UBAGUZI WAMPA KIFUNGO MCHEZAJI MECHI 5, RUFAA YA VARDY YATUPWA SASA NI KIFUNGO MECHI 3!

WAKATI Fowadi wa England anaechezea kwa Mabingwa Leicester City Jamie Vardy akitakiwa kutumikia Kifungo cha Mechi 3 baada ya Rufaa yake kupinga Kadi Nyekundu kutupwa, Kiungo mwingine aliewahi kuichezea England amefungiwa Mechi 5 kwa Ubaguzi Uwanjani.

NJONJO SHELVEY AFUNGIWA MECHI 5 KWA UBAGUZI

NJONJO-MBAGUZIKiungo wa Newcastle Jonjo Shelvey amefungiwa Mechi 5 na kutwangwa Faini ya Pauni 100,000 na FA, Chama cha Soka England baada ya kupatikana na hatia ya kutumia Lugha chafu ya Kibaguzi Uwanjani.

Tukio lilomhukumu Njonjo, ambae alishawahi kukwaruzana na Sir Alex Ferguson Uwanjani kwenye Mechi alipokuwa akiichezea Liverpool walipobamizwa na Manchester United, lilitokea Dakika ya 87 kwenye Mechi ya Newcastle na Wolverhampton Wanderers Jumamosi Septemba 17 alipomkashifu Kiungo kutoka Morocco, Romain Saiss, na Mchezaji mwingine wa Wolves kuliripoti kwa Refa Tim Robinson mara tu baada ya Mechi.

Njonjo amepewa Siku 7 kukata Rufaa ikiwa anapinga Adhabu yake.

VARDY: RUFAA YATUPWA KIFUNGO MECHI 3!

Straika wa Mabingwa wa England Leicester City anaechezea England Jamie Vardy sasa atakosa Mechi 3 baada ya Rufaa yake kupinga Kadi Nyekundu aliyopewa Jumamosi Leicester ikitoka 2-2 na Stoke City kutupiliwa mbali.

Vardy, mwenye Miaka 29, atazikosa Mechi za Leicester dhidi ya Everton, West Ham na Middlesbrough.

Vardy alitolewa nje na Refa Craig Pawson katika Dakika ya 28 kwa Rafu ya Miguu Miwili kwa Straika wa Stoke Mame Diouf.

LEICESTER KUKATA RUFAA NYEKUNDU YA VARDY, ENGLAND NA WASHIRIKA WAKE WATWANGWA FAINI NA FIFA KWA KUVAA UA!

VARDY-REDWAKATI Klabu Bingwa ya England Leicester City ikiwa mbioni kukata Rufaa kupinga Kadi Nyekundu ya Straika wao Jamie Vardy, FIFA imezitwanga Faini FA za England, Scotland, Wales na Northern Ireland kwa kuvaa Utepe wa Maua Mkononi wakati wa Mechi zao Mwezi uliopita.

LEICESTER CITY KUKATA RUFAA KADI NYEKUNDU YA JAMIE VARDY

Leicester City wapo mbioni kukata Rufaa kupinga Kadi Nyekundu ya Straika wao ambae pia anachezea England, Jamie Vardy, aliyopewa Jumamosi wakitoka Droo ya 2-2 na Stoke City.

Vardy alionyeshwa Kadi Nyekundu na Refa Craig Pawson kwa kumrukia Miguu miwili Mame Diouf.

Lakini Leicester inataka kupeleka utetezi kuwa Vardy alisukumwa na ndio maana akatua kwa Miguu Miwili na hakukusudia kutenda hiyo Rafu.

FA, Chama cha Soka cha England, kinatarajiwa kuishushia Leicester Faini kwa vile Refa Pawson aliwapa Kadi za Njano Wachezaji Watano wa Timu hiyo mwishoni mwa Kipindi cha Kwanza na mpaka mwisho wa Mechi hiyo na Stoke Kadi zilishushwa kwa Wachezaji wao 6.

Kanuni za FA zinatamka kuwa Timu inapigwa Faini moja kwa moja ikiwa Wachezaji wao 6 au zaidi watapewa Kadi za Njano.

Miongoni mwa waathirika wa Kadi hizo ni Robert Huth na Christian Fuchs ambao sasa wamelimbikiza Jumla ya Kadi za Njano 5 na sasa watakuwa Kifungoni Mechi 1 na kuikosa Mechi ya Leicester na Everton hapo Desemba 26.

