchisio, Barzagli, Lemina, Asamoah, Lichtsteiner, Rincon. 

Barcelona: ter Stegen, Sergi Roberto, Pique, Umtiti, Mathieu, Rakitic, Mascherano, Iniesta, Messi, Luis Suarez, Neymar.

Akiba: Cillessen, Denis Suarez, Alcacer, Jordi Alba, Digne, Andre Gomes, Alena. 

REFA: Szymon Marciniak (Poland)

UEFA CHAMPIONZ LIGI

Robo Fainali

***Mechi zote kuanza Saa 3 Dak 45 Usiku

Jumatano Aprili 12

Borussia Dortmund v Monaco

Atletico Madrid v Leicester City

Bayern Munich v Real Madrid

Marudiano

**Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza

Jumanne Aprili 18

Leicester City v Atletico Madrid

Real Madrid v Bayern Munich

Jumatano Aprili 19

Barcelona v Juventus [0-3]

Monaco v Borussia Dortmund

++++++++++++++++++++++++++++

TAREHE MUHIMU:

MECHI ZA MTOANO:

11–12/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Kwanza

18–19/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Pili

02–03/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Kwanza

09–10/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Pili

03/06/17: Fainali (National Stadium of Wales, Cardiff)

 

 

 

KLABU BINGWA ULAYA: LEO ROBO FAINALI JUVE-BARCA, BVB-MONACO!

PATA DONDOO!
UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI
Robo Fainali
***Mechi zote kuanza Saa 3 Dak 45 Usiku
Jumanne Aprili 11
Borussia Dortmund v Monaco
Juventus v Barcelona
×××××××××××××××××××××××××××
UCL-16-17-SITUSIKU huu Mechi 2 za Robo Fainali za kwanza za UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI zitaanza kuchezwa huko Italy na Germany.
PATA DONDOO ZA MECHI HIZO:
JUVENTUS v BARCELONA
Juventus Stadium 
Turin, Italy
Hii ni mara ya 8 kwa Timu hizi kukutana Ulaya na Mwaka 2015 Barca iliichapa Juve 3-1 katika Fainali ya UCL.
Kwenye Mechi hii Barca itamkosa Kiungo wao mahiri Sergio Busquets ambae yupo Kifungoni.
Juve, ambao wako kwenye mbio za kutofungwa Mechi 21 za Ulaya Nyumbani kwao, wanaivaa Barca ambayo haijawahi kuifunga hapo Juventus Stadium.
Mechi zao Wikiendi iliyopita:
Juventus 2 Chievo 0
Malaga 2 Barcelona 0
VIKOSI VINATARAJIWA:
Juventus: Buffon; Dani Alves, Bonucci, Chiellini, Alex Sandro; Pjanić, Khedira; Cuadrado, Dybala, Mandžukić; Higuaín.
WATAKAOKOSA MECHI: Pjaca (Majeruhi)
Barcelona: Ter Stegen; Sergi Roberto, Piqué, Umtiti, Jordi Alba; Rakitić, Mascherano, Iniesta; Messi, Luis Suárez, Neymar
WATAKAOKOSA MECHI: Busquets (Kifungoni), Rafinha (Majeruhi), Aleix Vidal (Majeruhi), Arda Turan (Maheruhi)
BORUSSIA DORTMUND v MONACO
BVB Stadion, Dortmund
Dortmund na Monaco zinakutana kwa mara ya kwanza Ulaya huku Monaco wakitinga bila nguzo yao imara Tiemoué Bakayoko ambae yupo Kifungoni.
Hii itakuwa ni mara ya pili katika Miaka Mitatu kwa Monaco kutinga Robo Fainali ya UCL wakati Dortmund walifika hatua hii Msimu wa 2013/14.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
Dortmund: Bürki; Pisczcek, Papastathopoulos, Bartra, Schmelzer; Weigl; Dembélé, Kagawa, Pulišić, Guerreiro; Aubameyang.
WATAKAOKOSA MECHI: Götze (Mgonjwa), Schürrle (Majeruhi), Durm (Majeruhi)
Monaco: Subašić; Fabinho, Raggi, Glik, Mendy; Moutinho, Bernardo Silva, Lemar; Mbappé, Falcao, Germain.
WATAKAOKOSA MECHI: Bakayoko (Kifungo), Sidibé (Mgonjwa), Boschilia (Majeruhi), Carrillo (Majeruhi)
Mechi zao Wikiendi iliyopita:
Bayern Munich 4-1 Dortmund 
Angers 0-1 Monaco
UEFA CHAMPIONZ LIGI
Robo Fainali
Jumatano Aprili 12
Atletico Madrid v Leicester City
Bayern Munich v Real Madrid
Marudiano
***Mechi zote kuanza Saa 3 Dak 45 Usiku
Jumanne Aprili 18
Leicester City v Atletico Madrid
Real Madrid v Bayern Munich
Jumatano Aprili 19
Barcelona v Juventus
Monaco v Borussia Dortmund

