UEFA CHAMPIONZ LIGI: MBIVU, MBICHI JUMANNE NA JUMATANO, NANI KWENDA NUSU FAINALI?

UCL-2014-15-LOGO-1Klabu 4 ambazo zitatinga Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI zitapatikana Jumanne na Jumatano baada ya kukamilika kwa Mechi za Marudiano za Robo Fainali.
Baada ya Mechi za Kwanza za Robo Fainali, ni Barcelona pekee ipo hali njema baada ya kupata ushindi mnono wa Bao 3-1 Ugenini huko Paris, France walipoinyuka Paris Saint-Germain dhaifu iliyokosa Mastaa wake kadhaa.
Safari hii, wakiwa kwao Nou Camp Jumanne Usiku, Barcelona kidogo watapata kashkash kwani PSG itaimarika kwa kuwemo baadhi ya Mastaa hao pamoja na Supastaa Zlatan Ibrahimovic aliekosa Mechi ya kwanza kwa kuwa Kifungoni.
Lakini, ili kufuzu, PSG wana kibarua kigumu cha kupata ushindi mnono ili kupiku Bao za Ugenini za Barcelona.
Timu nyingine ambayo iliambua ushindi mnono ni FC Porto ya Ureno walipoichapa Bayern Munich 3-1 huko Mjini Porto lakini sasa Jumanne wako Ugenini Allianz Arena Jijini Munich ambako Bayern watasaka ushindi wa 2-0 ili wafuzu.
Jumatano Usiku, Juventus, walioshinda kwao Turin, Italy Bao 1-0, wako Ugenini kurudiana na AS Monaco.
Siku hiyo hiyo Jumatano, ipo El Derbi Madrileno, Dabi ya Jiji la Madrid, wakati Mahasimu Real Madrid na Atletico Madrid watakaporudiana huko Santiago Bernabeu huku matokeo ya Mechi ya kwanza yakiwa ni 0-0.
UEFA CHAMPIONZ LIGI
Robo Fainali-Mechi za Marudiano
**Mechi zote kuanza Saa 3 Dakika 45 Usiku, Saa za Bongo
**Kwenye Mabano ni Mabao Mechi za Kwanza
Jumanne Aprili 21
Bayern Munich v FC Porto [Allianz Arena, Munich, Germany] [1-3]
Barcelona v Paris Saint-Germain [Nou Camp, Barcelona, Spain] [3-1]
Jumatano Aprili 22
Real Madrid v Atletico Madrid [Santiago Bernabeu, Madrid, Spain] [0-0]
AS Monaco v Juventus [Stade Louis II, Monaco, France] [0-1]
 

FA CUP: SANCHEZ AIPELEKA ARSENAL FAINALI, KUKUTANA VILLA AU LIVERPOOL!

FACUP-SAFIJAN3-1Mabingwa Watetezi wa FA CUP, Arsenal, Leo hii Uwanja wa Wembley Jijini London, wameichapa Timu ya Daraja la chini la Championship, Reading, Bao 2-1 katika Nusu Fainali ya FA CUP.
Pasi safi ya Mesut Ozil ndiyo iliyompa nafasi Alexis Sanchez kuipa Bao la kwanza Arsenal Dakika ya 30 Bao ambalo lilidumu hadi Mapumziko.
++++++++++++++++++++++
DONDOO MUHIMU:
Uso kwa Uso
Kabla Mechi hii ya Leo, Katika Mechi 12 zilizopita kati ya Arsenal na Reading, Arsenal wameshinda Mechi zote.
Katika Mechi hizo 12, Arsenal walifunga Bao 37.
++++++++++++++++++++++
Reading walisawazisha katika Dakika ya 54 kwa Bao la McCleary  alieunganisha krosi ya Pogrebnyak kutoka kushoto kwa Goli. 
Hadi Dakika 90 kumalizika Gemu ilikuwa 1-1 na kuongezwa Dakika za Nyongeza 30.
Alexis Sanchez aliipa Arsenal Bao la Pili na la ushindi katika Dakika ya 106 baada ya Shuti lake kumpenya Kipa Federici.
Nusu Fainali nyingine itachezwa Kesho, pia Uwanjani Wembley, kati ya Aston Villa na Liverpool.
VIKOSI:
Reading: Federici, Gunter, Hector, Pearce, Obita, McCleary, Williams, Chalobah, Robson-Kanu, Mackie, Pogrebnyak.
Akiba: Stephen Kelly, Norwood, Cox, Yakubu, Karacan, Andersen, Cooper.
Arsenal: Szczesny, Debuchy, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Coquelin, Cazorla, Ramsey, Ozil, Sanchez, Welbeck.
Akiba: Gabriel, Wilshere, Giroud, Ospina, Walcott, Monreal, Flamini.
REFA: Martin Atkinson
FA CUP
Ratiba/Matokeo:
**Saa za Bongo
Nusu Fainali
Jumamosi Aprili 18
Reading 1 Arsenal 2
Jumapili Aprili 19
1700 Aston Villa v Liverpool
FAINALI
Jumamosi Mei 30
Arsenal v Aston Villa/Liverpool

FA CUP: LEO NUSU FAINALI WEMBLEY, READING v ARSENAL!