FIFA YAZITWANGA FAINI ENGLAND, SCOTLAND, WALES, NORTHERN IRELAND NA REPUBLIC OF IRELAND!

POPPY-UTEPE

FIFA imevipiga Faini Vyama vya Soka vya England, Scotland, Wales na Northern Ireland baada ya Wachezaji wa Timu zao kuvalishwa Utepe wenye Alama ya Ua Mikononi mwao wakati wa Mechi za Makundi yao ya Nchi za Ulaya ya kufuzu kucheza Fainali za Kombe la POPPYDunia za Mwaka 2018 huko Russia.

England na Sotland zote zilikubaliana Wachezaji wao kuvaa Utepe huo wa Ua wakati wa Mechi yao ya Novemba 11 ya Kundi lao la kuwania kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia kwani Siku hiyo ilikuwa Siku ya Kumbumbu ya Waliokufa Vitani kati Vita Kuu zilizopita.

Siku hiyo, kwenye Nchi hizo, Wananchi wake hununua Maua Madogo ya Plastiki na kuyavaa kwenye Nguo zao. [PICHA KULIA].

FIFA ilionya kabla ya Mechi hiyo kuhusu uamuzi huo na kusisitiza kuwa Kanuni zao haziruhusu kuvaliwa au kuwepo na ujumbe wowote wa Kisiasa au Kibiashara nje ya Makubaliano katika Mechi zao.

FA ya England imetakiwa kulipa Faini ya £35,000, zile za Wales na Scotland kutozwa £15,700 kila mmoja, na Northern Ireland kutakiwa kulipa £11,800.

 

EPL: COSTA AIPA CHELSEA USHINDI WA 11 MFULULIZO, WAKO POINTI 9 MBELE KILELENI!

EPL LIGI KUU ENGLAND

Ratiba/Matokeo:

**Saa za Bongo

Jumamosi Desemba 17

Crystal Palace 0 Chelsea 1          

1800 Middlesbrough v Swansea City     

1800 Stoke City v Leicester City  

1800 Sunderland v Watford                  

1800 West Ham United v Hull City          

2030 West Bromwich Albion v Manchester United      

++++++++++++++++++++++

COSTA-CONTEVINARA wa EPL, Ligi Kuu England, Chelsea Leo huko Selhurst Park wameifunga Crystal Palace 1-0 na kupaa kileleni wakiwa Pointi 9 mbele.

Huo ni ushindi wa 11 mfululizo kwenye EPL wakiwania kuivunja Rekodi ya Arsenal ya kushinda Mechi 14 mfululizo iliyowekwa Mwaka 2002.

Bao la ushindi la Chelsea lilifungwa kwa Kichwa na Diego Costa katika Dakika ya 43 alipounganisha Krosi ya Cesar Azpilicueta.

Chelsea sasa wana Pointi 43 wakiwa wamecheza Mechi 1 zaidi ya Liverpool, walio Nafasi ya Pili, na Arsenal, walio Nafasi ya 3, zote zikiwa na Pointi 34 kila mmoja.

Jumapili Arsenal watacheza na Manchester City huko Etihad wakati Liverpool wakienda huko Goodison Park kucheza na Everton Jumatatu Usiku katika kimbembe cha Dabi ya Merseyside.

++++++++++++++++++++++

EP - REKODI ZA KUSHINDA MECHI NYINGI MFULULIZO:

Mechi  Timu                     Mechi ya Mwisho

14      Arsenal                    18 Agosti 2002

12      Manchester United  20 Agosti 2000

11      Manchester United  4 Machi 2009

11      Chelsea                   20 Septemba 2009

11      Liverpool                 20 Aprili 2014

11      Manchester City      12 Septemba 2015

11      Chelsea                  17 Desembar 2016 (Mbio zinaendelea)

++++++++++++++++++++++

VIKOSI:

Crystal Palace: Hennessey; Kelly, Dann, Delaney, Ward; McArthur, Ledley; Zaha, Cabaye, Puncheon; Benteke

Akiba: Speroni, Fryers, Mutch, Lee, Townsend, Husin, Campbell

Chelsea: Courtois; Azpilcueta, David Luiz, Cahill; Moses, Kanté, Matic, Alonso; Willian, Costa, Hazard

Akiba: Begovic, Ivanovic, Zouma, Chalobah, Fàbregas, Pedro, Batshuayi

REFA: JON MOSS

EPL, LIGI KUU ENGLAND

Ratiba:

**Saa za Bongo

Jumapili Desemba 18

1630 Bournemouth v Southampton       

1900 Manchester City v Arsenal   

1900 Tottenham Hotspur v Burnley                 

Jumatatu Desemba 19

2300 Everton v Liverpool  

         

 

 

EPL: JUMAMOSI CHELSEA WAANZA PALACE, KUENDELEA KUTUMBUA? MAN UNITED WAMALIZIA WBA, IBRA, POGBA KUTAMBA ZAIDI?

