UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI 2017/18 YAANZA!

MSIMU MPYA wa UCL UEFA CHAMPIONZ LIGI, wa 2017/18 tayari umeanza kwa Mechi za Raundi ya Kwanza Mtoano zilizochezwa Jumanne na Jumatano.

Mechi za Marudiano za Raundi hiyo zitachezwa Julai 4.

UCL SIT SAFIKatika Mechi hizo za kwanza za Raundi ya Kwanza ya Mtoano, Klabu za Alashkert, Europa, Hibernians, Víkingur na Linfield ziliibuka na ushindi.

Kwenye Raundi ya Kwanza ya Mtoano zipo Mechi 5 na Washindi wake Watano watasonga Raundi ya Pili ya Mtoano.

Raundi ya Pili Mtoano ina Mechi 17 na Washindi wake kusonga Raundi ya 3 ya Mtoano.

Moja ya Timu kubwa ambayo ipo Raundi ya Pili ya Mtoano ni Celtic ya Scotland ambao waliwahi kuwa Klabu Bingwa Ulaya.

Ikiwa Celtic watashinda watasonga Raundi ya 3 ya Mtoano ambako watajumuika na Timu kubwa nyingine kama vile Nice na Ajax.

Droo ya Raundi ya 3 ya Mtoano itafanyika Julai 14.

Washindi wa Raundi ya Tatu Mtoano watasonga Raundi ya Mwisho ya Mchujo ambako zitaingia Timu vigogo Liverpool, Sevilla, Napoli, Hoffenheim na Sporting Lisbon.

Droo ya Raundi ya Mwisho ya Mchujo itafanywa Agosti 24.

Washindi 10 wa Raundi hiyo wataingizwa Droo ya kupanga Makundi ambayo itafanywa Agosti 24 ambapo ina Klabu 22 zilizofuzu moja kwa moja Hatua hii wakiwemo Mabingwa Watetezi Real Madrid na Vigogo wengine kama vile Barcelona, Bayern Munich, Tottenham, Man City na Man United ambao wametinga hapo kwa Tiketi ya kuwa Mabingwa wa UEFA EUROPA LIGI.

Jumanne Julai 27

Alashkert 1-0 FC Santa Coloma

Víkingur 2-1 Trepça '89

Hibernians 2-0 FCI Tallinn

The New Saints 1-2 Europa

Jumatano Julai 28

Linfield 1-0 La Fiorita

**Marudiano Julai 4

Raundi ya Pili Mtoano (11/12 & 18/29 Julai)

APOEL (CYP) v Dudelange (LUX)

Žalgiris (LTU) v Ludogorets Razgrad (BUL)

Qarabag (AZE) v Samtredia (GEO)

Partizan (SRB) v Buducnost Podgorica (MNE)

Hibernians (MLT)/FCI Tallinn (EST) v Salzburg (AUT)

Sheriff Tiraspol (MDA) v Kukës (ALB)

Astana (KAZ) v Spartaks Jurmala (LVA)

BATE Borisov (BLR) v Alashkert (ARM)/FC Santa Coloma (AND)

Žilina (SVK) v København (DEN)

Hapoel Beer-Sheva (ISR) v Honvéd (HUN)

Rijeka (CRO) v The New Saints (WAL)/Europa (GIB)

Malmö (SWE) v Vardar (MKD)

Zrinjski (BIH) v Maribor (SVN)

Dundalk (IRL) v Rosenborg (NOR)

FH Hafnarfjördur (ISL) v Víkingur (FRO)/Trepça '89 (KOS)

Linfield (NIR)/La Fiorita (SMR) v Celtic (SCO)

IFK Mariehamn (FIN) v Legia Warszawa (POL)

UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI 2017/18

Kalenda

Droo

19/06/17: Droo Raundi ya 1 na 2 za Mtoano

Raundi ya Kwanza Mtoano

27–28/06/17: Mechi za Kwanza

04–05/07/17: Mechi za Pili

Raundi ya Pili Mtoano

11–12/07/17: Mechi za Kwanza

Droo

14/07/17: Droo Raundi ya 3 Mtoano

Raundi ya Pili Mtoano

18–19/07/17: Mechi za Pili

Raundi ya Tatu Mtoano

25–26/07/17: Mechi za Kwanza

01–02/08/17: Mechi za Pili

Droo

04/08/17: Raundi ya Mwisho Mchujo

Raundi ya Mwisho Mchujo

15–16/08/17: Mechi za Kwanza

22–23/08/17: Mechi za Pili

Droo

24/08/17: Makundi

Makundi

12–13/09/17: Mechi ya 1

26–27/09/17: Mechi ya 2

17–18/10/17: Mechi ya 3

31/10/17–01/11/17: Mechi ya 4

21–22/11/17: Mechi ya 5

05–06/12/17 Mechi ya 6

Droo

11/12/17: Raundi ya Mtoano Timu 16

Raundi ya Mtoano Timu 16

13–14/02/18 and 20–21/02/18: Mechi za Kwanza

06–07/03/18 and 13–14/03/18: Mechi za Pili

Droo

16/03/18: Robo Fainali

Robo Fainali

03–04/04/18: Mechi za Kwanza

10–11/04/18: Mechi za Pili

Droo

13/04/18: Nusu Fainali na Fainali

Nusu Fainali

24–25/04/18: Mechi za Kwanza

01–02/05/18: Mechi za Pili

Fainali

26/05/18: (NSK Olimpiyski, Kyiv, Ukraine)

KLABU NA HATUA WANAZOANZIA:

Makundi

Real Madrid

Chelsea

FC Porto

Feyenoord

Barcelona

Tottenham Hotspur

AS Monaco

Besiktas

Atletico Madrid

Man City

Paris Saint-Germain

FC Basel

Bayern Munich

Juventus

Man United

RB Leipzig

AS Roma

Shakhtar Donetsk

Borussia Dortmund

Benfica

Anderlecht

Raundi ya Mwisho Mchujo

Sevilla

Liverpool

Sporting Lisbon

1989 Hoffenheim

Napoli

Raundi ya 3 Mtoano

Slavia Prague

Nice

Ajax

AEK Athens

Olympiacos

CSKA Moscow

Istanbul Basaksehir

Steau Bucuresti

Viitorul Constanta

Dynamo Kyiv

Young Boys

Club Brugge

Viktoria Plzen

MAN UNITED WAKARIBIA KUMSAINI KIUNGO WA CHELSEA!

MANUNITED MOU PLAYERS TRAININGRIPOTI zimeibuka kuwa Manchester United wanakaribia kumsaini Liungo wa Chelsea Nemanja Matic.

Mwenyewe Matic ameripotiwa kutaka sana kuungana na Meneja wa Man United Jose Mourinho ambae ndie alimrudisha tena Matic kutoka Benfica ya Ureno Mwaka 2014.

Man United wamekuwa wakiongea na Chelsea kuhusu Uhamisho huu unaomhusu Matic mwenye Miaka 28 na inaaminika Dili ya Dau linalokaribia Pauni Milioni 40 inakaribia kukamilika.

Msimu uliopita, Matic alikuwa sehemu muhimu ya Kikosi cha Meneja Antonio Conte kilichopeleka Ubingwa huko Chelsea akicheza Mechi 35 za EPL, LIGI KUU ENGLAND, kati ya 38.

Kuondoka kwa Matic kumesaidiwa hasa na Chelsea kukaribia kumsaini Kiungo kutoka AS Monaco Tiemoue Bakayoko na hilo limemfanya Conte abariki Uhamisho wa Matic.

Kwa Mourinho, kutua kwa Matic ni nafasi murua kupata Mrithi wa muda mrefu wa Kiungo Michael Carrick, ambae nae ameongezewa Mkataba wa Mwaka Mmoja, lakini pia ni kutoa mwanya kwa Paul Pogba kuwa Kiungo Mshambuliaji halisi.

Ikiwa Dili hii itakamilika, basi Matic atakuwa Mchezaji wa Pili kusainiwa na Man United katika Kipindi hiki baada ya kumsaini Victor Lindelof kutoka Benfica kwa Dau la Pauni Milioni 30.

JUVE, CHELSEA DILI YA STAA MBRAZIL!

CHELSEA imeripotiwa kufikia makubaliano na Juventus ili wamnunue Fulbeki Staa kutoka Brazil.

Alex Sandro, nwenye Miaka 26, amekuwa akihusishwa sana kuhamia Stamford Bridge hasa baada ya Meneja wao Antonio Conte kutaka Mtu wa kumpa changamoto Fulbeki wao wa Kushoto Marcos Alonso.

SANDROWiki iliyopita Mkuu wa Juve Giuseppe Marotta alitoboa wameikataa Ofa nzuri ya Chelsea wakitaka kumnunua Staa huyo alieichezea Timu ya Taifa ya Brazil mara 12.

Lakini sasa duru za Kisoka zimebaini Chelsea watamwaga Pauni Milioni 60 kumchota Sandro.

Tayari Mchezaji huyo ashakubaliana na Chelsea Maslahi yake binafsi na Mshahara wake wa Pauni 75,000 kwa Wiki huko Juve kuongezeka maradufu huko Jijini London.

