UEFA CHAMPIONZ LIGI: FAINALI JUMAMOSI JUVE NA REAL, TIMU ZILIZOPAMBANA MARA 18 ULAYA!

>PATA UNDANI:

UCL-FINAL-2017Juventus na Real Madrid zitakutana kwenye Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI Jumamosi Juni 3 huko Millenium Stadium, Jijini Cardiff, Wales na hiyo itakuwa mara yao ya 19 kucheza kwenye Mashindano haya ya Klabu Bingwa Ulaya.

Kila Timu imeshinda mara 8 na Sare 2 Juve ikifunga Bao 21 na Real 18.

PATA NINI KILIJIRI KATIKA MARA HIZO 18:

1961/62 Robo Fainali Kombe la Klabu Bingwa Ulaya

Juventus 0-1 Real Madrid

Real Madrid 0-1 Juventus

Real Madrid 3-1 Juventus (Marudiano Paris, France)

1986/87 Raundi ya Pili Kombe la Klabu Bingwa Ulaya

Real Madrid 1-0 Juventus

Juventus 1-0 Real Madrid (Baafa Dakika za Nyongeza, Real Madrid walishinda kwa Penati 3-1)

1995/96 Robo Fainali UEFA CHAMPIONZ LIGI

Real Madrid 1-0 Juventus

Juventus 2-0 Real Madrid

-Real walishinda Mechi ya Kwanza kwa Bao la Raúl González.

Kwenye Mechi ya Pili Juve waliibuka kidedea kwa Bao za Alessandro Del Piero na Michele Padovano.

1997/98 Fainali UEFA CHAMPIONZ LIGI

Juventus 0-1 Real Madrid

-Fainali hii ilichezwa huko Amsterdam ArenA, Nchini Netherlands na Predrag Mijatović kuwapa Real Bao pekee na la ushindi Dakika ya 66.

2002/03 Nusu Fainali UEFA CHAMPIONZ LIGI

Real Madrid 2-1 Juventus

Juventus 3-1 Real Madrid

-Real walishinda Mechi ya Kwanza kwa Bao za Ronaldo na Roberto Carlos huku Juve wakifunga Bao lao pekee kupitia David Trezeguet.

Katika Mechi ya Pili, Juve walipiga Bao 3 kupitia Trezeguet, Del Piero na Pavel Nedvěd wakati Real wakifunga Bao lao 1 kupitia Zinédine Zidane.

2004/05 Raundi ya Mtoano ya Timu 16 UEFA CHAMPIONZ LIGI

Real Madrid 1-0 Juventus

Juventus 2-0 Real Madrid (Baada Dakika 120)

-Juve walifungwa Mechi ya Kwanza huko Madrid 1-0 kwa Bao la Iván Helguera lakini katika Mechi ya Pili huko Turin Trezeguet aliipa Bao zikibaki Dakika 15 na Gemu kwenda Dakika za Nyongeza 30 Marcelo Zalayeta akapiga Bao la Pili na la ushindi kwa Juve katika Dakika ya 116 kwenye Mechi ambayo Ronaldo na Mchezaji wa Juve kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu Dakika ya 113.

2008/09 UEFA CHAMPIONZ LIGI Makundi

Juventus 2-1 Real Madrid

Real Madrid 0-2 Juventus

-Juve walishinda Mechi zote 2 za Makundi na Mechi ya Kwanza Bao za Juve zilifungwa na Del Piero na Amauri na la Real kupachikwa na Ruud van Nistelrooy wakati Mechi ya Pili Del Piero alipiga Bao zote mbili.

Timu hizi 2 zilifuzu kutoka Makundi lakini zilikwama Hatua ya iliyofuatia.

2013/14 UEFA CHAMPIONZ LIGI Makundi

Real Madrid 2-1 Juventus

Juventus 2-2 Real Madrid

-Safari hii Real waliwanyosha Juve kwenye Makundi kwa Bao 2 za Cristiano Ronaldo katika Mechi ya Kwanza huku Fernando Llorente akiwapa Juve Bao lao 1.

Mechi ya Pili ngoma ilikuwa Sare kwa Bao za Arturo Vidal na Llorente na Real kupiga kupitia Ronaldo na Gareth Bale.

