HATIMA YA WENGER KUTANGAZWA NA BODI YA ARSENAL BAADA FAINALI YA FA CUP!

WENGER-OUT-APR1Arsene Wenger ametamka kuwa Arsenal itakuwa na Kikao cha Bodi yake kuamua hatima yake mara baada ya Fainali ya FA CUP.

Arsenal itakutana na Mabingwa Wapya wa England Chelsea hapo Mei 27 huko Wembley kwenye Fainali ya FA CUP.

Pamoja na hatima ya Wenger kubaki au kung’oka kama Meneja pia Bodi hiyo itapitia Masuala ya Uhamisho wa Wachezaji kwa ajili ya Msimu Mpya pamoja na Mazungumzo yanayoendelea ya Mikataba Mipya ya Mastaa wao Mesut Ozil na Alexis Sanchez.

Akiongea na Wanahabri kuhusu Mechi yao ya mwisho ya EPL, LIGI KUU ENGLAND, yah apo Jumapili dhidi ya Everton, Wenger aligoma kwenda kwa undani kuhusu hatima yake.

Alieleza: “Siwezi kuwaambia. Kitu muhimu ni kushinda Gemu yetu Jumapili na linaloweza kutokea kwangu litasubiri. Nipo hapa kutumikia Klabu!”

Aliongeza: “Nadhani Bodi itakutana baada ya Fainali ya FA CUP. Nitakuwepo. Kwa sasa mkazo ni hii Gemu yetu.”

Kuhusu Ozil na Sanchez, ambao Mikataba yao inaisha Mwakani lakini sasa wanasita kusaini Mikataba Mipya, Wenger alieleza Wachezaji hao bado wanatumikia vyema Klabu na hawaonyeshi kama wanania ya kuhama.

MOURINHO AIJIA JUU EPL KUWEKA ‘MECHI ISIYO MAANA’ JUMAPILI WAKATI WANA FAINALI JUMATANO!

>JUMAPILI NA PALACE, JUMATANO FAINALI ULAYA HUKO SWEDEN!

MANUNITED-MOU-CELEBRATES-WITH-TEAMJOSE MOURINHO ameijia juu EPL, LIGI KUU ENGLAND, na kudai popote kwingine Duniani Manchester United ingepewa Siku 1 ya ziada ya kupumzika kabla ya Mechi yao ya Fainali ya UEFA EUROPA LIGI.

Jumapili Man United wapo kwao Old Trafford kucheza Mechi yao ya mwisho ya EPL ambayo haina manufaa yeyote kwa Timu zote 2 mbali ya kukamisha Ratiba na kisha Jumatano wapo safarini huko Sweden kucheza Fainali ya UEFA EUROPA LIGI dhidi ya Ajax Amsterdam ambao Ligi yao ya Netherlands ilimalizika Jumapili Mei 14.

Mourinho amedai baada ya Wiki iliyopita Palace kujihakikishia kubaki EPL kwa kuifunga Hull City na wao kuganda Nafasi ya 6 tu basi Mechi hii ingechezwa Jumamosi na si Jumapili ili wao kupata Siku 1 ya ziada ya Mapumziko.

Kutokana na kutopata msaada huo Mourinho ameamua kuchezesha Kikosi kipya kwenye Mechi hiyo Jumapili na Palace.
Akiongea Jana baada ya kutoka 0-0 na Southampton, Mourinho alieleza: "Nchi nyingine yeyote Mechi hii ingekuwa Jumamosi. Sisi ni wa 6, Palace wako salama!"

Mourinho amedai hakuna anaezijali Timu za England huko England na pia kueleza kimzaha: "Natumai Mashabiki watasapoti Kikosi cha Jumapili na kusamehe ugeni wake na kutojiamini. Na pia Big Sam ataonyesha urafiki na kuwa laini kwetu na kumwambia Wilfried Zaha acheze polepole na kumwacha Christian Benteke nyumbani!"

Mourinho amedokeza kuwa kwenye Kikosi cha Jumapili atakuwepo Paul Pogba ambae hajacheza Wiki yote hii baada kufiwa na Baba yake Mzazi.

Ameeleza: "Lakini pia watakuwepo Chipukizi Demetri Mitchell, Scott McTominay, Axel Tuanzebe, Josh Harrop na Zachary Dearnley huku Kipa akiwa Joel Castro Pereira pamoja na Beki Eric Bailly!" 

