UEFA CHAMPIONZ LIGI: JUVE YATINGA FAINALI!

RATIBA/MATOKEO:
Nusu Fainali – Mechi za Marudiano
**Mechi kuanza Saa 3 Dakika 45 Usiku, Saa za Bongo
***Kwenye Mabano Mabao Mechi 2
Jumanne Mei 9
Juventus 2 Monaco 1 [4-1]
Jumatano Mei 10
***Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza
Atletico Madrid v Real Madrid [0-3]
=============================
UCL-16-17-SITMABINGWA wa Italy Juventus Jana waliichapa AS Monaco 2-1 Mjini Turin na kutinga Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Juve wamesonga Fainali kwa Jumla ya Mabao 4-1 kwani walishinda pia Mechi ya kwanza 2-0.
Hii ni Fainali ya Pili kwa Juve katika Misimu Mitatu iliyopita.
Jana Juve waliongoza 2-0 hadi Mapumziko kwa Bao za Mario Mandzukic na Dani Alves zilizofungwa Dakika za 33 na 44.
Bao la Monaco liliingizwa Dakika ya 69 na Chipukizi Kylian Mbappe.
Juve, ambao hawajatwaa Kombe hili tangu 1996 na walifungwa 3-1 na Barcelona kwenye Fainali ya 2015, Fainali ya Mwaka huu watacheza na Mshindi kati ya Atletico Madrid na Real Madrid wanaorudiana Leo huko Vicente Calderon huko Madrid huku Real wakiongoza 3-0 baada kushinda Mechi ya kwanza.
 

EPL: WEST HAM YAIDUNDA SPURS, KWEUPE CHELSEA KUTWAA UBINGWA WAKISHINDA 2 ZIJAZO!

WESTHAM-LANZINIBAO la Dakika ya 65 la Manuel Lanzini limewapa ushindi West Ham wa 1-0 walipocheza na Tottenham Hotspur ambao sasa wamepoteza matumaini ya kuwakaba Chelsea kwenye mbio za Ubingwa wa EPL, Ligi Kuu England.

Kama Leo Spurs wangeshinda pengo lao na Vinara lingekuwa Pointi 1 tu lakini kipigo hiki kwao kimefungua njia kwa Chelsea kuwa Bingwa ikiwa watashinda Mechi 2 zijazo kati ya 4 walizobakiza.

Jumatatu Chelsea wako kwao Stamford Bridge kucheza na Middlesbrough na Ijumaa wapo Ugenini huko The Hawthorns kucheza na West Bromwich Albion.

VIKOSI:

WEST HAM: Adrian, Collins, Reid, Fonte, Byram, Noble, Kouyate, Cresswell, Lanzini, Ayew, Calleri

Akiba: Randolph, Nordtveit, Feghouli, Snodgrass, Fletcher, Fernandes, Rice.

TOTTENHAM HOTSPUR: Eriksen, Davies, Alli, Son, Kane

Akiba: Janssen, Vorm, Nkoudou, Trippier, Sissoko, Wimmer, Dembele.

REFA:

EPL, LIGI KUU ENGLAND

Ratiba/Matokeo:

Ijumaa Mei 5

West Ham United 1 Tottenham Hotspur 0

Jumamosi Mei 6

1430 Manchester City v Crystal Palace

1700 Bournemouth v Stoke City

1700 Burnley v West Bromwich Albion

1700 Hull City v Sunderland

1700 Leicester City v Watford

1930 Swansea City v Everton

Jumapili Mei 7

1530 Liverpool v Southampton

1800 Arsenal v Manchester United

Jumatatu Mei 8

2200 Chelsea v Middlesbrough

Jumatano Mei 10

2145 Southampton v Arsenal                

Ijumaa Mei 12

2145 Everton v Watford              

2200 West Bromwich Albion v Chelsea             

Jumamosi Mei 13

1430 Manchester City v Leicester City             

1700 Bournemouth v Burnley                

1700 Middlesbrough v Southampton     

1700 Sunderland v Swansea City 

1930 Stoke City v Arsenal 

Jumapili Mei 14

1400 Crystal Palace v Hull City    

1615 West Ham United v Liverpool       

1830 Tottenham Hotspur v Manchester United  

UEFA CHAMPIONZ LIGI: RONALDO HATARI, AIFYEKA ATLETICO 3 KWENYE EL DERBI MADRILENO HUKO BERNABEU!

>LEO MONACO v JUVENTUS!

UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI

Nusu Fainali – Mechi za Kwanza

Jumanne Mei 2

Real Madrid 3 Atletico Madrid 0

++++++++++++++++

RONALDO-HATARIJANA huko Estadio Santiago Bernabéu Jijini Madrid Nchini Spain Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali ya Kwanza ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, kati ya Mahasimu wakuu wa Mji huo Real Madrid na Atletico Madrid ambayo hubatizwa El Derbi Madrileno, ilichezwa na Mchezaji Bora Duniani Cristiano Ronaldo aliibuka Shujaa kwa kubamiza Bao zote 3 wakati Real ikishinda 3-0.

Hii ilikuwa ni mara ya 5 kwa Timu hizi kupambana katika Mechi za Ulaya na Real Madrid walimaliza ndoto za Atlético Madrid kwenye UCL katika Misimu Mitatu iliyopita, ikiwa ni pamoja wa Fainali za Mwaka 2014 na 2016, na safari hii hali inaelekea ni hiyohiyo labda Atletico wamudu kubadilika katika Marudiano Wiki ijayo wakiwa kwao Vicente Calderon na kupindua kipigo hiki cha 3-0.

Ronaldo aliipa Real Bao lao la Kwanza Dakika ya 10 kwa Kichwa alipounganisha Krosi ya Casemiro na kupiga Bao nyingine 2 Dakika za 73 na 86.