EVERTON YAICHARAZA LEICESTER, YAISHIKA ARSENAL!

=LUKAKU APIGA 2 NDIE MFUNGAJI BORA!
=LEO ARSENAL KUILAZA PALACE NA KUIRUDISHA MAN UNITED YA 6?

EPL – Ligi Kuu England

Matokeo:

Jumapili Aprili 9

Sunderland 0 Manchester United 3                 

Everton 4 Leicester City 2     

+++++++++++++++++++++++++++++++

EVERTON-LUKAKU-GOLIJANA huko Goodison Park Evrrton walitamba kwa kuitandika Leicester City 4-2 huku Straika wao Romelu Lukaku akipiga Bao 2 na kushika hatamu Mfungaji Bora EPL, Ligi Kuu England.
Matokeo haya yameiweka Everton Nafasi ya 7 wakiwa Pointi sawa na Arsenal walio Nafasi ya 6 lakini Arsenal wamecheza Mechi 3 pungufu.
Leo Arsenal wako huko Selhurst Park Jijini London kuivaa Crystal Palace na ushindi kwao utawafanya waishike Man United kwa Pointi na kukalia Nafasi ya 5 kwa Ubora wa Magoli.
Katika Mechi ya Jana Everton walitangulia kufunga Dakika ya Kwanza kupitia Davies na Leicester kujibu kwa Bao 2 za Dakika za 4 na 10 kupitia Slimani na EPL-2Albrighton.
Everton wakacharuka na kutoka nyuma kwa Bao hizo 2-1 na kupiga Bao Dakika za 23 Mfungaji akiwa Lukaku, Dakika ya 41 Jagielka na Lukaku tena Dakika ya 57.
Bao hizo 2 zimemfanya Lukaku awe na Bao 23 za EPL na aongoze kwa Bao 4 mbele ya Straika wa Tottenham Harry Kane katika Listi ya Wafungaji Bora.

EPL – Ligi Kuu England

Ratiba:

Jumatatu Aprili 10

2200 Crystal Palace v Arsenal

Jumamosi Aprili 15

1430 Tottenham Hotspur v Bournemouth                   

1700 Crystal Palace v Leicester City              

1700 Everton v Burnley     

1700 Stoke City v Hull City

1700 Sunderland v West Ham United             

1700 Watford v Swansea City               

1930 Southampton v Manchester City           

Jumapili Aprili 16

1530 West Bromwich Albion v Liverpool 

1800 Manchester United v Chelsea        

Jumatatu

2200 Middlesbrough v Arsenal       


 
 

MOURINHO AKIRI UBUTU, SARE OLD TRAFFORD ZAWATAFUNA!

>ADAI OLD TRAFFORD WAMINYWA MAAMUZI, ‘WAPINZANI DABO DEKA’!

MANUNITED-MOU-REF2HII LEO JOSE MOURINHO ametoa ujumbe tofauti kuhusu Timu yake Manchester United katika Msimu wake wa kwanza Klabuni hapo.

Mourinho amesisitiza wana Rekodi nzuri Uwanja wao wa Nyumbani Old Trafford licha kukaribia Rekodi ya Matokeo mabovu ya Mechi za EPL na pia kukiri kuwa hawako vizuri kwa kushindwa kuzibadili droo 9 walizopata hapo kwao na kuwa ushindi.

Man United wamezoa Pointi 27 kati ya 48 wakiwa Old Trafford Msimu huu.

Wakibakiza Gemu 3 za Nyumbani za EPL Msimu huu, Man United wapo hatarini kuifikia Rekodi mbovu ya Poiinti 27 tu za Nyumbani walizopata Msimu wa 2013/14 chini ya David Moyes aliesimamia Mechi 16 na Ryan Giggs Mechi 3 za mwisho.