Bailly hatacheza Fainali ya Jumatano baada ya Kadi Nyekundu kwenye Mechi ya Nusu Fainali na Celta Vigo.

MOURINHO - AGUSIA HATARI YA 'KUWEKA MAYAI YOTE KAPU 1'!

==ADAI MAN UNITED KIPAU MBELE KILIKUWA NI EUROPA SI LIGI!
MANUNITED-MOU-CELEBRATES-WITH-TEAMJose Mourinho ametoboa Manchester United walishaamua kuipa kipau mbele UEFA EUROPA LIGI na si EPL, LIGI KUU ENGLAND, kwa sababu kuweka umuhimu kwa vyote viwili ilikuwa haiwezekani.
Jana Man United ilifungwa 2-1 na Tottenham huko White Hart Lane na kuiacha Tottenham ikipata hakika ya kubaki Nafasi ya Pili kwenye Ligi wakati Man United wakivunjiwa matumaini yao finyu ya kumaliza ndani ya 4 Bora.
Tayari Man United wana nafasi ya kucheza UEFA EUROPA LIGI Msimu ujao kwanza kwa kutwaa EFL CUP na pia wakimaliza Ligi Nafasi ya 5 au ya 6 ambayo hawawezi kuikosa.
Licha ya kuikosa 4 Bora ya EPL na hivyo kukosa nafasi ya kushiriki UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao kutokana na Msimamo wa EPL, Man United wanayo nafasi ya kushiriki Mashindano hayo ikiwa tu wataifunga Ajax Amsterdam kwenye Fainali ya UEFA EUROPA LIGI itakayochezwa Jumatano Mei 24 huko Stockholm, Sweden.
Mourinho ameeleza: "Sikuchukizwa kutomaliza 4 Bora kwa sababu tuliamua. Watu wakisema tunacheza kamari kwa kutilia mkazo EUROPA LIGI..hatuchezi kamari. Hatukuchagua EUROPA, ilibidi iwe hivyo!"
Aliongeza: "Ningekuwa nao Ashley Young na Luke Shaw, Marcos Rojo, Zlatan Ibrahimovic, Tim Fosu-Mensah - ningekuwa nao hao, ningeweza kubadili Timu na kutilia mkazo kila Mechi! Lakini nina Wachezaji 14 au 15 tu. Siwezi kutilia mkazo kila Mechi. Haiwezekani ucheze kila baada Siku 3!"
Huku akiweka Jicho moja Fainali ya EUROPA LIGI, Mourinho ashaweka bayana atabadili Kikosi kwenye Mechi za Ligi za Jumatano dhidi ya Southampton na ile ya mwisho ya Ligi Jumapili na Crystal Palace.
Hata hivyo, Mourinho ameseka kwenye Vikosi vyake hataweka Chipukizi watupu tu kwa sababu anataka atoe upinzani.
Amesema: "Tumefungwa 2-0 na Arsenal lakini tulipigana. Tumepoteza 2-1 na Spurs tulipigana. Dhidi ya Southampton ni hivyo hivyo, ntabadili Timu lakini.itakuwa na ushindani. Blind hatacheza lakini Fellaini atacheza!"
 

CHELSEA – MABINGWA 2017: CONTE ATAKA DABO, WABEBE PIA FA CUP, KOMBE LA UBINGWA KUPOKEWA KWA PAMOJA TERRY NA CAHILL!

CHELSEA-MABINGWA-2016-17ANTONIO CONTE, Meneja wa Mabingwa Wapya wa England, Chelsea, ameitaka Timu yake kuugeuza Msimu huu ‘mkubwa’ kuwa Msimu wa ‘raha tupu’ kwa pia kulibeba Kombe la FA CUP.

Jana Chelsea waliibuka Mabingwa wa EPL, LIGI KUU ENGLAND, huku wakibakiza Mechi 2 kwa kuifunga West Bromwich Albion 1-0 huko The Hawthorns kwa Bao la Dakika ya 82 la Michy Batshuayi.

Huo ni Ubingwa wa 6 wa England kwa Chelsea.

Hapo Mei 27 huko Wembley Jijini London, Chelsea wataivaa Arsenal katika Fainali ya FA CUP.