EPL LIGI KUU ENGLAND

Ratiba:

**Saa za Bongo

Jumamosi Desemba 17

1530 Crystal Palace v Chelsea               

1800 Middlesbrough v Swansea City     

1800 Stoke City v Leicester City  

1800 Sunderland v Watford                  

1800 West Ham United v Hull City          

2030 West Bromwich Albion v Manchester United      

++++++++++++++++++++++

CHELSEA-CONTE-1ST GAMEVINARA wa EPL, Ligi Kuu England, Chelsea Jumamosi wapo huko Selhurst Park kuivaa Crystal Palace wakisaka kudumisha ubabe wao wa kushinda Mechi 11 mfululizo.

Hiyo ndio Mechi ya kwanza kabisa ya EPL na itafuatiwa na Mechi 4 za Saa 12 Jioni ambazo mojawapo ni ile ya Mabingwa Watetezi Leicester City kuwa Wageni wa Stoke City.

Mechi ya mwisho Jumamosi ni Mechi tamu huko The Hawthorns wakati West Bromwich Albion wakiikaribisha Manchester United huku Timu zote zikiwa hali njema ya wimbi mfululizo wa ushindi.EPL-DES15

Jumapili EPL itaendelea kwa Mechi 3 lakini Bigi Mechi ni huko Etihad kati ya Manchester City na Arsenal.

EPL, LIGI KUU ENGLAND

Ratiba:

**Saa za Bongo

Jumapili Desemba 18

1630 Bournemouth v Southampton       

1900 Manchester City v Arsenal   

1900 Tottenham Hotspur v Burnley                 

Jumatatu Desemba 19

2300 Everton v Liverpool   

EPL: LEO VINARA CHELSEA KUBAKI KILELENI HATA IWEJE, LIVERPOOL, MAN UNITED UGENINI, CITY ETIHAD!

EPL, LIGI KUU ENGLAND
Ratiba
COSTA-CONTE***Saa za Bongo        
Jumatano Desemba 14
2245 Middlesbrough v Liverpool  
2245 Sunderland v Chelsea         
2240 West Ham United v Burnley
2300 Crystal Palace v Manchester United
2300 Manchester City v Watford            
2300 Stoke City v Southampton            
2300 Tottenham Hotspur v Hull City               
2300 West Bromwich Albion v Swansea City   
===============
Leo Jumatano zipo Mechi 8 za EPL na Vinara Chelsea wapo Ugenini Stadium of Light kucheza na EPL-DEC14Sunderland, Liverpool Ugenini na Boro, Man United Ugenini na Crystal Palace wakati Spurs wako kwao kucheza na Hull City.
Mechi hizo ni mwendelezo wa Mechi 2 za Jana za Raundi ya 16 ya EPL ambapo Arsenal walipoteza nafasi ya kutwaa uongozi wa Ligi walipotandikwa na Everton 2-1 huko Goodison Park Jijini Liverpool.
Matokeo haya yabaibakisha Chelsea kileleni hata kama Leo watafungwa kwani wana Pointi 37 wakifuata Arsenal wenye 31 na wa 3 ni Liverpool wenye Pointi 31zikifuata Man City 30, Spurs 27 na Man United 24.
EPL, Ligi Kuu England
Ratiba
***Saa za Bongo
Jumamosi Desemba 17
1530 Crystal Palace v Chelsea               
1800 Middlesbrough v Swansea City     
1800 Stoke City v Leicester City  
1800 Sunderland v Watford                  
1800 West Ham United v Hull City          
2030 West Bromwich Albion v Manchester United      
Jumapili Desemba 18
1630 Bournemouth v Southampton       
1900 Manchester City v Arsenal   
1900 Tottenham Hotspur v Burnley                 
Jumatatu Desemba 19h
2300 Everton v Liverpool