Ripoti hizi za Sandro zimepata uzito Mkuu baada ya Giuseppe Marotta Jana kukiri Juve imepata Ofa kubwa mno kuhusu Sandro ambae walimsaini kutoka FC Porto ya Ureno kwa Pauni Milioni 23 Miaka Miwili iliyopita.

Marotta ameeleza: "Ofa kubwa imekuja Wiki hii. Hatuna nia kuuza Mchezaji lakini Mchezaji akiamua kuondoka, kama ilivyotokea Miaka ya nyuma, mwisho wa Siku lazima aondoke tu. Hatulazimishi Mtu kubaki!"

Mbali ya Sandro, Chelsea pia ipo mbioni kuwezesha Dili ya kumsaini Kiungo wa AS Monaco Tiemoue Bakayoko, mwenye Miaka 22, kwa Dau la Pauni Milioni 35.

Kutua kwa Mchezaji huyo wa Kimataifa wa France huko Stamford Bridge kutafungua njia kwa Kiungo Nemanja Matic kujiunga na Manchester United kama anavyowania Meneja wa Man United Jose Mourinho.

Mourinho, alipokuwa Chelsea, ndie aliemrudisha tena Matic Klabuni hapo kutoka Benfica ya Ureno.

ARSENAL YAANUA JEZI MPYA, NAMBA 7 YA SANCHEZ ANAYO WELBECK, MASHABIKI WAHOFU ‘KAUZWA’!

ARSENAL JEZI MPYALEO Arsenal wametangaza Jezi zao mpya kwa ajili ya Msimu Mpya wa 2017/18 na Danny Welbeck akaonekana ndie mwenye Namba 7 aliyokuwa akivaa Alexis Sanchez Msimu uliopita.

Matangazo yalikuwa ya kuwapa nafasi Mashabiki wa Arsenal kuona Jezi hizo Mpya na kuweka Oda ya Kununua Jezi hizo ambazo zitaanza kuwa Sokoni Julai 3.

Mashabiki walipoingia kwenye Tovuti hiyo kuchagua Jezi na wale waliochagua Jina la Danny Welbeck walishtushwa walipoona Mgongoni ipo Namba 7 iliyokuwa ya Alexis Sanchez.

Hivi sasa upo uvumi mkubwa kuwa Sanchez anataka kuhama na hili linazidi kushika kasi kwa vile hataki kusaini Mkataba Mpya wakati huu wa sasa ukiwa unaisha Mwakani.

Zipo taarifa Man City, Bayern Munich na Klabu kadhaa huko Italy zinamnyemelea huku Arsenal wakiwa wamejiwekea thamani yake kuwa ni zaidi ya Pauni milioni 50.

Mara baada ya Mashabiki kuhoji kulikoni kuhusu Jezi Mpya na Namba 7 kupewa Welbeck, haraka haraka Tovuti ya Arsenal ikamrejesha Welbeck kwenye Namba yake ya kawaida 23.

MOURINHO NAE ABURUZWA KWA PILATO KWA MADAI YA UKWEPAJI KODI!

MANUNITED MOU BLACKMENEJA wa Manchester United Jose Mourinho nae ameungana na mlolongo wa Mastaa Wachezaji Soka walioburuzwa Mahakamani huko Nchini Spain kwa tuhuma za Ukwepaji Kulipa Kodi.

Imedaiwa Mourinho amekwepa kulipa Kodi ya kiasi cha Pauni Milioni 2.9, Euro Milioni 3.3, aliyopaswa kulipa kati ya Miaka 2011 na 2012.

Mwendesha Mashitaka kwenye Mahakama ya Spain amedai Mourinho hakubainisha Mapato yake yatokanayo na Mauzo ya Umiliki wake wa Picha na Matangazo mengine.

Mashitaka ya Mourinho, mwenye miaka 54, ni Mawili ya kukwepa Kodi ya Euro Milioni 1.6 Mwaka 2011 na Euro Milioni 1.7 Mwaka 2012.

Mourinho mwenyewe hajatamka lolote kuhusu tuhuma hizi.

Mastaa wengine wa Soka walioandamwa na Kesi za aina hii ni pamoja na Cristiano Ronaldo anmbae Wiki iliyopita alifunguliwa rasmi Mashitaka kiasi cha kumuudhi na sasa ametishia kuihama Spain na kuacha kuichezea Real Madrid.

Wengine waliowahi kushitakiwa na kuhukumiwa ni Fowadi wa Barcelona, Lionel Messi, ambae alipigwa Faini na kuamriwa ende Jela Miezi 21 ingawa Kifungo hiki kinaaminika kitakuwa cha nje, na Javier Mascherano wa Barcelona aliefungwa Kifungo cha nje cha Mwaka Mmoja.