EVERTON YAICHARAZA LEICESTER, YAISHIKA ARSENAL!

=LUKAKU APIGA 2 NDIE MFUNGAJI BORA!
=LEO ARSENAL KUILAZA PALACE NA KUIRUDISHA MAN UNITED YA 6?

EPL – Ligi Kuu England

Matokeo:

Jumapili Aprili 9

Sunderland 0 Manchester United 3                 

Everton 4 Leicester City 2     

+++++++++++++++++++++++++++++++

EVERTON-LUKAKU-GOLIJANA huko Goodison Park Evrrton walitamba kwa kuitandika Leicester City 4-2 huku Straika wao Romelu Lukaku akipiga Bao 2 na kushika hatamu Mfungaji Bora EPL, Ligi Kuu England.
Matokeo haya yameiweka Everton Nafasi ya 7 wakiwa Pointi sawa na Arsenal walio Nafasi ya 6 lakini Arsenal wamecheza Mechi 3 pungufu.
Leo Arsenal wako huko Selhurst Park Jijini London kuivaa Crystal Palace na ushindi kwao utawafanya waishike Man United kwa Pointi na kukalia Nafasi ya 5 kwa Ubora wa Magoli.
Katika Mechi ya Jana Everton walitangulia kufunga Dakika ya Kwanza kupitia Davies na Leicester kujibu kwa Bao 2 za Dakika za 4 na 10 kupitia Slimani na EPL-2Albrighton.
Everton wakacharuka na kutoka nyuma kwa Bao hizo 2-1 na kupiga Bao Dakika za 23 Mfungaji akiwa Lukaku, Dakika ya 41 Jagielka na Lukaku tena Dakika ya 57.
Bao hizo 2 zimemfanya Lukaku awe na Bao 23 za EPL na aongoze kwa Bao 4 mbele ya Straika wa Tottenham Harry Kane katika Listi ya Wafungaji Bora.

EPL – Ligi Kuu England

Ratiba:

Jumatatu Aprili 10

2200 Crystal Palace v Arsenal

Jumamosi Aprili 15

1430 Tottenham Hotspur v Bournemouth                   

1700 Crystal Palace v Leicester City              

1700 Everton v Burnley     

1700 Stoke City v Hull City

1700 Sunderland v West Ham United             

1700 Watford v Swansea City               

1930 Southampton v Manchester City           

Jumapili Aprili 16

1530 West Bromwich Albion v Liverpool 

1800 Manchester United v Chelsea        

Jumatatu

2200 Middlesbrough v Arsenal       


 
 

MOURINHO AKIRI UBUTU, SARE OLD TRAFFORD ZAWATAFUNA!

>ADAI OLD TRAFFORD WAMINYWA MAAMUZI, ‘WAPINZANI DABO DEKA’!

MANUNITED-MOU-REF2HII LEO JOSE MOURINHO ametoa ujumbe tofauti kuhusu Timu yake Manchester United katika Msimu wake wa kwanza Klabuni hapo.

Mourinho amesisitiza wana Rekodi nzuri Uwanja wao wa Nyumbani Old Trafford licha kukaribia Rekodi ya Matokeo mabovu ya Mechi za EPL na pia kukiri kuwa hawako vizuri kwa kushindwa kuzibadili droo 9 walizopata hapo kwao na kuwa ushindi.

Man United wamezoa Pointi 27 kati ya 48 wakiwa Old Trafford Msimu huu.

Wakibakiza Gemu 3 za Nyumbani za EPL Msimu huu, Man United wapo hatarini kuifikia Rekodi mbovu ya Poiinti 27 tu za Nyumbani walizopata Msimu wa 2013/14 chini ya David Moyes aliesimamia Mechi 16 na Ryan Giggs Mechi 3 za mwisho.

Lakini Mourinho amedai wamepoteza Mechi 1 tu hapo Old Trafford na hilo ni jambo jema kwa wakati wa baadae huku pia akilalama kwamba Sare zao nyingi hutokana na Wapinzani ‘Kupaki Basi’ wakitua Old Trafford.