Hii ni mara ya Pili mfululizo kwa Ronaldo kupiga Hetitriki kwani katika Mechi 2 zilizopita za Robo Fainali za UCL dhidi ya Bayern Munich alipiga Hetitriki kwenye Mechi hizo alizofunga Jumla ya Bao 5.

Ronaldo ndie Mfungaji Bora katika Historia ya UCL akiwa na Bao 103.

Hii Leo ipo Mechi nyingine ya Kwanza ya Nusu Fainali ya UCL huko Monaco kati ya AS Monaco na Juventus.

VIKOSI:
REAL MADRID:
Navas, Carvajal, Ramos, Varane, Marcelo, Kroos, Casemiro, Modrić, Isco, Benzema, Ronaldo

Akiba: Casilla, Nacho, James Rodríguez, Kovačić, Vázquez, Asensio, Morata
ATLÉTICO MADRID: Oblak, Lucas Hernández, Savić, Godin, Filipe Luis, Koke, Gabi, Saúl Ñíguez, Carrasco, Griezmann, Gameiro

Akiba: Moyà, Tiago, Torres, Correa, Thomas, Gaitán, Alberto Rodríguez

REFA: Martin Atkinson [England]

UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI

Nusu Fainali – Mechi za Kwanza

**Mechi kuanza Saa 3 Dakika 45 Usiku, Saa za Bongo

Jumatano Mei 3

AS Monaco v Juventus

TAREHE MUHIMU:

MECHI ZA MTOANO:

02–03/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Kwanza

09–10/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Pili

03/06/17: Fainali (National Stadium of Wales, Cardiff)

 

 

 

UCL-NUSU FAINALI: HISTORIA IPO KWA JUVE ILA MONACO WANAE TINEJA KYLIAN MBAPPE!

UCL-16-17-SIT-1NUSU FAINALI ya Pili ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, itachezwa Jumatano Usiku Stade Louis II, Monaco kati ya Wenyeji AS Monaco na Juventus ya Italy.
Mechi hii inakutanisha Difensi imara dhidi ya Washambuliaji hatari huku Monaco wakisifika kwa kupiga Bao nyingi wakati Juve wakifungwa Goli chache.
Monaco ni Timu yenye Vijana wengi wakati Juve ina Wakongwe na Wazoefu wengi.
Wakati Juve wakitumia Mfumo wa 4-2-3-1 chini ya Kocha Max Allegri ambao huhakikisha Pjanic, Dybala, Higuain, Mandzukic pamoja na Maveterani Buffon, Chiellini, Bonucci na Dani Alves wote kuwepo Uwanjani, Monaco, chini ya Kocha kutoka Ureno Leonardo Jardim, wao hung'ara kwa Mfumo wa kasi wa 4-4-2 unaotoa mwanya kwa Tineja wao wa Miaka 18 Kylian Mbappe kuliza Watu.
Tineja huyo, ambae amefunga Bao 18 katika Mechi 18 zilizopita, hupata sapoti kubwa toka kwa Almamy Toure, Bejamin Mendy, Bernardo Silva, na Nabil Dirar huku Radamel Falcao akiibuka upya Msimu huu na kupiga Bao 28.
Hii ni mara ya kwanza kwa Monaco kutinga Nusu Fainali tangu 2004 lakini mara 2 wamepigwa na Juventus kwenye Mashindano haya ya Ulaya.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:

Juventus (Mfumo 4-2-3-1): Buffon, Dani Alves, Bonucci, Chiellini, Alex Sandro, Pjanic, Marchisio, Cuadrado, Dybala, Mandzukic, Higuain

Monaco (Mfumo 4-4-2): Subasic, Dirar, Glik, Fabinho, Toure, Silva, Moutinho, Bakayoko, Lemar, Mbappe, Falcao

REFA: Antonio Mateu Lahoz (Spain)


 

UEFA KLABU ULAYA - WIKI YA NUSU FAINALI, KUANZA JUMANNE EL DERBI MADRILENO REAL-ATLETI, KUMALIZA CELTA VIGO-MAN UNITED!

UCL-16-17-SIT-1HII ndio Wiki ya kusaka Klabu Vigogo Ulaya ambapo Mechi za Nusu Fainali za UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, na UEL, UEFA EUROPA LIGI, zitaanza kuchezwa.
Kwenye UCL, Jumanne Mei 2 ni mtanange mkali huko Stadio Santiago Bernabeu ambako kutakuwa na Dabi ya Jiji la Madrid maarufu kama EL DERBI MADRILENO kati ya Mabingwa Watetezi Real Madrid na Atletico Madrid.
Jumatano ni Nusu Fainali nyingine ya Mashindano haya kati ya AS Monaco na Juventus.
Siku hiyo hiyo pia ipo Nusu Fainali ya kwanza ya UEL, UEFA EUROPA LIGI, itakayochezwa huko Amsterdam, Netherlands kati ya Ajax Amsterdam na Lyon.
Alhamisi ni huko Spain ambako Nusu Fainali nyingine ya UEL itafanyika kati ya Celta Vigo na Manchester United.
Marudiano ya Nusu Fainali hizi ni Wiki ijayo.
RATIBA
UEFA CHAMPIONZ LIGI
Nusu Fainali - Mechi za Kwanza
Jumanne Mei 2
2145 Real Madrid v Atletico Madrid
Jumatano Mei 3
2145 AS Monaco v Juventus
UEFA EUROPA LIGI
Nusu Fainali - Mechi za Kwanza
Jumatano Mei 3
Ajax v Lyon
Alhamisi Mei 4
Celta Vigo v Manchester United
 

Habari MotoMotoZ