IBRAHIMOVIC RUKSA KWENDA, SHAKESPEARE MENEJA KUDUMU LEICESTER, KIPA EDERSON ASAINI CITY KWA £35M TOKA BENFICA!

PATA FUPI ZILIZOBAMBA:

IBRAHIMOVIC RUKSA KWENDA,

IBRA-UELManchester United wanatarajiwa kutompa Straika wao Zlatan Ibrahimovic Mkataba Mpya baada wa sasa kwisha hapo Juni 30.

Straika huyo toka Sweden mwenye Miaka 35 alisaini Mkataba wa Mwaka Mmoja wenye Nyongeza ya Mwaka Mmoja wakiafikiana, mwanzoni mwa Msimu uliopita.

Lakini Nyongeza hiyo imeshindwa kutumika baada Ya Mwezi Aprili Ibrahimovic kuumia vibaya Goti lake ambalo litamweka nje kwa muda mrefu.

Leo EPL, LIGI KUU ENGLAND, inatarajiwa kutoa Listi ya Wachezaji wa Klabu zote za Ligi hiyo ambayo itaanika nani watabakia kwenye Timu zao na nani wataondoka.

Hivyo hili la Ibrahimovic litathibitika hii Leo.

Akiwa na Man United, Ibrahimovic alicheza Mechi 46 na kufunga Bao 28 akiwasaidia mno kubeba Ngao ya Jamii, LEICESTER-SHAKESPEAREEFL CUP na UEFA EUROPA LIGI katika Msimu wa Kwanza tu wa Meneja Jose Mourinho.

SHAKESPEARE MENEJA WA KUDUMU LEICESTER!

Meneja wa Muda wa Leicester City, Craig Shakespeare, amepewa Mkataba wa Kudumu na Mabingwa hao wa zamani wa England ambao ni wa Miaka Mitatu.

Shakespeare, mwenye Miaka 53, aliteuliwa Meneja wa Muda Mwezi Februari baada ya kufukuzwa Claudio Ranieri.

Hiki ndicho kitakuwa kibarua cha kwanza kwake kama Meneja kamili baada ya kufanya kazi kama Msaidizi wa Meneja chini ya Ranieri na kabla chini ya Meneja aliepita hapo Leicester, Nigel Pearson.

Tangu ashike hatamu hapo Leicester, Shakespeare alishinda Mechi 8 kati ya 16 na kuwawezesha kuwa Timu pekee ya England kutinga Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI kabla CITY-EDERSON-DUNIAkutolewa na Atletico Madrid Mwezi Aprili.

KIPA EDERSON MORAES ASAINI CITY KWA £35M TOKA BENFICA!

Manchester City rasmi imemsaini Kipa Ederson Moraes kwa Dau la Pauni Milioni 35 kutoka Klabu ya Portugal Benfica.

Ederson, Mbrazil mwenye Miaka 23, alianza kuichezea Timu ya Kwanza ya Benfica Mwezi Machi na kuwasaidia kubeba Ubingwa na Kombe la FA Msimu ulioisha Mei.

Ederson atatambulika rasmi kama Mchezaji wa City kuanzia Julai Mosi.

Dau hili la kumnunua Ederson limevunja Rekodi ya Dunia kwa Bei ya Kipa ambalo liliwekwa Mwaka 2001 wakati Juventus ikimnunua kutoka Parma Gianluigi Buffon.

Habari hizi za Kipa huyo kusaini City pia zimethibitishwa Jana na Benfica ambao pia wametoboa kuwa Dau la kumnunua Kipa huyo Mgao wake wa Asilimia 50 utakwenda ‘Upande wa Tatu’ kitu ambacho ni tata kwa FIFA n ahata FA, Chama cha Soka England ambao Kanuni zao wanataka Mchezaji amelimikiwe na Klabu na si Klabu na ‘Upande wa Tatu’.

Hilo sasa litafanya FA, na EPL, Ligi Kuu England, wapitie Uhamisho huu na kujiridhisha unakidhi Kanuni zao na ndipo wauthibitishe.

Habari MotoMotoZ