Mourinho ameeleza: “Nadhani licha ya matokeo mabovu, na kwetu Sare ni matokeo mabovu, sisi tupo imara mno Nyumbani. Kwa nini? Tumefungwa Mechi 1 tu na tunajua kwa nini tulifungwa! Kuna vitu vya ajabu vilitokea Mechi hiyo!”

Hata hivyo, Mourinho amekiri ubutu wao wakiwa wamefunga Bao 21 tu katika Mechi 16 za Nyumbani na kutoka Sare na Klabu ambazo walitarajiwa kuzifunga kama vile Stoke, Burnley, Hull, Bournemouth, West Ham na West Brom lakini pia kubanwa na Vigogo Liverpool, Everton na Arsenal.

Mourinho ametamka: “Hatuko safi au wenye nguvu kwa sababu hatushindi, hatuko safi au wenye nguvu kwa sababu hatufungi magoli tunayopaswa kufunga. Tunawapa Wapinzani na Kipa wao Tuzo za Mchezaji Bora wa Mechi mara nyingi tu!”

Aliongeza: “Narudia nlichokisema baada ya Mechi iliyopita, na hii si lawama, lakini maamuzi mengi yametuadhibu sisi, na hivyo naamini tuna nguvu Nyumbani!”

Akimalizia, Mourinho alieleza: “Tukiangalia nini tutakikuta Msimu ujao, nadhani tunajisikia vyema kwamba hatujapoteza Mechi nyingi. Ni kitu kuzuri kuona hatujafungwa katika Mechi 20, Nyumbani na Ugenini, za Ligi. Najua Sare 10 ni Pointi 10, Katika Mechi 10 ukishinda 5 na Kufungwa 5 ni Pointi 15 Nini bora? Pointi 15 lakini ukiangalia mbele ni Bora Mechi 10, Sare 10! Unakuwa ni mgumu, umekakamaa kiakili, ni mgumu kufungwa! Lakini kuwa na Pointi ndio uhalisia, ni bora uwe na Pointi 15 ukishinda Mechi 5 na Kufungwa 5! ”

JESSE LINGARD AVUNA DILI MPYA MANCHESTER UNITED!

>ANENA: ‘NAFURAHIA KUICHEZEA MAN UNITED, MOYO WANGU NI MAN UNITED!’

MANUNITED-LINGARDJESSE LINGARD anasemekana atapewa Dili mpya Klabuni kwake Manchester United ya Mkataba wa Miaka Minne na Mshahara wake kuongezeka mara 3 na kuvuna zaidi ya £100,000 kwa Wiki.

Lingard amebakiza Mwaka Mmoja kwenye Mkataba wake wa hivi sasa na Man United wamekuwa wakitaka abakie kwa muda mrefu zaidi.

Fowadi huyo mwenye Miaka 24 yupo Man United tangu akiwa na Umri wa Miaka 7 na alipewa Mkataba wake wa kwanza kama Profeshenali Mwaka 2011.

Lingard alianza kuchomoza na kubaki Timu ya Kwanza Msimu uliopita chini ya Meneja Louis van Gaal na kabla ya hapo alipelekwa kwa mkopo kwenye Klabu za Leicester City, Birmingham City, Brighton na Derby County.

Kabla habari hizi kuibuka Lingard, ambae ameanza Mechi 3 zilizopita za Man United, alithibitisha yupo mazungumzoni kuongeza Mkataba wake huku yeye akisisitiza angependelea kubakia hapo hapo.

Alieleza: “Nafurahia kuichezea Man United na Moyo wangu ni Man United!”

Lingard amebainisha kuna ushindani mkali kwenye Timu kupata namba lakini pia amekiri hilo ni jambo jema kwa Timu ambalo linakufanya ukipata nafasi basi lazima ujitume.

Amesema: “Ukiwaangalia Mkhitaryan, Zlatan, Pogba, ni Majina makubwa kwenye Timu yetu na ni vyema kuwaiga kwa yale waliyofanikiwa na ni wazi tunapata uzoefu toka kwao hasa kwa Wachezaji Chipukizi!”

MOURINHO AMSIFIA LUKE SHAW LAKINI...!!