Jana Antonio Conte alisema: “Nasikia fahari kubwa kutwaa Ubingwa hapa England katika Msimu wangu wa kwanza tu. Wachezaji wangu walionyesha juhudi kubwa. Tuna Gemu 2 za kusheherekea halafu tunapaswa kuugeuza Msimu huu mkubwa kuwa wa raha tupu!”

Conte, ambae alijiunga na Chelsea mwanzoni mwa Msimu baada ya kuiacha Timu ya Taifa ya Italy mara baada ya Fainali za EURO 2016, amesema kubadili Mfumo na kutumia Difensi ya Mtu 3 Mwezi Septemba mara baada ya kupigwa 3-0 na Arsenal kuliwazindua na kupigania Ubingwa.

Wakati huo Chelsea walikuwa Nafasi ya 8 Pointi 8 nyuma ya Vinara Man City lakini walipobadili Mfumo na kutumia 3-4-3 walikwenda Mechi 13 bila kufungwa na sasa wanaongoza Ligi wakiwa na Mechi 2 mkononi na Pointi 10 mbele ya Timu ya Pili.

WAKATI HUO HUO, Nahodha wa Chelsea John Terry ametoboa kuwa watalipokea Kombe la Ubingwa wa EPL yeye pamoja na Gary Cahill kwenye Siku ya mwisho ya Msimu hapo Mei 21 wakati Chelsea wakimaliza Ligi na Sunderland huko Stamford Bridge.

Msimu huu Terry amecheza Mechi 5 tu za Ligi lakini Cahill amecheza zote kasoro moja tu.

UEFA CHAMPIONZ LIGI: ATLETI YAIFUNGA REAL LAKINI MABINGWA REAL WATINGA FAINALI KUIVAA JUVE!!

>>REAL YAWANIA KUWA BINGWA WA KWANZA KUTETEA TAJI VYEMA!

MATOKEO:

Nusu Fainali – Mechi za Marudiano

***Kwenye Mabano Mabao Mechi 2

Jumanne Mei 9

Juventus 2 Monaco 1 [4-1]

Jumatano Mei 10

Atletico Madrid 2 Real Madrid 1 [2-4]

real-fainaliMABINGWA WATETEZI wa Kombe la UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, Real Madrid Jana walifungwa 2-1 na Mahasimu wao Atletico Madrid huko Vicente Calderon Jijini Madrid lakini ni Real ndio waliotinga Fainali ambako watacheza na Juventus ya Italy.

Real, ambao wanawania kuwa Timu ya kwanza kabisa kutetea Taji la UCL, waliifunga Atletico 3-0 kwrenye Mechi ya kwanza huko EstadionB Santiago Bernabeu Wiki iliyopita na sasa wamesonga kwa Jumla ya Bao 4-2.

Jana, kwenye Mechi hii ambayo hubatizwa El Derbi Madrileno, Atletico walitangulia 2-0 kwa Bao za ndani ya Dakika 16 za kwanza na kuleta matumaini ya kupindua kipigo cha 3-0.

Bao hizo zilifungwa Dakika za 12 na 16 na Saul Niguez kwa Kichwa na Penati ya Antoine Griezmann.

Lakini Dakika ya 42, Isco akaipa uhai mkubwa Real alipofunga Bao ambalo lilifanya kuwa Atletico ahitaji Bao 3 ili wao watinge Fainali.

Hadi mwisho Atletico 2 Real 1.

Fainali ya UCL itachezwa huko Cardiff, Wales hapo Juni 3.

VIKOSI:

Atletico:Oblak, Gimenez, Savic, Godin, Filipe Luis, Koke, Gabi, Saul Niguez, Carrasco, Griezmann, Torres.
Akiba: Moya, Tiago, Correa, Lucas Hernandez, Gameiro, Thomas, Gaitan.

Real:Navas, Danilo, Varane, Ramos, Marcelo, Casemiro, Modric, Isco, Kroos, Bemzema, Ronaldo.

Akiba: Casilla, Nacho, Rodriguez, Kovacic, Vazquez, Asensio, Morata.

REFA:Cuneyt Cakir (Turkey)

UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI

TAREHE MUHIMU:

03/06/17: Fainali (National Stadium of Wales, Cardiff)

Habari MotoMotoZ