2014/15 UEFA CHAMPIONZ LIGI Nusu Fainali

Juventus 2-1 Real Madrid

Real Madrid 1-1 Juventus

-Wakikutana kwa mara ya kwanza tangu Msimu wa 2002/03, Juve waliwalaza Real kwa kushinda Mechi ya Kwanza wakiwa Nyumbani kwa Bao za Álvaro Morata na Carlos Tévez wakati Bao la Real likipigwa na Ronaldo na kutoka Sare huko Madrid wakifunga Bao lao moja kupitia Alvaro Morata zikisalia Dakika 12 wakati Ronaldo aliwafungia Real kwa Penati Dakika ya 23 na kuwapa matumaini ya kusonga.

**Juventus wamekuwa Mabingwa wa Ulaya mara 2, Real Madrid wao wamebeba Kombe mara 11.

 

MAN UNITED KUISHUPALIA REAL INAYOMTAKA DE GEA!

MANUNITED-MAKIPAManchester United wanatarajia kuiwekea ngumu Real Madrid katika azma yao ya kumnasa Kipa wao David de Gea.

Mwaka 2015, Real Madrid, ambao Jumamosi wako huko Cardiff, Wales kucheza Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI na Juventus huku wakiwania kutetea Taji lao na kuwa Klabu ya Kwanza kufanya hivyo, walijaribu kumnunua De Gea lakini Dili ikakwama Dakika za mwisho katika Siku ya Mwisho ya Uhamisho huku pande zote zikiwa zimeafikiana Dau la Pauni Milioni 29.

De Gea, mwenye Miaka 26, alipigwa Benchi kwenye Fainali ya UEFA EUROPA LIGI hapo Mei 24 Man United wakiichapa Ajax 2-0 na kutwaa Kombe na langoni aliwekwa Kipa wa Timu ya Taifa ya Argentina Sergio Romero.

Hivi sasa, kama ilivyo kawaida ya Spain, Magazeti ya huko hushabikia mno Klabu kubwa na yale ya upande wa Real Madrid kila kukicha hawakosa kupiga ‘mdogo mdogo’ kuhusu De Gea kutua kwa Mabingwa hao wa Spain.

Lakini hivi sasa, kupita ule Mwaka 2015 ambao De Gea alikuwa kwenye Mwaka wa Mwisho wa Mkataba wake, Kipa huyo mahiri ana Mkataba unaokwisha 2019 na hivyo Man United hawana presha kubwa.

Hadi sasa, habari toka ndani ya Klabu ya Man United, zimedokeza kuwa De Gea hajaomba Uhamisho kama ilivyo kwa Wachezaji ambao wana nia hiyo.

MAN CITY ‘KUMDAKA’ KIPA WA BENFICA KWA DAU LA DUNIA!

CITY-EDERSON-DUNIAManchester City wako mbioni kumdaka Kipa wa Benfica Ederson na kumfanya awe Mchezaji wao wa pili kumsaini katika kipindi hiki kuelekea Msimu Mpya wa 2017/18 utakaoanza Agosti 12.

City washaafikiana na Benfica kulipa Dau la Pauni Milioni 35 kumnunua Ederson mwenye Miaka 23.

Dili hii itamfanya Kipa huyo kutoka Brazil kuwa Kipa wa Bei Ghali mno katika Historia akivunja Rekodi ya Juventus ya Italy ya Mwaka 2001 ilipolipa Pauni Milioni 32.6 kumnunua Gianluigi Buffon kutoka Parma.

Jana Ederson alatajiwa kutua Jiji la Manchester ili kupimwa Afya yake na kisha kukamilisha Uhamisho wake ambao ni wa pili kwa city hivi sasa baada ya kumchukua Mchezaji wa Portugal Bernado Silva kutoka AS Monaco kwa Dau la Pauni Milioni 45.

ZA AWALI:

SILVA KUTUA CITY

BERNARDO-SILVABernardo Silva Kiungo wa AS Monaco anaetoka Portugal, yuko mbioni kukamilisha Dili ya kutua Manchester City inayosemekana itagharimu Pauni Milioni 43.

Msimu huu, Silva, mwenye Miaka 22, aliisaidia sana Monaco kutwaa Ubingwa wa Ligi 1 huko France na pia kuifikisha Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.

Silva ameichezea Timu ya Taifa ya Portugal mara 12 na kufunga Bao 1 na kukipiga Mechi 58 na Monaco akifunga Bao 11.

NI RASMI, KIUNGO MICHAEL CARRICK KUBAKI OLD TRAFFORD MWAKA MWINGINE!