MANUNITED-MOU-SHAWMENEJA wa Manchester United amemsifia Fulbeki wake Luke Shaw ambae Jana aliingizwa Kipindi cha Pili na kuzua Bao la kusawazisha la Dakika za Majeruhi la Timu yake walipotoka 1-1 na Everton Uwanjani Old Trafford.
Majuzi Mourinho alimponda Shaw kwa kutojituma na huku wengi wakidhani zama za Mchezaji huyo zimekwisha, Meneja huyo akamjumuisha kwenye Kikosi cha kuivaa Everton.
Jana Shaw, mwenye Miaka 21, alianza Benchi na kuingizwa Kipindi cha Pili kumbadili Ashley Young ambapo Shuti lake lililolenga Goli lilishikwa na Beki wa Everton Ashley Williams na kuzaa Penati ambayo Zlatan Ibrahimovic aliifunga katika Dakika ya 94 na kuipa Man United Sare ya 1-1.
Akiongea baada ya Mechi hiyo Mourinho alieleza: "Nishamwambia haya. Amecheza vizuri kwa kutumia mwili wake na akili zangu. Alikuwa mbele karibu yangu na nilimwamulia kila kitu. Inabidi sasa afanye bidii afanye maamuzi mwenyewe. Ni Mchezaji mzuri mwenye kipaji. Mchango wake ulikuwa mzuri na kuifanya Timu icheze vyema!"
Mbali ya Shaw, Mourinho pia alilalamikia baadhi y maamuzi ya Mechi yao.na Everton ya kukataliwa Bao zao 2 kwa Ofsaidi tata hasa lile la Ibrahimovic huku Paul Pogba na Ander Herrera wakipiga Posti.
 
 

 

LIVERPOOL HOFU, KUMKOSA SADIO MANE MSIMU WOTE ULIOBAKI?

MANE-INJUREDLiverpool wapo kwenye hofu kubwa juu ya Sadio Mane kutocheza tena Msimu huu uliobaki baada ya Jumamosi kuumia Goti kwenye Mechi waliyowachapa Everton 3-1.
Fowadi huyo kutoka Senegal ambae ndie tegemeze kubwa la Liverpool na ambae ndie aliewafungia Bao la Kwanza kwenye Mechi hiyo na Everton aliumia baada kuvaana na Leighton Baines wa Everton.
Baada ya Mechi hiyo ya Jumamosi, licha mwenyewe Mane kusisitiza yuko fiti kwa Mechi yao ya Jumatano dhidi ya Bournemouth, Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amesema hataweza kucheza Mechi ijayo.
Mane anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa kina baada uvimbe kupungua kwenye Goti lake lakini upo wasiwasi mkubwa huenda asionekane tena hivi karibuni.
Fowadi huyo anaungana na Majeruhi wengine Jordan Henderson na Adam Lallana ambao wamepelekwa.huko USA kwa matibabu zaidi.
Mchezaji mwingine alieumia kwenye Mechi hiyo na Everton ni Kiungo Emre Can ambae ameshindwa kufanya hata Mazoezi kutokana na maumivu ya Goti.
Lakini habari njema kwa Liverpool ni kuanza tena Mazoezi kwa Straika wao Daniel Sturridge ambae kitambo yuko nje kwa maumivu na upo uwezekano akawepo Benchi Jumatano wakiivaa Bournemouth.
EPL – Ligi Kuu England

Ratiba:
Jumanne Aprili 4
2145 Burnley v Stoke City          
2145 Leicester City v Sunderland          
2145 Watford v West Bromwich Albion            
2200 Manchester United v Everton     
Jumatano Aprili 5
2145 Arsenal v West Ham United         
2145 Hull City v Middlesbrough            
2145 Southampton v Crystal Palace               
2145 Swansea City v Tottenham Hotspur        
2200 Chelsea v Manchester City          
2200 Liverpool v Bournemouth             
Jumamosi Aprili 8
1430 Tottenham Hotspur v Watford               
1700 Manchester City v Hull City         
1700 Middlesbrough v Burnley             
1700 Stoke City v Liverpool                 
1700 West Bromwich Albion v Southampton             
1700 West Ham United v Swansea City          
1930 Bournemouth v Chelsea              
Jumapili Aprili 9
1530 Sunderland v Manchester United           
1800 Everton v Leicester City              
Jumatatu Aprili 10
2200 Crystal Palace v Arsenal