Lakini Mourinho amedai wamepoteza Mechi 1 tu hapo Old Trafford na hilo ni jambo jema kwa wakati wa baadae huku pia akilalama kwamba Sare zao nyingi hutokana na Wapinzani ‘Kupaki Basi’ wakitua Old Trafford.

Mourinho ameeleza: “Nadhani licha ya matokeo mabovu, na kwetu Sare ni matokeo mabovu, sisi tupo imara mno Nyumbani. Kwa nini? Tumefungwa Mechi 1 tu na tunajua kwa nini tulifungwa! Kuna vitu vya ajabu vilitokea Mechi hiyo!”

Hata hivyo, Mourinho amekiri ubutu wao wakiwa wamefunga Bao 21 tu katika Mechi 16 za Nyumbani na kutoka Sare na Klabu ambazo walitarajiwa kuzifunga kama vile Stoke, Burnley, Hull, Bournemouth, West Ham na West Brom lakini pia kubanwa na Vigogo Liverpool, Everton na Arsenal.

Mourinho ametamka: “Hatuko safi au wenye nguvu kwa sababu hatushindi, hatuko safi au wenye nguvu kwa sababu hatufungi magoli tunayopaswa kufunga. Tunawapa Wapinzani na Kipa wao Tuzo za Mchezaji Bora wa Mechi mara nyingi tu!”

Aliongeza: “Narudia nlichokisema baada ya Mechi iliyopita, na hii si lawama, lakini maamuzi mengi yametuadhibu sisi, na hivyo naamini tuna nguvu Nyumbani!”

Akimalizia, Mourinho alieleza: “Tukiangalia nini tutakikuta Msimu ujao, nadhani tunajisikia vyema kwamba hatujapoteza Mechi nyingi. Ni kitu kuzuri kuona hatujafungwa katika Mechi 20, Nyumbani na Ugenini, za Ligi. Najua Sare 10 ni Pointi 10, Katika Mechi 10 ukishinda 5 na Kufungwa 5 ni Pointi 15 Nini bora? Pointi 15 lakini ukiangalia mbele ni Bora Mechi 10, Sare 10! Unakuwa ni mgumu, umekakamaa kiakili, ni mgumu kufungwa! Lakini kuwa na Pointi ndio uhalisia, ni bora uwe na Pointi 15 ukishinda Mechi 5 na Kufungwa 5! ”

JESSE LINGARD AVUNA DILI MPYA MANCHESTER UNITED!

>ANENA: ‘NAFURAHIA KUICHEZEA MAN UNITED, MOYO WANGU NI MAN UNITED!’

MANUNITED-LINGARDJESSE LINGARD anasemekana atapewa Dili mpya Klabuni kwake Manchester United ya Mkataba wa Miaka Minne na Mshahara wake kuongezeka mara 3 na kuvuna zaidi ya £100,000 kwa Wiki.

Lingard amebakiza Mwaka Mmoja kwenye Mkataba wake wa hivi sasa na Man United wamekuwa wakitaka abakie kwa muda mrefu zaidi.

Fowadi huyo mwenye Miaka 24 yupo Man United tangu akiwa na Umri wa Miaka 7 na alipewa Mkataba wake wa kwanza kama Profeshenali Mwaka 2011.

Lingard alianza kuchomoza na kubaki Timu ya Kwanza Msimu uliopita chini ya Meneja Louis van Gaal na kabla ya hapo alipelekwa kwa mkopo kwenye Klabu za Leicester City, Birmingham City, Brighton na Derby County.

Kabla habari hizi kuibuka Lingard, ambae ameanza Mechi 3 zilizopita za Man United, alithibitisha yupo mazungumzoni kuongeza Mkataba wake huku yeye akisisitiza angependelea kubakia hapo hapo.

Alieleza: “Nafurahia kuichezea Man United na Moyo wangu ni Man United!”

Lingard amebainisha kuna ushindani mkali kwenye Timu kupata namba lakini pia amekiri hilo ni jambo jema kwa Timu ambalo linakufanya ukipata nafasi basi lazima ujitume.

Amesema: “Ukiwaangalia Mkhitaryan, Zlatan, Pogba, ni Majina makubwa kwenye Timu yetu na ni vyema kuwaiga kwa yale waliyofanikiwa na ni wazi tunapata uzoefu toka kwao hasa kwa Wachezaji Chipukizi!”

Habari MotoMotoZ