MAN UNITED WAAFIKIANA NA BENFICA DILI KUMSAINI VICTOR LINDELOF!

VICTOR-LINDELOFManchester United wamukubalina na Klabu ya Portugal Benfica dili ya Pauni Milioni 31 kumsaini Beki wa Kimataifa wa Sweden Victor Lindelof.

Lindelof, mwenye Miaka 22, hivi sasa yupo na Kikosi cha Sweden ambacho Ijumaa kiliifunga France 2-1 katika Mechi ya Kundi lao ya kusaka kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 zitakazochezwa Russia.

Lindelof ameichezea Timu ya Taifa ya Sweden mara 12.

Beki huyo, ambae hucheza kama Sentahafu na pia Beki wa Kulia, amekuwa na Benfica tangu Mwaka 2012 na Msimu uliopita aliichezea Benfica mara 47 na kuwasaidia kutwaa Mataji Dabo yaani Ubingwa na Kombe la FA la Portugal.

Huyu anakuwa Mchezaji wa Kwanza kusainiwa na Man United kuelekea Msimu Mpya wa 2017/18 utakaoanza Agosti 12.

Habari za Dili hii pia zimethibitishwa na Tovuti rasmi ya Man United ambayo imeeleza Dili hii itakamilika baada ya Lindelof kupimwa Afya, kupata Kibali cha Kimataifa na kuafikiana na Maslahi yake binafsi.

Habari MotoMotoZ