MANUNITED-CARRICK-ABEBA-FACUP-1KIUNGO wa Manchester United Michael Carrick amesaini Mkataba Mpya wa Mwaka Mmoja.
Carrick, mwenye Miaka 35, alitua Old Trafford kutoka Tottenham kwa dili ya £18.6m Mwaka 2006 na kucheza Mechi 458 akifunga Bao 24.
Carrick, ambae Mkataba wake wa sasa ulikuwa ukiisha Juni 4, ameeleza: "Nimefurahi safari yangu na hii Klabu Bora bado inaendelea!"
Hapo Juni 4 inatarajiwa kuchezwa Mechi Maalum Uwanjani Old Trafford kwa ajili ya kumuenzi Carrick kwa Utumishi wake mwema na Man United.
Meneja Jose Mourinho nae alizungumza: "Nimefurahi kufanya kazi na Michael Carrick Msimu huu wote. Mbali ya kuwa Mchezaji bora pia ni Binadamu mwema na mfano bora kwa Wachezaji Chipukizi!"
Carrick, ambae ni Mchezaji wa Kimataifa wa England, akiwa na Man United ameweza kutwaa UEFA CHAMPIONZ LIGI, EUROPA LIGI, FA CUP na Kombe la Ligi mara 2.
Michael Carrick na Wayne Rooney ndio Wachezaji pekee toka England ambao wamefanikiwa kutwaa Makombe ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, EUROPA LIGI, FA CUP, Kombe la Ligi na Kombe la Dunia kwa Klabu.
 

KEPTENI ROONEY AJITATHMINI, ABAKI AU ANG’OKE MAN UNITED!

>ENGLAND YAMWACHA KUMCHUKUA KIKOSINI!

MANUNITED-KEPTENI-ROONEYWayne Rooney amekataa hatajiunga na Klabu yeyote ya EPL, LIGI KUU ENGLAND, zaidi ya Everton wakati hivi sasa akijitathmini kama abaki au la Manchester United.

Msimu huu Rooney, ambae ni Kepteni wa Man United, amekuwa hana Namba Kikosini na ameanza Mechi 15 tu.

Lakini Jana Meneja wa Man United, Jose Mourinho, mara baada ya wao kubeba UEFA EUROPA LIGI kwa kuichapa Ajax Amsterdam huko Stockholm, Sweden, alisema angependa Rooney abakie Kikosini kwa ajili ya Msimu ujao.

Akiongea hiyo Jana Rooney alisema atafikia uamuzi katika Wiki 2 zijazo na pia kukiri amepokea Ofa nyingi toka Klabu za England na nje lakini amesema ikiwa ataondoka Man United basi ni Everton pekee ndio atajiunga nayo.

Everton ndiyo Klabu aliyoanzia tangu Utotoni na baadae kujiunga Man United chini ya Sir Alex Ferguson.

Rooney ndie anaeshikilia Rekodi ya Kufunga Bao nyingi kwa Man United na Timu ya Taifa ya England.

Kutokuwa na Namba ya kudumu Klabuni Man United kumeathiri Uteuzi kwenye Timu ya Taifa ya England kwani Meneja Derrick Southgate ametangaza Kikosi cha Wachezaji 25 bila Rooney.

England itacheza Ugenini huko Hampden Park Juni 10 na Scotland kwenye Mechi ya Kundi F la Nchi za Ulaya zinazowania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia.

Baada ya Mechi hiyo, England itasafiri kwenda France kucheza Mechi ya Kirafiki na France hapo Juni 13.

ENGLAND – KIKOSI KAMILI WACHEZAJI 25:

MAKIPA:

Jack Butland (Stoke), Fraser Forster (Southampton), Joe Hart (Torino, Mkopo toka Man City), Tom Heaton (Burnley)

MABEKI:

Ryan Bertrand (Southampton), Gary Cahill (Chelsea), Nathaniel Clyne (Liverpool), Aaron Cresswell (West Ham), Ben Gibson (Middlesbrough), Phil Jones (Man United), Chris Smalling (Man United), John Stones (Man City), Kieran Trippier (Tottenham), Kyle Walker (Tottenham)

VIUNGO:

Dele Alli (Tottenham), Eric Dier (Tottenham), Adam Lallana (Liverpool), Jesse Lingard (Man United), Jake Livermore (West Brom), Alex Oxlade-Chamberlain (Arsenal), Raheem Sterling (Man City)

MAFOWADI:

Jermain Defoe (Sunderland), Harry Kane (Tottenham), Marcus Rashford (Man United), Jamie Vardy (Leicester)