FACUP-SAFIJAN3-1Mabingwa Watetezi wa FA CUP, Arsenal, Leo wataingia Uwanja wa Wembley Jijini London kucheza na Timu ya Daraja la chini la Championship katika Nusu Fainali ya FA CUP.
Nusu Fainali nyingine itachezwa Kesho, pia Uwanjani Wembley, kati ya Aston Villa na Liverpool.
Hali za Timu
Reading hawaruhusiwi kuwachezesha Wachezaji wao Wawili wa Mkopo, Nathan Ake na Kwesi Appiah, kwa vile walishachezea Timu nyingine katika FA CUP Msimu huu.
Arsenal itawakosa Majeruhi Mikel Arteta na Alex Oxlade-Chamberlain lakini huenda Majeruhi waliopona, Jack Wilshere na Mathieu Debuchy, wakacheza sehemu ya Mechi hii.
Tathmini
Hii ni Nusu Fainali ya kwanza ya FA CUP kwa Reading tangu Mwaka 1927 wakati Arsenal walitinga hatua hii Msimu uliopita kuelekea kutwaa Kombe hili.
Hadi kufikia hapa, Reading hawahuwahi kukutana na Timu ya LIgi Kuu England kwenye FA CUP Msimu huu na hivi sasa hawajashinda Mechi kwa Mwezi mzima.
Akiongelea matumaini ya Timu yake, Meneja wa Reading, Steve Clarke, amesema wanahitaji kucheza Gemu isiyo na makosa ili washinde.
Ushindi kwao utategemea hasa Mastraika wao wenye nguvu Pavel Pogrebnyak na Jamie Mackie huku Walinzi wao, Jordan Obita na Michael Hector, wakitakiwa kuwa makini na watulivu.
Uso kwa Uso
Katika Mechi 12 zilizopita kati ya Arsenal na Reading, Arsenal wameshinda Mechi zote.
Katika Mechi hizo 12, Arsenal walifunga Bao 37.
FA CUP
Nusu Fainali
Ratiba
**Saa za Bongo
Jumamosi Aprili 18
1920 Reading v Arsenal
Jumapili Aprili 19
1800 Aston Villa v Liverpool

MJUE 'MCHEZA RAFU' MKUBWA LIGI KUU ENGLAND!

8d9be99a-702f-4218-8410-5e45a0661e25-620x372WALIMKEBEHI Kepteni wa Liverpool Steven Gerrard kwa kupewa Kadi Nyekundu Sekunde 30 tu tangu aingie Uwanjani kutoka Benchi Uwanjani Anfield wakati Liverpool inachapwa 2-1 na Manchester United na Gemu ya Burnley na Chelsea ilishuhudia Wachezaji Wawili, Ashley Barnes na Diego Costa, wakifungiwa kwa kutimba, lakini Je ni nani hasa ndie 'Mfalme wa Rafu' Uwanjani LIGI KUU ENGLAND Msimu huu?
PATA LISTI YA WALIOCHEZA RAFU MARA NYINGI:
9. Alex Song [West Ham], Fernandinho [Man City], Gareth Barry [Everton]: RAFU 47
7. Marouane Fellaini [Man United], Moussa Sissoko [Newcastle]: 48
5. Mame Biram Diouf [Stoke], Connor Wickham [Sunderland]: 50
4. Graziano Pelle [Southampton]: 56
3. Leonardo Ulloa [Leicester City]: 57
2. Victor Wanyama [Southampton]: 58
1. Ashley Barnes [Burnley]: 65

MJUE MCHEZAJI ANAEPIGWA BUTI KUPITA MWINGINE YEYOTE ENGLAND!

e67570d87b92bd2d1f2ff4d35438af40 crop northMsimu huu kwenye Ligi  Kuu England Wachezaji kadhaa wameng'ara kwa kuonyesha uchawi wao Uwanjani lakini wapo ambao hadi sasa wametinga 10 Bora ya kuchezewa Faulo nyingi kupita wengine.
Takwimu hizi zimeletwa na Wanastadi wa Takwimu za Soka.
WACHEZAJI 10 WA LIGI KUU ENGLAND WANAOONGOZA KWA KUCHEZEWA RAFU:
10. Remy Cabella, Newcastle: Rafu 49
9. Connor Wickaham, Sunderland: 50
8. Stephane Sessegnon, WBA: 53
7. Santi Cazorla, Arsenal:  54
6. Gabriel Agbonlahor, Aston Villa: 56
5. Steven Naismith, Everton: 58
4. Sadio Mane, Southampton: 60
3. Alexis Sanchez, Arsenal: 61
2. Raheem Sterling, Liverpool: 77
1. Eden Hazard, Chelsea: 94